buswelu moja
JF-Expert Member
- Aug 24, 2014
- 226
- 147
Siku chache Mara baada ya Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, James Ole Milya kuibua tuhuma kwamba mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti anapokea rushwa kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara mbalimbali wa madini ya Tanzanite kwa lengo la kuwafichia madudu afisa madini mkoani Manyara, Daud Ntalima ametaja hadharani majina ya wafanyabiashara hao huku akiwataka waripoti ofisini kwake siku ya jumatatu Novemba 4.
Ole Milya aliibua tuhuma hizo mbele ya Waziri wa madini, Dotto Biteko kwamba Rc Mnyeti anapokea rushwa kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaotuhumiwa kutorosha madini ya Tanzanite Kama njia ya kuwafichia madudu yao.
Aliwataja baadhi ya wafanyabiashara hao kuwa ni Husein Gonga, Feisal Shabhai na Oleshangiki Mulla.
Jana katika mkutano ulioitishwa na afisa madini mkoani humo alitaja orodha ya wafanyabiashara wanaoficha madini na wengine kujihusisha na otoroshaji kuwa wako 25 na baadhi yao wanaficha shehena ya madini kwenye majumba yao kama njia mojawapo ya kuhujumu soko la madini hayo.
Mbali na kutaja majina hayo pia aliwataka wafike ofisini kwake wiki ijayo kwa mahojiano huku akisema kwamba wamekuwa wakipanga bei na kusumbua soko kana kwamba nchi hii ni ya wajomba wao.
"nawaambia madini yote yatarudi tu wamekuwa wakipanga bei na kusumbua soko la madini ya Tanzanite jumatatu nawataka ofisini na kila mmoja nitamwambia ameficha ndani kiasi gani lazima tufuate taratibu za nchi kwani hii nchi sio ya wajomba zenu "alisema Ntalima
Aliwataja kwa majina wafanyabiashara hao kuwa ni Husein Gonga, Feisal Shabhai, Oleshangiki Mulla, Rajan Verma, Peter Pereira, Bimel, Sailesh Pandit, Rakesh, Husein Lemari, Sunda, Saitoti, Tarimo, Vimel, Sunil, Reno, na wengine mbalimbali.
Alisema kwamba ana ushahidi kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wameficha madini hayo kwenye majumba yao na atakwenda kuwaumbua endapo wasiporipoti ofisini kwake siku ya November 4.
Husein Gonga na Feisal Shabhai wanamiliki kampuni ya Tanzanite One ambayo shughuli za uzalishaji zimesitishwa mpaka pale watakapolipa kodi ya serikali ambapo mwaka jana walikamatwa na kisha kupelekwa jijini Dar es salaam kwa mahojiano.
Hatahivyo, Rajan Verma mmiliki wa kampuni ya Crown Lapidary ni miongoni mwa wafanyabiashara ambao wanashikiliwa na vyombo vya dola tangu wiki iliyopita jijini Dar es salaam kwa madai ya kukwepa kodi serikalini pamoja na kujihusisha na utoroshaji wa madini ya Tanzanite .
Mwisho