SoC01 Orodha ya startups Tanzania na mawazo ya kuanzisha startups mpya

Stories of Change - 2021 Competition

Nijosnotes

Member
Aug 1, 2021
85
79
Habari wana Jf,
kama kichwa cha habari kinavyojeleza, lengo la uzi huu ni kuwa endelevu, kuorodhesha startups mbalimbali na mawazo mbalimbali ya kuanzisha Startups hapa Tanzania ili kuletata hamsa ya ukuwaji wateknolojia yenye kuleta faida kwa jamii yetu na ulimwengu kwaujumla.

Kwanini tuzungumzie startups na sio biashara?

Hii inabidi tutambue kwanza Startup ni nini, na inautofauti gani na biashara.

Startup:-

Startup ni kingereze ukitafuta maana kwa Kiswahili itasomeka kama anzisha, lakini ukitafuta maana kwa kingerezeza utapata maana mbili ambayo moja itakupeleka kwenye maana kama hiyo ya Kiswahili anzisha, ya pili itakupeleka kwenye maana ya kampuni au mradi mchanga ulioanzishwa kukuza bidhaa/huduma ya kipekee yenye tija kwenye soko kwa ubunifu wake[forbes].

Maana ya startup zipo nyingi lakini zote zinaendana na maana hiyo hapo juu, unaweza ku google kuangalia maana nyingine za Startup.

Tofauti ya startup na biashara:-

Startup ina lenga Zaidi kutengeneza mfumo mpya wa kibiashara wenye kutoa bidhaa/huduma za kipekee. Lengo lake ni kuliteka soko kiubunifu tofauti na lilivyo zoeleka. Tija kwanza faida baadae.
Mara nyingi startup inaangazia kutatua changamoto kwenye jamii.

Biashara ina lenga kutengeneza faida mara tu inapoanzishwa kwenye soko, lakini startup faida ni hatua ya pili kwenye lengo. Biashara inaangalia zaidi soko linachohitaji na kutumia mifumo inayokubalika wakati huo sokoni ilikusudi kupata faida mapema.

Kwa utangulizi huu natumai utakua umelewa maana ya startup kama kuna cha kuongezea tuongezee kwenye komenti.

Twende moja kwa moja kuorodhesha startup za Tanzania, iwe ya zamani, ya sasahivi, ilianzishwa ikafa zote unaweza kuorodhesha kwa maelezo kidogo ilitupate mwanga kuifahamu. Kama unawazo/mawazo yakuanzisha startup yaweke hapa pia sio zambi kwasababu binadamu uwa tuna mawazo mengi lakini sio lazima yote tuyafanyie kazi unaweza kugawia wenzako hapa wakaleta manufaa kwajamii yetu.

Orodha yangu ya Startups Tanzania.

1. Clouds Media Group ( zamani )
clouds1.jpg

founders (waanzilishi): Joseph kusaga C.E.O na marehemu Ruge Mtahaba mkurugezi wa vipindi .
Kuanshishwa: mwaka 1998

Ni chombo cha habari Tanzania kilicho leta mapinduzi kwenye sekta ya burudani. Walianza na Redio CloudsFM mwaka 1998, ni moja kati ya redio za kwanza kupaisha mziki wa bongo fleva kitaifa na kimataifa. Namna yake ya kuajiri watangazaji kwa kuangalia kipaji na ubunifu Zaidi ya vyeti umekua mfano wa kuigwa hadi sasa. Waanzilishi wakati huo walikua na umri mdogo(vijana) kulinganisha na wenzao waliowatangulia kwenye sekta ya habari. Imeleta maendeleo makubwa kwa vijana hasa kufanya mziki na burudani kama biashara. Clouds Media Group sasa ina miliki vituo cha Televisheni CloudsTV, Clouds Plus, Clouds Rwanda, Clouds Botswana na vituo kadhaa vya redio kama coconutfm ya zanzibar na Choicefm. SLogan: Redio ya watu na Tunakufungulia dunia.
Mytake: kuna uhaba wa historia ya Clouds Media Group kwa maandishi.
kusaga1.jpg

Marehemu Ruge Mtahaba na Joseph Kusaga

Historia ya clouds (video)



2. Jamiiforums
jamii.png

Founders(waanzilishi): Maxene melo C.E.O na Mike Mushi co founder
Kuanzishwa: mwaka 2006 kama jamboforums

Ni mtandao wakijamii kwenye mfumo wa majukwaa (forums), ulianzishwa kama jamboforums mwaka 2006 na baadae 2008 kubadili jina na kuitwa jamiiforums. Ni mtandao wa kijamii namba moja Tanzania na afrika maishariki wenye maudhui ya Kiswahili. Mbali na kupata misukosuko mwaka 2008 Maxence Melo na Mike Mushi kukamatwa kwa makossa ya kijinai kwaajili ya harakati za kisiasa kwenye mtandao wao, ambapo walishinda kesi na mwaka 2016 kufikishwa mahakamani kwa makossa ya kimtandao na kuto sajiliwa Tanzania, bado jamiiforums imekuwa msaada mkubwa sio tu kwa wanaharakati huru bali kwa wafanya biashara na sekta ya burudani kwaujumla. Slogan: "Where we dare to talk openly".
max.jpg

Maxence Melo na Mike Mushi

Historia ya jamiiforums (VIDEO)

<center><iframe width="560" height="315" src="https://www.youtube.com/embed/0fnYdOsEh1o" title="YouTube video player" frameborder="0" allow="accelerometer; autoplay; clipboard-write; encrypted-media; gyroscope; picture-in-picture" allowfullscreen></iframe></center>

3. MillardAyo
logomillard.png

Kuanzishwa: mwaka 2010
Founder(mwanzilishi): MillarAyo

Ni kampuni ya habari yenye lengo la kutoa habari za uhakika na kwa wakati(breaking news) mtandaoni, ilianza kama blog millardayo .com baadae ikaja online tv Ayotv. Millardayo imeleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya habari mtandaoni mpaka kupelekea kupata tuzo ya kuwa media yenye watazamaji wengi Afrika kwenye mtandao wa youtube. Kwa mujibu wa millardayo miongoni mwa watu waliomshawishi kuanzisha blog ni wasanii wa hiphop Tanzania mwanaFA na AY. Millard Ayo alianza kazi ya utangazaji akiwa na umri wa miaka 18 tu, historia yake mpaka kufikia hatua ya kuanzisha tovuti [millardayo .com] na online Tv[AyoTV] inayo amnika zaidi Tanzania na Afrika kwa ujumla ni ya kusimumua na kuamasisha zaidi.
Soma Zaidi kuhusu millardayo www.millardayo .com/bio
millard.jpg

Millard Ayo


Historia ya MillardAyo (VIDEO)

<center><iframe width="560" height="315" src="https://www.youtube.com/embed/yr6iZPKMSxI" title="YouTube video player" frameborder="0" allow="accelerometer; autoplay; clipboard-write; encrypted-media; gyroscope; picture-in-picture" allowfullscreen></iframe></center>


4. Kopagas
kopagas.png

Founder(mwanzilishi): Andron Mendes
Kuanzishwa: mwaka 2016

Kopagas ni watengenezaji wa mfumo wakulipia Gas ya LPG kadiri unavyotumia. Andron Mendes ameuza patent ya mfumo huu kwa kampuni ya Uingereza Cyclegas Tsh. Bilioni 57. NI miongoni mwa startup zilizouzwa kwa bei ghari Zaidi Tanzania. Unanunua gas kama unavyo nunua luku ya umeme.
andron.jpg

Andron Mendes

Historia ya Kopagas (Video)

<center><iframe width="560" height="315" src="https://www.youtube.com/embed/8dYX7hApIkQ" title="YouTube video player" frameborder="0" allow="accelerometer; autoplay; clipboard-write; encrypted-media; gyroscope; picture-in-picture" allowfullscreen></iframe></center>

WAZO LANGU LA STARTUP
DigitalTour:-
Kuanzisha kampuni ya kitalii itakayo kuwa inatembeza watalii kwa kutumia Virtual Reality(VR). Yani mtalii anakuja ofisini (kwenye hiyo kampuni ya kitalii) anavaa miwani ya VR kisha anaanza kuona video zilizo rekodiwa kwa kutumia camera za 360 zinzazo onesha sehemu usika ya kutalii kama ni serengeti, Bujora, Manyara, n.k
wanaweza kuwa anatembea pia kwenye hicho chumba kidogo ofisini na akajiisi kabsa yupo serengeti ama manyara anatembea. sio tu mbuga mtu anaweza kutembelea nchi mbalimbali hku amekaa kwenye ofisi za Digital Tour. .... Chamuhimu nukuchukua video nzuri za 360.

Karibuni sana wadau tuoredheshe Startups kwenye komenti hapo chini maelezo kidogo tupate kuitambua, hii ni kwamnufaa yetu watanzania inabidi tuwekeze zaidi kwenye teknolojia ilikusudi tuweze kutatua changamoto zetu sisi wenyewe.

Startups ni kipimo namba moja cha kuangalia ukuaji wa teknolojia nchini, inabidii tuwe na startups nyingi kadri tuwezavyo ulikukuza teknolojia nchini lakini pia kupunguza changamoto ya ajira kwani makampuni makubwa yatazaliwa humo.

NB: kama umependezwa na uzi huu husisahau kubonyeza kimshale hapo chini cha ku VOTE

kopagas.png
 
download.jpeg

Edwin Bruno C.E.O and founder Smartcodes

Smartcodes
Ni startup iliopata umaarufu kwa kuuza app yao ya kusoma magazeti M-paper kwa kampuni ya simu Tanzania Vodacom mwaka 2010.

Smartcodes inajihusisha zaidi na maswala ya uwaka kidigitali (digatal Agency) ikiwa pamoja na masoko mtandaoni, lakini pia inasaidia startups zingine kukua kupitia kampuni yao ya smartlab na smartstudio.

Smartcodes imefanya na inaendelea kufanya kazi na makampuni makubwa kama Vodacom, Heineken n.k

Ofisi zao zinapatika Mikocheni, Senga Road.
 
George-Akilimali-Profile-2020.jpg

George Akilimali ........ co founder Smartcore

Smartcore ni startup ya kitanzania inayo jiusisha na ufundishaji kupitia njia ya mtandao.

Startup hii inamakao yake makuu jijini Arushi, inafahamika zaidi kwa app yake yakufundisha kwanjia ya mtandao inayo itwa "Kisomo". Kisomo App inatumia teknolojia ya kisasa kufundisha kama vile Artifical Intelligency, Virtual reality na Machine Learning.

Inaufadhili wa makampuni makubwa kama Vodacom na taasisi kama Udom. Soma zaidi kuhusu smartcore kupitia website yao smartcore .co.tz
 
Tanzania ya leo imekuwa na vijana wengi wanaothubutu kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii zetu kwa kutumia teknolojia na ubunifu, tusaidiane kutaja watu hao na jinsi project zao zinavyosaidia jamii.
 
Tunzaa app ni moja ya startup pia, ambapo app hii inamsaidia mteja wa bidhaa za elektroniki kulipia bidhaa kwa awamu bila utapeli.

sijapata taarifa zake zakutosha lakini nimoja ya startup ya kujivunia Tanzania
 
Back
Top Bottom