Orodha ya open spaces zilizojengwa

tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,193
1,434
moja ya matatizo sugu nchini Tanzaniz kama zao la rushwa ni kuuzwa kwa viwanja vya wazi. kadri siku zinavyosonga mbele, viwanja hivi vinaisha. Nahofia watoto wetu hawatakuta viwanja vya wazi vya michezo kama vilivyokuwepo wakati wetu. Viwanja hivi havikuwa wazi kwa sababu ya kukosa kitu cha kufanyia bali vilikuwa wazi kwa malengo maalum ya mipango miji kama bustani za wazi, kuchezea watoto na kupitishia/kutengenezea hewa nzuri/upepo. Ila inasikitisha sana, siku hizi has kuanzia awamu ya pili watu wamejiona wao ndio wanajua kujenga.
Leo natoa mfano mmoja ninaoukumbuka, naomba wengine waongezee orodha yao
Mtoni kwa azizi ali ambapo sasa kuna keep-left pale njia panda ya temeke,mbagala, uhasibu na kwa kabuma kulikuwa na open space nzuri sana sana sana. open space hiyo sasa imejengwa Filling Station. Inasemekana alihonga viongozi wadogo (ofisi ya CCM wilaya na halmashauri0 akapigwa stop then akahonga juu (makao makuu ya CCM Dodoma na wizara ya ardhi HQ) akamilikishwa. Hapo zamani, watoto wengi kama si wote wa maeneo ya karibu (kwa kombo, mwembe madafu, kwa kabuma, sifa, mtongani) tulikuwa tunakutana pale kucheza maana kulikuwa na facilities zote za mnichezo...si watoto tu hata watu wazima maana kulikuwa na vivuli vizuri na upepo mzuri sana
 
Pale kisutu kuna jengö la gorofa kadhaa limeziba barabara: ukitoka peacock hotel kuelekea soko la kisutu, mwanzo wa soko kaibu na banda la kuchinjia kuku, mahali hapa zamani kulikuwa na mtaa sambamba na mtaa unaotokea kariakoo. mahali hapa pamejengwa jengo refu limeziba mtaa wote.
 
jamani mimi nazipenda sana open space lakini nina maslahi nazo, inaniuma sana nikifikiria itavyochukuliwa
 
Hivi vilikwenda zamani lakini. Mjini Mwanza open space kwenye kiwanja cha golf. Viwanja vilitolewa kimbinu hapo.
 
mama tibaijuka...chadema wanakukubali kwa kazi uifanyayo...hapa wanakuorodheshea sehemu za kupambana nazo ili urejeshe heshima ya CCM ambayo wachache walianza kuipoteza....BIG UP MWANA-MAHESABU
 
Ukienda MWenge kijijini... wilaya ya kinondoni utakuta madudu ya miaka

Kile ni kijiji cha mfano kilijengwa na nguvu ya mpango bora wa mwaka 1974, ni kijiji pekee cha makazi kilichokuwa na kila kitu kama modern area lakini ushirika wa mwenge ukiongozwa na bwana mmoja anayeitwa Mosha umeharibu mpango, umeuza open spaces zaidi ya ishirini, umeruhusu mabanda ya mama ntilie hadi sehemu za njia na watoto kucheza

suala limeshapelekwa sana kwa halmashauri lakini wakihongwa hata alfu hamsini wanafunika kombe
 
Kuna uwanja wa UFI club ambao Lowassa aliuuza kwa mwekezaji na akajenga ukuta haraka haraka huku wajenzi wakiwa chini ya ulinzi mkali na bunduki juu. Kuchukuliwa kwa uwanja huu lilikuwa ni pigo kwa wakazi wa Ubungo kisiwani, Ubungo Maziwa na Mabibo Shungashunga. Kuna haja ya kuangalia mazingira ya kuchukuliwa kwa uwanja. Kwa sasa eneo lote lile kuanzia Ubungo TANESCO mpaka Mabibo Shunga shunga hakuna eneo lolote la wazi na watoto hawana hata sehemu moja ya kuchezea!!!

Hapo awali uwanja huu ulikuwa unamilikiwa na kiwanda cha UFI ambacho baadae kiliuzwa kwa mwekezaji. Sioni kama kulikuwa na sababu ya kuuza uwanja kwa mwekezaji vile vile kwani uwanja ulikuwa open kwa public.

Tiba
 
Back
Top Bottom