Orodha kamili ya makatibu wakuu wa CCM tokea ilipoanzishwa mwaka 1977

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,523
4,991
Kwanza nianze kwa kutoa orodha kamili ya makatibu wakuu wa CCM tokea ilipoanzishwa mwaka 1977 baada ya kuungana na ASP:

kw.png

Ukiacha Pius Msekwa na Rashid Kawawa, Mwenyezi Mungu amweke mahali pema, hao wanaofuatia hakuna aliyeondoka vizuri katika nafasi yake. Horace Kolimba nadhani hapo hakuna mjadala, maana ile kauli yake kali aliyoitoa kwamba CCM HAINA DIRA, ndiyo ilianzisha kile kinachoitwa KUKOLIMBWA. Jamaa Walimkolimba. Mungu amweke mahali pema. Lawrence Gama, Mwenyezi Mungu amweke mahali pema, nakumbuka kulikuwa na figisufigisu wakati wa uchaguzi mkuu wa 1995, alikwaruzana sana na JK, ambaye alikuwa anaongoza kwenye kura za ndani ya CCM mpaka pale Nyerere alipoingilia kati.

Inaaminika Philip Mangula alikuwa moja ya makatibu wakuu bora na imara wa CCM. hakuwa na maneno mengi hadharani lakini alikuwa mtendaji mzuri sana ndani ya CCM, na aliijua vema. lakini alitupwa nje na Kikwete, tena kwa kejeli na manyanyaso. pamoja na kuwa mtendaji bora, hakwenda sawa na mfumo wa JK. JK akaona zee la mjini Makamba ndiyo chaguo sahihi.

Kwa maoni yangu, Makamba alikuwa Katibu Mkuu mbovu kuliko wote waliowahi kushika cheo hicho. alilea mfumo wa rushwa katika CCM, na malalamiko ya ubaguzi na utendaji mbovu yalishamiri enzi zake. JK alijaribu kukiokoa chama kwa kuja na sera ya KUVUA GAMBA, ambayo ilikuwa matokeo ya utafiti uliofanywa na tume ya Wilson Mukama. Huyu alipewa kazi ya ukatibu mkuu ili atekeleze sera aliyoifanyia utafiti. lakini hakuwa na nguvu za kisiasa ndani ya CCM, na hapakuwa na utayari wa kisiasa kumuunga mkono kati ya vigogo wa CCM. akakwamba na CCM ikazidi kuyoyoma. Akiwa desperate, JK ndipo alipomleta Abdulrahman Kinana.

Kinana anatajwa kama Katibu mkuu bora kabisa katika orodha ya makatibu wakuu wa CCM. anajumlisha uzoefu katika uongozi wa serikali na chama, kukielewa chama, kiwango cha juu cha upevu na hekima. ukiacha tuhuma mbalimbali kuhusu nyara za serikali, ni mtu anayekubalika na wengi katika ngazi mbalimbali za chama. ni Kinana ambaye ameshindwa kwenda na kile kinachoitwa "kasi" ya Rais Magufuli. ilionekana wazi kwamba Kinana haivi na JPM. mitizamo na staili ya Kinana ni tofauti kabisa na ya JPM. Kinana amenukuliwa akisema wazi kwamba kiongozi hawezi kuhodhi ukweli, kwamba ni lazima awe tayari kusikiliza maoni tofauti. inajulikana kwamba JPM anahitaji kusifiwa daima, yeye hakosei, neno lake ni amri.

Sasa Bashiru Ally anaingia kwa mfano wa nani hapo? Bashiru kaingia kwa staili ya Wilson Mukama. wote walipewa kazi ya kuongoza "kamati maalum" na kutoa ripoti, ambayo ilipelekea wao kukabidhiwa kazi ya kutekeleza hayo waliyogundua. lakini tofauti ni kwamba Bashiru hakupata nafasi ya kuwashughulikia waliohodhi mali za chama. Bashiru pia siyo mtu wa ndani katika CCM, japo anadai kwamba amekuwa ndani ya CCM kwa miaka kadhaa.

Kwa kipindi cha mwanzo, Bashiru alionekana kufuata amri za Mwenyekeiti wake na kuzitekeleza, hata pale ambapo zilikuwa kinyume na katiba ya CCM. Bashiru ametetea utaratibu wa kuwaruhusu wanaoguswa na utendaji wa JPM na kujiuzulu ubunge au udiwani, kugombea tena nafasi hizo ndani ya CCM bila kupitia mchakato wa kura za maoni. Bashiru pia amekubali na kubariki wizi na uporaji katika sanduku la Kura, ili kuhakikisha kwamba CCM inashinda viti vyote katika chaguzi ndogo. mwenyewe amejenga hoja kwamba hii ni dalili ya kukubalika kwa chama!

Lakini inaonekana hata yeye haamini hayo, kwa kauli zake za hivi karibuni. anaonekana kujiondoa taratibu kwenye "uJPM" na "uMakonda", kwa kuwa na msimamo unaoendana na hali halisi zaidi, msimamo unaoakisi maoni ya watanzania walio wengi. si wengi wanaoingizwa mjini na kauli za "kuguswa na utendaji wa JPM", kiasi cha kuliingiza taifa katika gharama za uchaguzi ambazo wala hazina sababu, na wala hazina mantiki hata kwa akili ya kawaida tu. eti "DEMOKRASIA NI GHARAMA!!!" EBO!

Sasa swali linakuja, kama Bashiru anaanza kuwa na mawazo ya ki-Kinana Kinana hivi, mwisho wake ni upi? atajiuzulu au atangojea kutumbuliwa? au ndio ameamua kutumia nafasi hii "kuibadilisha CCM" jambo ambalo siyo rahisi hivyo, lakini pia inawezekana. hasa kama atakuwa mjanja wa kutafuta uungwaji mkono na watu muhimu ndani ya chama. inajulikana kwamba wengi katika CCM hawafurahishwi na mambo yanavyokwenda. lakini hii inahitaji tahadhari kubwa. Kwa kuonesha mwelekeo mapema hivi, ataweza kweli kufaulu kugeuza mwelekeo wa manowari hii kubwa? Tujadili
 
Kwa mwenyekiti huyu ambaye umemjadili vema, Itoshe kumwombea dua Bashiru Ally, katibu mkuu. Kama Kolimba alikolimbwa na "malaika", itakuwaje sasa? Ajitahidi, Mungu wake amtangulie, la sivyo anyong'onyee kama aliyetoka.
 
Kati ya Makatibu wakuu ambao CCM walikula hasara ni Wilson Mukama, huyu hata Kikwete Mwenyewe aliona kabisa amebugi kumteua.

Eti Chadema wameingiza Magaidi.
 
Kauchambuzi kazuri sana Mindi. Dk huyo wa sayansi ya siasa alinde heshima yake kwa kuendelea kueleza ukweli na kuibua uozo ndani ya CCM. Kama mwenyekiti wake atazidi kuendekeza ubabe na kulea unafiki basi Bashiru anaweza kujiuzulu.
Dunia itamuelewa!
 
Makawago mbona ujamuweka Katika Makatibu wakuu
Daudi Ngalautwa Mwakawago, Naam. Kama vile kweli amewahi kuwa Katibu Mkuu vile??? ila sina hakika kama alikuwa upande wa TANU au amewahi kukanyaga ukatibu mkuu wa CCM. tunaomba wenye taarifa kamili watujuze
 
Nakumbuka alishawahi kuwa waziri wa elimu, sayansi na teknolojia....sina kumbukumbu ya ukatibu mkuu wa ccm
 
To substitute him with slowslow
Kwa kweli ni wazi kwamba Bashiru aliamua kuunga mkono juhudi. Nadhani ameusoma vizuri mchezo wa Magu. Ukijifanya eti umejiuzulu, inakula kwako, naam, Big Time.

Samia Suluhu kaeleza wazi. Baada ya kugongana na Magu mara kadhaa, sasa kanyoosha mikono juu. Inaonekana Magu sasa kawatiisha wooote. Na kwa kujipangia mwenyewe nani awe mbunge na nani asiwe, kwa ccm na kwa upinzani pia, sasa yuko huru kabisaaa. Ndio, hata hao wanne wa upinzani kawachagua mwenyewe. Hakuna upinzani, hakuna vyombo vya habari, hakuna Bunge...raha mustarehe...kwa Magu
 
Sijaisoma hiyo orodha bali nimejiuliza inatusaidia nini hasa kwa yaliyotokea mwaka huu?
 
Kolimba alikufa kwa mshtuko wa moyo; hakupigwa risasi wala kulishwa sumu.

Hiyo ya kukolimbwa ulikuwa msamiati wa Mtikila lakini haukuwa na uhusiano wowote na kifo halisi cha Kolimba.

Viongozi wengi huwa wana matatizo ya blood pressure, hivyo katika maisha yo hawataki purukushani zaidi ya wanazoweza kumduu.

Marehemu Kolimba alijikuta na purukushani zaidi ya uwezo ambao mwili wake ungeweza kumudu wakati huo ndiyo maana akafariki ghafla.

Ingekuwa ni kuwa CCM inawaua watu wanaoiasi, nadhani mtu wa kuuwawa mapema angekuwa ni Lowassa mwaka 2015 kwani kweli yeye aliivuruga sana safu ya CCM wakati huo, Kolimba hakuwa na nguvu kama hiyo ya Lowassa.
 
Kolimba alikufa kwa mshtuko wa moyo; hakupigwa risasi wala kulishwa sumu. Hiyo ya kukolimbwa ulikuwa msamiati wa Mtikila lakini haukuwa na uhusiano wowote na kifo halisi cha Kolimba. Viongozi wengi huwa wana matatizo ya blood pressure, hivyo katika maisha yo hawataki purukushani zaidi ya wanazoweza kumduu. Marehemu Kolimba alijikuta na purukushani zaidi ya uwezo ambao mwili wake ungeweza kumudu wakati huo ndiyo maana akafariki ghafla. Ingekuwa ni kuwa CCM inawaua watu wanaoiasi, nadhani mtu wa kuuwawa mapema angekuwa ni Lowassa mwaka 2015 kwani kweli yeye aliivuruga sana safu ya CCM wakati huo, Kolimba hakuwa na nguvu kama hiyo ya lowassa.
Vipi Mwakyembe? Ule ulikuwa ugonjwa gani hadi nywele kupukutika?
 
Kwanza nianze kwa kutoa orodha kamili ya makatibu wakuu wa CCM tokea ilipoanzishwa mwaka 1977 baada ya kuungana na ASP:

View attachment 891793
Ukiacha Pius Msekwa na Rashid Kawawa, Mwenyezi Mungu amweke mahali pema, hao wanaofuatia hakuna aliyeondoka vizuri katika nafasi yake. Horace Kolimba nadhani hapo hakuna mjadala, maana ile kauli yake kali aliyoitoa kwamba CCM HAINA DIRA, ndiyo ilianzisha kile kinachoitwa KUKOLIMBWA. Jamaa Walimkolimba. Mungu amweke mahali pema. Lawrence Gama, Mwenyezi Mungu amweke mahali pema, nakumbuka kulikuwa na figisufigisu wakati wa uchaguzi mkuu wa 1995, alikwaruzana sana na JK, ambaye alikuwa anaongoza kwenye kura za ndani ya CCM mpaka pale Nyerere alipoingilia kati.
Inaaminika Philip Mangula alikuwa moja ya makatibu wakuu bora na imara wa CCM. hakuwa na maneno mengi hadharani lakini alikuwa mtendaji mzuri sana ndani ya CCM, na aliijua vema. lakini alitupwa nje na Kikwete, tena kwa kejeli na manyanyaso. pamoja na kuwa mtendaji bora, hakwenda sawa na mfumo wa JK. JK akaona zee la mjini Makamba ndiyo chaguo sahihi.

Kwa maoni yangu, Makamba alikuwa Katibu Mkuu mbovu kuliko wote waliowahi kushika cheo hicho. alilea mfumo wa rushwa katika CCM, na malalamiko ya ubaguzi na utendaji mbovu yalishamiri enzi zake. JK alijaribu kukiokoa chama kwa kuja na sera ya KUVUA GAMBA, ambayo ilikuwa matokeo ya utafiti uliofanywa na tume ya Wilson Mukama. Huyu alipewa kazi ya ukatibu mkuu ili atekeleze sera aliyoifanyia utafiti. lakini hakuwa na nguvu za kisiasa ndani ya CCM, na hapakuwa na utayari wa kisiasa kumuunga mkono kati ya vigogo wa CCM. akakwamba na CCM ikazidi kuyoyoma. Akiwa desperate, JK ndipo alipomleta Abdulrahman Kinana.

Kinana anatajwa kama Katibu mkuu bora kabisa katika orodha ya makatibu wakuu wa CCM. anajumlisha uzoefu katika uongozi wa serikali na chama, kukielewa chama, kiwango cha juu cha upevu na hekima. ukiacha tuhuma mbalimbali kuhusu nyara za serikali, ni mtu anayekubalika na wengi katika ngazi mbalimbali za chama. ni Kinana ambaye ameshindwa kwenda na kile kinachoitwa "kasi" ya Rais Magufuli. ilionekana wazi kwamba Kinana haivi na JPM. mitizamo na staili ya Kinana ni tofauti kabisa na ya JPM. Kinana amenukuliwa akisema wazi kwamba kiongozi hawezi kuhodhi ukweli, kwamba ni lazima awe tayari kusikiliza maoni tofauti. inajulikana kwamba JPM anahitaji kusifiwa daima, yeye hakosei, neno lake ni amri.

Sasa Bashiru Ally anaingia kwa mfano wa nani hapo? Bashiru kaingia kwa staili ya Wilson Mukama. wote walipewa kazi ya kuongoza "kamati maalum" na kutoa ripoti, ambayo ilipelekea wao kukabidhiwa kazi ya kutekeleza hayo waliyogundua. lakini tofauti ni kwamba Bashiru hakupata nafasi ya kuwashughulikia waliohodhi mali za chama. Bashiru pia siyo mtu wa ndani katika CCM, japo anadai kwamba amekuwa ndani ya CCM kwa miaka kadhaa.

Kwa kipindi cha mwanzo, Bashiru alionekana kufuata amri za Mwenyekeiti wake na kuzitekeleza, hata pale ambapo zilikuwa kinyume na katiba ya CCM. Bashiru ametetea utaratibu wa kuwaruhusu wanaoguswa na utendaji wa JPM na kujiuzulu ubunge au udiwani, kugombea tena nafasi hizo ndani ya CCM bila kupitia mchakato wa kura za maoni. Bashiru pia amekubali na kubariki wizi na uporaji katika sanduku la Kura, ili kuhakikisha kwamba CCM inashinda viti vyote katika chaguzi ndogo. mwenyewe amejenga hoja kwamba hii ni dalili ya kukubalika kwa chama!

Lakini inaonekana hata yeye haamini hayo, kwa kauli zake za hivi karibuni. anaonekana kujiondoa taratibu kwenye "uJPM" na "uMakonda", kwa kuwa na msimamo unaoendana na hali halisi zaidi, msimamo unaoakisi maoni ya watanzania walio wengi. si wengi wanaoingizwa mjini na kauli za "kuguswa na utendaji wa JPM", kiasi cha kuliingiza taifa katika gharama za uchaguzi ambazo wala hazina sababu, na wala hazina mantiki hata kwa akili ya kawaida tu. eti "DEMOKRASIA NI GHARAMA!!!" EBO!

Sasa swali linakuja, kama Bashiru anaanza kuwa na mawazo ya ki-Kinana Kinana hivi, mwisho wake ni upi? atajiuzulu au atangojea kutumbuliwa? au ndio ameamua kutumia nafasi hii "kuibadilisha CCM" jambo ambalo siyo rahisi hivyo, lakini pia inawezekana. hasa kama atakuwa mjanja wa kutafuta uungwaji mkono na watu muhimu ndani ya chama. inajulikana kwamba wengi katika CCM hawafurahishwi na mambo yanavyokwenda. lakini hii inahitaji tahadhari kubwa. kwa kuonesha mwelekeo mapema hivi, ataweza kweli kufaulu kugeuza mwelekeo wa manowari hii kubwa? Tujadili
Wilson mukama alitia fora,
 
Hii list inasaidia kufanya niweke heshima Bar ???
 
CCM imeshavurugwa kabisa! Chama kinachoamini kuwa bila dola hakiwezi kubaki madarakani hakina jipya.
 
Back
Top Bottom