Orodha ya majina ya wafanyabiashara 25 wanaoficha madini ya Tanzanite majumbani hii hapa, waitwa nov 4 ofisi ya madini Mererani

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
147
Siku chache Mara baada ya Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, James Ole Milya kuibua tuhuma kwamba mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti anapokea rushwa kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara mbalimbali wa madini ya Tanzanite kwa lengo la kuwafichia madudu afisa madini mkoani Manyara, Daud Ntalima ametaja hadharani majina ya wafanyabiashara hao huku akiwataka waripoti ofisini kwake siku ya jumatatu Novemba 4.

Ole Milya aliibua tuhuma hizo mbele ya Waziri wa madini, Dotto Biteko kwamba Rc Mnyeti anapokea rushwa kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaotuhumiwa kutorosha madini ya Tanzanite Kama njia ya kuwafichia madudu yao.

Aliwataja baadhi ya wafanyabiashara hao kuwa ni Husein Gonga, Feisal Shabhai na Oleshangiki Mulla.

Jana katika mkutano ulioitishwa na afisa madini mkoani humo alitaja orodha ya wafanyabiashara wanaoficha madini na wengine kujihusisha na otoroshaji kuwa wako 25 na baadhi yao wanaficha shehena ya madini kwenye majumba yao kama njia mojawapo ya kuhujumu soko la madini hayo.

Mbali na kutaja majina hayo pia aliwataka wafike ofisini kwake wiki ijayo kwa mahojiano huku akisema kwamba wamekuwa wakipanga bei na kusumbua soko kana kwamba nchi hii ni ya wajomba wao.

"nawaambia madini yote yatarudi tu wamekuwa wakipanga bei na kusumbua soko la madini ya Tanzanite jumatatu nawataka ofisini na kila mmoja nitamwambia ameficha ndani kiasi gani lazima tufuate taratibu za nchi kwani hii nchi sio ya wajomba zenu "alisema Ntalima

Aliwataja kwa majina wafanyabiashara hao kuwa ni Husein Gonga, Feisal Shabhai, Oleshangiki Mulla, Rajan Verma, Peter Pereira, Bimel, Sailesh Pandit, Rakesh, Husein Lemari, Sunda, Saitoti, Tarimo, Vimel, Sunil, Reno, na wengine mbalimbali.

Alisema kwamba ana ushahidi kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wameficha madini hayo kwenye majumba yao na atakwenda kuwaumbua endapo wasiporipoti ofisini kwake siku ya November 4.

Husein Gonga na Feisal Shabhai wanamiliki kampuni ya Tanzanite One ambayo shughuli za uzalishaji zimesitishwa mpaka pale watakapolipa kodi ya serikali ambapo mwaka jana walikamatwa na kisha kupelekwa jijini Dar es salaam kwa mahojiano.

Hatahivyo, Rajan Verma mmiliki wa kampuni ya Crown Lapidary ni miongoni mwa wafanyabiashara ambao wanashikiliwa na vyombo vya dola tangu wiki iliyopita jijini Dar es salaam kwa madai ya kukwepa kodi serikalini pamoja na kujihusisha na utoroshaji wa madini ya Tanzanite .

Mwisho
IMG_20191101_163431_082.JPG
IMG_20190719_115334.jpeg
 
Insanity! Sasa kama wameficha si ukawakamate kwa kushtukiza badala ya kuwapa nafasi ya kuyaondosha kule walikoyaficha na kupoteza ushahidi?

Maigizo mengine ya kitoto sana.
____________________________________
IG: @marble_na_granite
 
JPM sijui anakwama wapi? Alitaka kudhibiti korosho ikabuma watu mpka leo wanadai, amajenga ukuta wa mabilioni kudhibiti Tanzanite bado haileti tija, lakini kama nimeamua kuyahifadhi madini yangu nyumbani kusubiri muda nitakao kuuza ni kosa? Yaani nikichimba nikayauze chap chap kama yana augonjwa wa kuambukiza?! kazi basi.
 
Mwisho View attachment 1250978View attachment 1250980
.mkuu kwenye mkutano nlikuepo RC hakuepo,istoshe huyu rmo anaongea kwa ubabe sana kana kwamba hayo madini mali yake yeye,mtu ametoa production mgodini kwake kodi amekulipa unataka pia umpamgie matumizi ya tanzanite yake,kwani akiweka kwenye safe yake na kuamua ntauza 2021 yeye inamhusu nini.
Biashara hii ya tanzanite imekua ngumu sana kwasasa bei imeshuka mpka laki 6 kwa gram.
Badala ya kusimamia kazi yake analeta masharti kama anatoa fedha kuhudumia mgodi,navyoongea sasahivi ukiuza niwe la gram 200 kupata cash utasubiria hata wiki mbili ndio ulipwe hakuna mzunguko wa pesa kabisa
 
Huku hali mbaya sana watu wana madini ila wanunuzi hawana cash wanakopa sana,mtu mwenye production mgodini kwake mfano gram 2000 hawezi kupata mtu wa kununua gram hizo kwa cash atalipwa kwa mafungu ya kutosha
 
Mwanzoni ilikuwa sh ngapi kwa gram?
 
Swala la kutorosha sidhani kama litawezekana kwani maafisa usalama lazima watakuwa underway,cha msingi ni hicho labda cha kuwa wameyaweka majumbani mwao wakisubiria bei zipande ndio wayauze,hapo ndio sijui sheria ikoje...
 
Siku chache Mara baada ya Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, James Ole Milya kuibua tuhuma kwamba mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti anapokea rushwa kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara mbalimbali wa madini ya Tanzanite kwa lengo la kuwafichia madudu afisa madini mkoani Manyara, Daud Ntalima ametaja hadharani majina ya wafanyabiashara hao huku akiwataka waripoti ofisini kwake siku ya jumatatu Novemba 4.

Ole Milya aliibua tuhuma hizo mbele ya Waziri wa madini, Dotto Biteko kwamba Rc Mnyeti anapokea rushwa kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaotuhumiwa kutorosha madini ya Tanzanite Kama njia ya kuwafichia madudu yao.

Aliwataja baadhi ya wafanyabiashara hao kuwa ni Husein Gonga, Feisal Shabhai na Oleshangiki Mulla.

Jana katika mkutano ulioitishwa na afisa madini mkoani humo alitaja orodha ya wafanyabiashara wanaoficha madini na wengine kujihusisha na otoroshaji kuwa wako 25 na baadhi yao wanaficha shehena ya madini kwenye majumba yao kama njia mojawapo ya kuhujumu soko la madini hayo.

Mbali na kutaja majina hayo pia aliwataka wafike ofisini kwake wiki ijayo kwa mahojiano huku akisema kwamba wamekuwa wakipanga bei na kusumbua soko kana kwamba nchi hii ni ya wajomba wao.

"nawaambia madini yote yatarudi tu wamekuwa wakipanga bei na kusumbua soko la madini ya Tanzanite jumatatu nawataka ofisini na kila mmoja nitamwambia ameficha ndani kiasi gani lazima tufuate taratibu za nchi kwani hii nchi sio ya wajomba zenu "alisema Ntalima

Aliwataja kwa majina wafanyabiashara hao kuwa ni Husein Gonga, Feisal Shabhai, Oleshangiki Mulla, Rajan Verma, Peter Pereira, Bimel, Sailesh Pandit, Rakesh, Husein Lemari, Sunda, Saitoti, Tarimo, Vimel, Sunil, Reno, na wengine mbalimbali.

Alisema kwamba ana ushahidi kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wameficha madini hayo kwenye majumba yao na atakwenda kuwaumbua endapo wasiporipoti ofisini kwake siku ya November 4.

Husein Gonga na Feisal Shabhai wanamiliki kampuni ya Tanzanite One ambayo shughuli za uzalishaji zimesitishwa mpaka pale watakapolipa kodi ya serikali ambapo mwaka jana walikamatwa na kisha kupelekwa jijini Dar es salaam kwa mahojiano.

Hatahivyo, Rajan Verma mmiliki wa kampuni ya Crown Lapidary ni miongoni mwa wafanyabiashara ambao wanashikiliwa na vyombo vya dola tangu wiki iliyopita jijini Dar es salaam kwa madai ya kukwepa kodi serikalini pamoja na kujihusisha na utoroshaji wa madini ya Tanzanite .

Mwisho View attachment 1250978View attachment 1250980
sirudishi kitu mimi
 
Insanity! Sasa kama wameficha si ukawakamate kwa kushtukiza badala ya kuwapa nafasi ya kuyaondosha kule walikoyaficha na kupoteza ushahidi?

Maigizo mengine ya kitoto sana.
____________________________________
IG: @marble_na_granite
Kwa mazingira yalivyo, amini usiamini hizo nyumba za hawa jamaa tayari kuna watu wamesha take cover wakirogwa tu kuyatoa yana kamatiwa gatein na mzigo wote unakua mali ya serikali. Hakuna mzigo utakao toka hapo usofikiri watu ni wajinga kiasi ambavyo unafikiri. Hawezi tangaza hivyo halafu hajaweka mitego, hapo drones zinafanya kazi, jiulize huo ujasiri wa kutaja hayo majina, hapo serilali ina mkono wake tayari
 
Huku hali mbaya sana watu wana madini ila wanunuzi hawana cash wanakopa sana,mtu mwenye production mgodini kwake mfano gram 2000 hawezi kupata mtu wa kununua gram hizo kwa cash atalipwa kwa mafungu ya kutosha
Halafu akigoma kukopesha akaweka mzigo wake nyumbani anaitwa kwenda kujieleza kwa wakubwa? Ajanu sana yaani mtu achimbe kwa garama zake halafu achezee tu madini yake asitafute faida? Hawa watu wameharibu kila sekta.
 
Kwa mazingira yalivyo, amini usiamini hizo nyumba za hawa jamaa tayari kuna watu wamesha take cover wakirogwa tu kuyatoa yana kamatiwa gatein na mzigo wote unakua mali ya serikali. Hakuna mzigo utakao toka hapo usofikiri watu ni wajinga kiasi ambavyo unafikiri. Hawezi tangaza hivyo halafu hajaweka mitego, hapo drones zinafanya kazi, jiulize huo ujasiri wa kutaja hayo majina, hapo serilali ina mkono wake tayari
Insanity!, si wanayaweka hata chini ya ulimi na kuyaondosha kidogo kidogo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom