Orodha ya wabunge bubu bungeni yawekwa hadharani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Orodha ya wabunge bubu bungeni yawekwa hadharani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtanzania, Jun 21, 2009.

 1. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hata JF kuna watu wengi tu hawachangii, je nao ni bubu?

  Orodha ya wabunge bubu bungeni yawekwa hadharani.

  Na Leon Bahati


  WAKATI tukielekea mwaka wa lala salama wa Bunge la mwaka 2005-2010, huku baadhi ya wabunge wakiibuka mashujaa kwa kutoa michango mizito inayoitingisha serikali, imebainika kuwa baadhi yao hadi sasa hawajawahi kuuliza hata swali moja wala kuchangia.

  Uchunguzi huo umefanywa na Mwananchi Jumapili kwa msaada wa tovuti ya bunge ambako kila mchango wa mbunge hurekodiwa kwa kuonyesha swali la msingi au la nyongeza alilouliza, majibu yake na mchango aliotoa.

  Kati ya wabunge 319 walioko katika Bunge la sasa ambao hawajawahi kuuliza maswali ya msingi wanakadiriwa kufikia 50 na wasiouliza maswali ya msingi wala nyongeza ni zaidi ya 30.

  Mawaziri na wabunge ambao pia ni wakuu wa mikoa, hawajahusishwa kwenye hesabu hizo kwa sababu wapo upande wa serikali na wote wamekuwa hawaulizi maswali. Wengine ambao hawakuhusishwa kwenye vipengele hivyo ni Spika na Naibu Spika, lakini wote wameonyeshwa kuwahi kuchangia hoja mbalimbali.

  Kwa mujibu wa mtandao huo, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ndiye pekee ameonyeshwa kuwa hajawahi kuuliza swali lolote wala kuchangia jambo lolote tangu Bunge limeanza.

  Wabunge wengine ambao wameonyeshwa hawajawahi kuuliza maswali, lakini wamekuwa wakichangia hoja mbalimbali nao ni Yusuf Makamba (Katibu Mkuu wa CCM); John Shibuda, Harith Mwapachu, Ali Haji Ali, Omar Sheha Musa, Abdallah Sumry, Gideon Cheyo, Juma N抙unga, Nazir Karamagi, Anna Abdalah, Ali Haji Ali, Thomas Mwang抩nda, Salum Khamis Salum, Hassan Rajabu Khatibu na Felix Mrema.

  Wengine ni Philemon Sarungi, Edward Lowassa, Andrew Chenge, Abdisaalam Issa Khatib, Dk Ibrahim Msabaha, Zakia Meghji, Kingunge Ngombale Mwiru, Salimu Yusufu Mohamed, Salum Ahamed Sadiq, Omar Sheha Mussa, Manju Msambya na Benedict Ole-Nangoro.

  Wabunge ambao pia ni wakuu wa mikoa ufanisi wao wa kuchangia bungeni ni mdogo ni Abdul Aziz ?Iringa (7); Dk James Msekela ?Dodoma (6); Monica Mbega ?Kilimanjaro (3); Dk Christine Ishengoma-Ruvuma (4) na William Lukuvi ?Dar es Salaam (3). Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliwahi kutoa michango bungeni mara mbili tu.

  Katika Kundi la wabunge 13 wanaoongoza kwa kuuliza maswali ya msingi linaongozwa na Mgana Msindai (CCM) mwenye maswali 34 na kufuatiwa na William Shellukindo (29); Diana Chilolo (28), Paschal Degera (28), George Lubelege (25), Raphael Mwalyosi (24) na Mhoga Ruhwanya (23).

  Wabunge wengine kwenye kundi hilo wana maswali 22 kila mmoja nao ni, James Msalika, Job Ndugai, Zitto Kabwe, Herbert Mtangi, Victor Mwambalaswa na Lucy Owenya.

  Wabunge 11 vinara wa kuuliza maswali ya nyongeza ni Dk Wilbrod Slaa (71), Hamad Rashid Mohamed (71), Mgana Msindai (67), Esther Nyawazwa (58), George Lubelege (56), Diana Chilolo (54), Hafidh Ali Tahir (52), Geofrey Zambi (50) na wawili waliofungana kwa kuuliza 49, Jenista Mhagama na John Kilimba (49).

  Katika kundi la kutoa michango mbalimbali kwenye vikao vya bunge linaongozwa na Naibu Spika Anne Makinda (495); akifuatiwa na Spika, Samweli Sita (494). Wengine ni Jenister Mhagama (193); Job Ndugai (147); Zitto Kabwe (125); Dk Slaa (106); Andrew Chenge (89); Suzan Lyimo (87); William Shelukindo (77); Geofrey Zambi (73); John Kilimba (69) na mawaziri wawili waliofungana kwa kufikisha michango 67 ambao ni Shamsa Mwangunga, Waziri wa Maliasili na Utalii na Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa.

  Mawaziri wengine wanaofuatia ni Dk Mary Nagu (64); Profesa David Mwakyusa (59); William Ngeleja (50); Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Johnson Mwanyika (47); Dk Makongoro Mahanga (45); Profesa Jumanne Maghembe (45); Stephen Wasira (41) na John Chiligati (40).

  Akizungumzia kuhusu kumbukumbu hizo wiki iliyopita, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema kuwekwa kwa taarifa hizo hakuna maana zaidi ya kuweka kumbukumbu za michango ya wabunge, lakini akasema kulikuwa na marekebisho kwa wakati huo.

  Alipotafutwa tena jana, alisema tovuti hiyo ya Bunge imefanyiwa marekebisho makubwa ili wananchi waweze kupata kwa undani kumbukumbu mbalimbali za vikao vya Bunge.

  Pamoja na maboresho hayo, Dk Kashililah alisema: "Tuna mpango wa kuongeza maboresho zaidi yakiwepo ya kuwezesha watu kufuatilia vikao vya Bunge kupitia tovuti hiyo."

  Licha ya baadhi ya wabunge kuwa na mchango hafifu, Bunge la sasa limeonekana kuwa mwiba mkali kwa viongozi serikalini hususan mawaziri, kutokana na baadhi ya wabunge kuwabana katika mambo mbalimbali ya utendaji mbovu na ufisadi, huku kufupishwa kwake kukipunguza nafasi ya kuuliza maswali na kuchangia kwa baadhi yao ambao walikuwa hawajafanya hivyo.

  Katika kipindi hicho miongoni mwa hoja nyingine zilizosisimua ni mjadala wa Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk Harrison Mwakyembe kuhusu utoaji wa zabuni ya umeme wa dharura iliyotolewa kwa kampuni ya Richmond Development Limited (LLC); na kusababisha Rais Jakaya Kikwete kuvunja baraza la mawaziri baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu pamoja na mawaziri wengine wawili
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  .... hapana. ni wanachama wasomaji wa jf. iwapo wanasoma na kuelewa, basi hilo linafaa tu pia.
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  SteveD,

  Hata wabunge wengine si ajabu wanakaa bungeni, wanachota yale yaliyo mazuri na kwenda kuyafanyia kazi majimboni kwao, je hao utawaita wabunge bubu?
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  kwani kuuliza swali sifa?

  wananchi wanaowakilishwa kama wanapata maji,dawa, shule,na mengineyo maswali ya nini?

  hao wanaoluliza maswali kila kukicha wamefikia wapi?
   
 5. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2009
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mi naona tuanzaze kutaja majina ...........haya naanza Mwakiembe.......
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Jun 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwa mujibu wa mtandao huo, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ndiye pekee ameonyeshwa kuwa hajawahi kuuliza swali lolote wala kuchangia jambo lolote tangu Bunge limeanza.
   
 7. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  sikazi wabunge wengine hawajui hata kazi ya mbunge ni nini.
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Dah mkuu usiseme. Mimi mbunge wa jimbo la nyumbani kakaa kuanzia 2000-2005 bila kusema wala kuchangia chochote bungeni. Haya jimboni kwetu hakuna alicho fanaya. Wakati ana gombea ubunge alikuwa ana wapa shikamoo hata watoto wadogo kushinda ubunge gari linafungwa vioo hakuna hata salamu. 2005 watu wakamkomesha aka pinduliwa. Wengi wao wanaenda tu kula mishahara na marupurupu mengine.
   
 9. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hivi wewe GT ndo Rostam Aziz mwenyewe nini?

  Unaongea utumbo kweli karibu mara zote. Hebu fikiria Bunge limekaa halafu watu wote wanakaa kimya kuna maana gani sasa ya kuwa na vikao vya Bunge? Au unaropoka tu. Hata kama si kuuliza swali basi achangie hoja za msingi za kuleta maendeleo. Yaani miaka 4 hata kufungua mdomo hakuna! Huyu jamaa yuko bungeni kwa maslahi yake binafsi tu wala hana shida na maendeleo ya wadanganyika. Yeye ni kwenda bungeni kutengeneza chanels zake za kuinyonya hii nchi tu basi. Rostam Aziz ni hatari sana kwa maendeleo ya taifa letu. He is too wicked I can say.
   
 10. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  wanokaa Bungeni bila kusema inafaa wapewe Miswaki na colgate ili wasafishe vinywa vyao maana vitakuwa vinatoa harufu mbaya sana mwishoni mwa miaka mitano yao...

  Walipoomba ridhaa za wananchi wa majombo yao sidhani kama waliwaambia kwamba wakifika bungeni watakaa kimya na hakuna kusema lolote..
  yaani si 1. kuuliza swali, 2.kuchangia au 3. kutoa hoja binafsi...
  Ya nini kuwakilisha wananchi kama huna uwezo wa matatu kati ya hayo?
   
 11. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #11
  Jun 21, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,873
  Trophy Points: 280
  I have learned to learn form others, mkuu maswali yako yanahitaji hoja hapa kwetu, maana kuna hatari ya kujenga jamii ya wasemao! kila kukicha kusema tu, na ukiwakuta wataalam wa kuongea ndio umekwisha!

  Yes kwa mujibu wa mtandao, but is this our standard to know who is best?

  Kaka nadhani una maneno mazuri lakini makali pia, anahitaji kujibiwa kwa hoja! mmoja wa wabunge that I can testify sio mmulizaji maswali ni Mwandosya, nenda jimboni kwake!

  Kuhusu Rostam, history is always good kuna wabunge wachache sana waliofikia rank yake bungeni.Kuna wachache waliofikia aliyokwisha wahi kuyafanya hebu soma hapa;

  Tusimbeze Rostam, hatikisi kiberiti

  Hiyo ni article ya Rostam kawahi kufanya nini!

  Imani yangu ya nikea juu ya ufisadi

  Mimi ni wale wanaoamini kuwa mafisadi wote wanatakiwa wawe treated equally kwa mujibu wa sheria husika. Naamini ufisadi Tanzania unaanzia kwa ndugu zangu, maboss wangu, mamesenja, na masekretari.

  Naamini kuwa CCM na serikali yake inahusika asilimia 100 kuwaachia mafisadi wengi huru.Hivyo basi nyundo yangu, hasira yangu na makombora yangu naelekeza serikalini moja kwa moja.

  Naamini kuw Rostam kama individual ni kasehemu kadogo tu ka ufisadi , kati ya ufisadi mkubwa unaoendelea nchini , kwenye mawizara ya utalii, kilimo n.k

  Naamini kuwa leo akiondoka Rostam bado ufisadi huko pale pale.Naamini kama aliiba basi alishirikiana na watanzania tunaowaita wazalendo weusi kama mimi, ambao basi ndio wabaya zaidi kuliko huyu! na ambao hatuwasemi kana kwamba walifanya jambo la kutukuka!


  Naamini kuwa wengi wenye rekodi za kutukuka kwa kuitumikia jamii, pia wengi wao ni mafisadi.

  Naamini jela ni sehemu pekee ya kuwapeleka mafisadi wote bila kujali rangi, kabila, cheo na historia zao.

  Naamini kuwa kama kuchoma moto vibaka si halali basi kumtuhumu mtu yeyote bila kuwa na uthibitisho, la kama huko basi vyombo husika vinatakiwa vichukue hatua za kisheria, kwani ni ndugu zetu na marafiki zetu

  Naamini ufisadi unahitaji dawa na sio kusingizia watu fulani na dawa ni kuiondoa CCM madarakani

  Naamini RA ni kamtu kadogo kiasi ambacho mawazo yangu na akili zangu sitakiwi kumuwazia yeye

  Naamini serikali ina nguvu mara 10000 ya Rostam na kama haimpeleki mahakamani basi HATUNA SERIKALI, na kama hatuna serikali hakuna siku huyu jamaa ataenda mahakamani, na lengo ni tuwe na serikali

  NAAMINI FISADI NAMBA MOJA NI JK .

  Naamini kuwa tukiendelea hivi tusiishie kwa ROSTAM tuendelee mpaka kwa majirani zetu, ndugu na marafiki zetu wanaotafuna nchi kila kukicha

  Naamini kuna watu wanatafuna nchii hii, tumepofushwa macho tuangalie upande mmoja tu wa RA, huku wengine wakila hela kwa stayle zile zile za kila siku!

  Imani yangu juu ya wabunge

  Tuna miaka 40 sasa tangu tupate uhuru je bado tunaamini style ya bunge, sera n.k vitatupeleka sehemu, mpaka tuamini kuwa usipouliza swali hufai??
   
 12. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii JF inaonyesha just how elementary our understandiing of the STATE is.. To be honest its worrying me... Maana kazi ya wabunge ni kuuliza maswali tuu.. kazi za kamati hakuna, bodi, uwakilishi katika pre-bill consultative seminars etc... This comes from a person who does not understand how things work... as it often seems to be the case JF sikuhizi, arguments zakisekodariiiiiiiiiiiiiiiiii sana..
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu... I beg to differ with you and agree with GT on this one; sometimes ni bora kukaa kimya na kufanya mambo bungeni kuliko kubwabwaja kutwa wakati jimbo lako halina manufaa na uwepo wako!!

  Actions speak louder than words as it is easier said than done!!
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ok kuweka records vizuri, ikumbukwe kuwa bunge hukaa kwa kipindi maalumu na hakuna muda wa kutosha wa kila mbunge kuchangia kwa maana ya kupewa maiki kutoa chenga au mchele. Kunapokosekana muda basi wabunge mbalimbali huchangia kwa maandishi na wizara husika hutakiwa kuyafanyia kazi. Hivyo basi sio kila anayeonekana mkimya bungeni basi hajachangia wapo wengine huchangia kwa maandishi..mkitaka rekodi nendeni kwenye wizara husika watawaonesha rekodi za kila mbunge na hoja aliyoitoa.
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  ..and who is JF...
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mazee ningependa ku-differ na wewe pia. Mbunge anaowajibu wa kusoma mwenendo wa serikali kwa ujumla na ku-respond. Response inaweza hata kupongeza sio lazima kukosoa tu na kudai hili au lile. Huwezi ukawa hau-respond halafu ukawa mbunge makini..the two do not walk together mazee.
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu inategemea wewe unataka kusema nini. Huyo mwandishi wa makala naona kama ni mvivu kiasi. Kuuliza maswali, au kuchangia hoja hakuna maana kuwa wewe ndio mwakilishi mzuri wa watu wako. Kuna wabunge tunawafahamu walikuwa wanaongea kila siku na wanapiga kelele kila siku lakini hakuna lolote la maana walilofanya kwa wananchi wao zaidi ya kupiga politiki. Nafahamu wabenge wengi tu ambao ni mawaziri hawajawahi kutoa hata mchango lakini ukiona wanayofanya kwenye majimbo yao utawasifu sana.
  Kuna wabunge wapiganaji kila kukicha utaona yuko wizara hii, yuko kwa katibu mkuu wa wizara hii kufanya kila analoweza kufanya kazi yake, sio kutumia vyombo vya habari kujitafutia umaarufu rahisi.
  Na yanayoongewa mengi huwa yanapita tu, tofauti na yale wanayofuatilia wapiganaji!
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  True mkuu... may i also differ with on that one?? as you rightly said, kazi ya mbunge sio kuongea tu na sio lazima asikike... most of the effective wabunges are good in submitting their hojas kwa maandishi kwasababu ya collective resposibility na culture tuliojiwekea ya kuogopa kukosoana. on the other side, hakuna haja ya kusimama na kurudia kupongeza kwa sababu tu ya kuongea

  Again, most of the effctive and influencial bunge decisions were not reached kwa vocals, watu wanawasilisha alternatively!!

  Lastly, i still believe kwamba first task ya mbunge ni kuwakilisha jimbo lake
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kazi ya mbunge sio kusikika tu kwenye kipaza sauti..lakini kusikika kwenye kipaza sauti kuna msisitizo wake pia na nadhani kuna tatizo iwapo mtu anamaliza miaka miwili hajasikika hata mara moja lazima kutakuwa na uwalakini mahala fulani.

  Kuhusu uwakilishi kwa jimboni anakotoka nakubaliana nako na napingana nako pia. Kuwakilisha ninakopingana nako ni kule kwa kung'ang'ania tu kuvutia kamba unakotoka. Uwakilishi wa namna hii hauwezi kulisaidia taifa na kila kitu kinakuwa into pieces badala ya kuwa kama one entity.Mathalan kuna sehemu huko kusini ktk pitapita yangu nilikutana na line kubwa tu ya umeme lakini nyumba zote za pembezoni hakuna hata nyumba inayotumia umeme..nilipoulizwa nikaambiwa.. aah mazee umeme uliletwa huku kisiasa na hamna mtu mwenye hela ya kuvuta umeme nyumbani kwake.. Ktk ishu kama hii ni kwamba TANESCO hapanshaka wamelamba garasa hapo na ndio maana kila siku wanalalamikia kupata hasara achilia mbali fedha ya kufidia mirija ya wafedhuli wengine. Kwa upande mwingine tunasikia kila siku makao makuu ya Kigoma Ujiji hakuna umeme wa gridi ya taifa....hapo ndipo unapoona matunda ya siasa ya kuvutia kamba unapotoka.
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,560
  Likes Received: 18,289
  Trophy Points: 280
  Niliwahi kusema kuhusu RA na Bungeni, sio tuu hajawahi kuchangia, bali kipindi anachohudhuria kikao cha Bunge, akikaa sana ni siku 3 tuu. Sijawahi kumuona zaidi ya siku 3 mfululizo. Yeye na mkono, huja Dodoma na ndege zao. ya Mkono huridi Dar kusubiri kuja kumchukua. Ya RA humsubiri hapo Airport ya Dodoma.

  RA haulizi swali lolote kwa sababu matatizo yote ya wananchi wake anayamaliza mwenywe kwa fedha yake ya mfukoni.

  Pia hachangii hoja yoyote kwa vile kichwani hamna kitu, hata ukimuona kwa macho tuu usoni, hilo utaliona wazi.

  Kuna baadhi ya wabunge hawachangii lolote kwa sababu wamesusa baada ya kukatiwa ulaji. Ila pia kuna wasio changia kwa sababu hawaoni umuhimu wowote kuchangia japo vichwani wako fiti, lakini kuna hawa wasiochangia kwa vile vichwani hawana kitu, japo pesa wanazo.
  Hivi kweli wananchi wakielimishwa kuhusu majukumu ya mwakilishi wao Bungeni, bado watawachagua mabubu?.
   
Loading...