ORLANDO PYRATES: Walivyochezewa nusu uwanja hata nyumbani kwao Afrika ya kusini waliona. Porojo za hujuma hazina nafasi.

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,036
Katika ulimwengu wa soka wa Leo Kila mmoja anajionea mwenyewe mambo yalivyokuwa uwanjani. Nafasi ya kudanganya watu kujitafutia huruma haipo.

Kusema kweli Orlando washukuru Sana kuishia kufungwa goli moja tu kwa jinsi walivyokuwa wamezidiwa! Hiyo penati ilikuwa ya wazi Sana, BM alipigwa ngwala ya kizamani!
 
Vipi zile dk 20 za mwisho bado waliendelea kuchezewa nusu uwanja
Zile dk 20 za mwisho wala zisikutishe. Simba waliamua kuwekeza nguvu kwenye kushambulia wakaacha kiungo mkabaji mmoja ndio maana wale jamaa walionekana bora. Kwenye mechi ijayo usidhani Simba wataingia kizembe. Subiri tuone.
 
Katika ulimwengu wa soka wa Leo Kila mmoja anajionea mwenyewe mambo yalivyokuwa uwanjani. Nafasi ya kudanganya watu kujitafutia huruma haipo.

Kusema kweli Orlando washukuru Sana kuishia kufungwa goli moja tu kwa jinsi walivyokuwa wamezidiwa! Hiyo penati ilikuwa ya wazi Sana, BM alipigwa ngwala ya kizamani!
Cha kusikitisha huyu naye unaweza kuambiwa ni mchambuzi wa mpira kwenye viredio vyetu vinavyoishia magomeni.
 
Jeff Lea anasema Simba ilishinda kwa kutumia dark arts, sijui ndio uchawi ?🐒
 
wewe uchambuzi wako uko wapi tuusome
Nitakwenda kukuchambulia kinachokwenda kutokea Soweto, baada ya kutolewa kule mtamkuta Mayele ameshapaka vumbi la Congo, baada ya mechi hiyo na Mayele kutetema ndio akili zitawarudia na kuusikia uchungu wa gap ya point 16, shughuri kwishney.
 
Nitakwenda kukuchambulia kinachokwenda kutokea Soweto, baada ya kutolewa kule mtamkuta Mayeke ameshapaka vumbi la Congo, baada ya mechi hiyo na Mayele kutetema ndio akili zitawarudia na kuusikia uchungu wa gap ya point 16, shughuri kwishney.
Wewe ni Yanga tu 🤣🤣🤣🤣
 
Nitakwenda kukuchambulia kinachokwenda kutokea Soweto, baada ya kutolewa kule mtamkuta Mayele ameshapaka vumbi la Congo, baada ya mechi hiyo na Mayele kutetema ndio akili zitawarudia na kuusikia uchungu wa gap ya point 16, shughuri kwishney.
HAHA safi sana
 
Vipi zile dk 20 za mwisho bado waliendelea kuchezewa nusu uwanja
Tunatumia takwimu/statistics za dakika zote 90! Mchezo wa kandanda ni dk 90. Ndiyo maana timu ya wiki ya CAF karibuni nusu yake ni wachezaji wa Simba!! Kati ya 11 Simba imeingiza wachezaji 5!
 
Vipi zile dk 20 za mwisho bado waliendelea kuchezewa nusu uwanja
Angalia mabadiliko yaliyofanyika pia kwenye kikosi cha Simba, walitolewa viungo wakabaji kisha wakaingizwa washambuliaji ni lazima mchezo ungebadilika tu pale kati.

Kwakua nyinyi sio watu wa mpira hilo huamuwezi hamuwezi kuliona.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom