Orodha ya Mataifa fisadi zaidi Africa Mashariki

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Baada ya waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kunaswa na kamera akiidunisha Nigeria kuwa mafisadi wakuu kote duniani BBC imeamua kuangazia kwa umakini ikiwa matamshi hayo ni ya kweli.
Je Nigeria imeorodheshwa katika nafasi ipi katika orodha ya mataifa fisadi kwa mujibu wa shirikisho la kupambana dhidi ya ufisadi duniani Transparency International ?
Tanzania inaorodheshwa katika nafasi ya 117 duniani

Ni vigumu kuelezea kwa kina ama hata kupiga msasa ufisadi katika mataifa kwani kila mwanauchumi anaelezea ufisadi akitumia mizani tofauti na mwenziye.

Kwa sababu hiyo tutatumia orodha ya mwaka wa 2015 ya shirikisho la kupambana dhidi ya ufisadi, Transparency International, ili kukupa taswira ya mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki na jinsi yanavyolinganishwa na mataifa mengine duniani katika mizani ya ubadhirifu na wizi wa mali ya uma.
Cha mno hata hivyo sharti tuweke bayana kuwa Nigeria sio taifa fisadi zaidi duniani.

Nigeria imeorodheshwa katika nafasi ya 136 Nigeria kati ya mataifa 167.
Kenya kwa mfano inasemekana kuwa na ufisadi mkubwa hata kuishinda Nigeria.

Zimbabwe wanaorodheshwa katika nafasi ya 150 duniani kwa ufisadi.
Katika kanda ya Afrika Mashariki , mali ya umma inafujwa sana na viongozi wa serikali hali ambayo inaiweka mataifa ya kanda katika nafasi za mwisho mwisho kuashiria viwango vya juu vya ufisadi.
Kati ya mataifa kumi Fisadi zaidi duniani Somalia inaongoza ikifwatwa na Sudan ,Sudan Kusini, Eritrea, Burundi, DRC, Uganda, Kenya Tanzania Ethiopia na kisha Rwanda katika usanjari huo.
Somalia inaongoza kwa Ufisadi duniani katika nafasi ya 167.

Viwango vya ufisadi
vinanasibishwa na Korea Kaskazini.
Nchi iliyojitenga kabisa na ufisadi kanda ya Afrika Mashariki na kati ni Rwanda.

Rwanda inaorodheshwa katika nafasi ya 44 duniani.
Taifa hilo linaloongozwa na rais Paul Kagame linaorodheshwa katika nafasi ya 44 duniani.
Je unakumbuka rais Robert Mugabe aliyewadunisha wakenya kwa kuwa wezi?

Kulingana na orodha hii iliyotayarishwa na shirika la TI Zimbabwe wanaorodheshwa katika nafasi ya 150 duniani kwa ufisadi.
Wanagawana nafasi hiyo na Burundi.

Orodha ya mataifa 10 fisadi zaidi kanda ya Afrika Mashariki na Duniani.
1. 167 Somalia / North Korea
2. 165 Sudan
3. 163 South Sudan/ Angola
4. 154 Eritrea/Yemen / Turkmenistan / Syria
5. 150 Burundi / Zimbabwe
6. 147 Democratic Republic of the Congo / Chad / Myanmar /
7. 139 Kenya / Uganda
8. 117 Tanzania
9. 103 Ethiopia
10. 44 Rwanda
 
Not surprising, ila ukiangalia kwa makini nchi zote hizo aidha zina migogoro ya kiuchumi, U communist, Vita vya wenyewe kwa wenyewe au ni nchi duni zinazosigana na maslahi ya "money printers" , Kenya was definetely, ila hata sisi?......ngoja tuone after 10yrs tutakuwa wapi, maana ni juzi tu tumetoka kwenye shamba la bibi.
 
Why not Rwanda?
Hahaha...huwezi kuilinganisha Rwanda na Korea ya Kaskazini kwenye maswala ya kimataifa!! North Korea imejitenga sana...tena hasa na mataifa ya kimagharibi...na Mara nyingi hizi international institutions nyingi ni za kimagharibi...na wanafanya mambo mengi kwa kushirikiana na hayo mataifa ya magharibi...na ni vigumu kwenda against them. Ingawa north Korea inawekwa kwenye ranking kama hivyo...bado ni vigumu kuamini kama hizo data/info ni za kweli...maana hiyo nchi imejitenga sana!¡! Ila pia ...watu Wa international relation watanena. Ila wakiwa Pro..Russia au pro..USA lazima watatoa data ambazo ni biased!!
 
Hawana lolote hao...it is just because the institution dealing with preparing those reports is western based!! Nothing more and nothing less brother!!!
Serikali yao hawa Waingereza ndiyo mafisadi.

The British arms and aircraft firm BAE Systems has been severely criticised by a UK parliamentary inquiry into a corruption case surrounding an air-traffic-control deal with Tanzania.MPs accused BAE of unilaterally setting up a compensation arrangement for Tanzania that was a "complete sham".BAE admitted to not keeping full accounting records of £8m ($12m) it paid to an agent who brokered the deal.After a plea bargain, it was not found guilty of any wider corruption charges.The controversy relates to the supply in 1999 of an air-traffic radar control system.But it could also be a test case for campaigners who say bribery and corruption are a brake on economic development.In a plea bargain with the prosecuting authorities, the Serious Fraud Office, BAE agreed to pay £30m to the Tanzanian people.
 
Back
Top Bottom