Orodha mpya ya nchi "salama" zilizoruhusiwa safari

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,321
11,313
Mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana juu ya kile yanachokiita “orodha salama” kwa mataifa 14 ambayo yataruhusiwa kwa safari zisizo muhimu kuanzia Julai, huku Marekani ikiwa haimo kwenye orodha hiyo.

Baraza la Umoja wa Ulaya limesema hapo jana kwamba nchi hizo salama ni Algeria, Australia, Canada, Georgia, Japan, Montenegro, Morocco, New Zealand, Rwanda, Serbia, Korea Kusini, Thailand, Tunisia na Uruguay.

Kundi hilo la mataifa 27 linatazamiwa kutoa muongozo unaolegeza au kuruhusu safari za matembezi ama kibiashara kuanzia kesho leo Jumatano kwa mataifa hayo.

Urusi na Brazil, kama ilivyo Marekani, hazikukidhi vigezo vya mataifa yaliyo salama kutokana na janga la COVID-19.

Uamuzi huu unakusudia kuunga mkono sekta ya usafiri na utalii barani Ulaya, hasa kwa mataifa ya kusini, ambayo yameathirika vibaya na janga la korona.
 
Mmeona matokeo ya kutochukulia corona serious? Rwanda wana kesi +1000, Tanzania kesi 409 lakini Rwana inachukuliwa kama nchi salama kwani wameonesha weledi mkubwa na kuwa serious kuliko Tanzania ambayo imekataa kutoa takwimu.

Nilisema huu ujinga utatuliza na watu hawakunielewa, sasa angalia watalii hawatakuja na ndio jiwe na wenzake watajua nini maana ya uongozi bora na udikteta.
 
Sisi tutakua wa mwisho yaani covid ikiisha duniani kote ndio tz itatangazwa Kama sehemu salama kwa watalii.
 
Kama US mwenyewe kapigwa chini (kwa madai nchi yao si salama kwa covid) sisi ni nani kwani?
 
Mmeona matokeo ya kutochukulia corona serious? Rwanda wana kesi +1000, Tanzania kesi 409 lakini Rwana inachukuliwa kama nchi salama kwani wameonesha weledi mkubwa na kuwa serious kuliko Tz ambayo imekataa kutoa takwimu. Nilisema huu ujinga utatuliza na watu hawakunielewa, sasa angalia watalii hawatakuja na ndio jiwe na wenzake watajua nini maana ya uongozi bora na udikteta.
Jambo jipya la kutalii limeibuka hapo kwanini tz hakuna korona tuna expect utalii mwingi sana kuhusiana na hilo.......
 
Mmeona matokeo ya kutochukulia corona serious? Rwanda wana kesi +1000, Tanzania kesi 409 lakini Rwana inachukuliwa kama nchi salama kwani wameonesha weledi mkubwa na kuwa serious kuliko Tz ambayo imekataa kutoa takwimu. Nilisema huu ujinga utatuliza na watu hawakunielewa, sasa angalia watalii hawatakuja na ndio jiwe na wenzake watajua nini maana ya uongozi bora na udikteta.
Ingekua imeziwiliwa tanzania pekee ninge kuunga mkono alafu acha propaganda
 
Ingekua imeziwiliwa tanzania pekee ninge kuunga mkono alafu acha propaganda
Unajua watanzania wengi ni wajinga, mmezoea kifikiri kifo cha wengi ni harusi. Tunakosa watalii na tutapata shida kama Watanzania.

Hamuendelei watanzania kwa sababu mnaangalia majirani zenu waliopo kwenye umaskini kama ninyi basi mnaridhika kwani mpo wengi kwenye umaskini. Uhh!
 
Unajua watanzania wengi ni wajinga, mmezoea kifikiri kifo cha wengi ni harusi. Tunakosa watalii na tutapata shida kama Watanzania. Hamuendelei watanzania kwa sababu mnaangalia majirani zenu waliopo kwenye umaskini kama ninyi basi mnaridhika kwani mpo wengi kwenye umaskini. Uhh!
Marekan na urus wapo kwenye umaskini kama sis
 
Marekan na urus wapo kwenye umaskini kama sis
Hawapo na hawadhuriki kama sisi sasa nyie mnaona sawa kwasababu na wao wamefungiwa kama sisi. Ujue wao wanauchumi imara na mtambuka sio sisi tunategemea watu kuona nyumbu wakivuka mto.
 
Hawapo na hawadhuriki kama sisi sasa nyie mnaona sawa kwasababu na wao wamefungiwa kama sisi. Ujue wao wanauchumi imara na mtambuka sio sisi tunategemea watu kuona nyumbu wakivuka mto.
Sasa sisi wabongo ulaya tunaenda kutalii Nini? Ni wao ndio wameziwia watu kutoka kwetu kwenda kwao ila hawajaziwia watu kutoka kwao Kuja kwetu Sasa sijui unaangaika kwa nn
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom