Orijino Komedi wanapokashifu afya ya Lowassa, wamesahau ya mwenzao VENGU?

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
11,440
12,294
Afya ni majaliwa ya Mungu,leo kundi la OK linasimama majukwaani kwenye kampeni za ccm hata kutoa post mitandaoni za kudhihaki afya ya Lowassa wamesahau yalimpata mwenzao Vengu? mwaka wa nne leo yuko kitandani.ikumbukwe huyu jamaa alikua ni bingwa wa kumuigiza Mrema na maradhi yake kwa bahati mbaya Mungu kampiga kofi leo hii yeye ndio yuko kitandani na Mrema huyoooo yuko mzima kabisa.

Tukumbuke tunayo yafanya Mungu anatuona.kuna Leo na kesho.
 

Attachments

  • 1441958160982.jpg
    1441958160982.jpg
    24.6 KB · Views: 4,386
Ze comedy hawana mvuto na mda mrefu ka miaka miwili sijaangalia kipindi chao. Tatizo ubunifu zero sasa ukishamkashifu afya ya mtu ndo umeongeza kura za CCM mijitu mingine bwana. Wananchi wanawachora tu kuna watu wazima na wanakufa ghafla usingizi. Wanatukana wakunga na uzazi ungalipo.
 
Ndiyo maana nikiwa kwenye mood ya kuangalia Comedy huwa naangalia Churchill ya Kenya yaani unajikuta unacheka na kutoa stress zote kabisa....Hata kama sintokuwa mzalendo lakin unakuta unaangalia Original Comedy unatafuta wapi utacheka mpaka show inaishia hakuna kichekesho hata kimoja.
 
Ze comedy hawana mvuto na mda mrefu ka miaka miwili sijaangalia kipindi chao. Tatizo ubunifu zero sasa ukishamkashifu afya ya mtu ndo umeongeza kura za CCM mijitu mingine bwana. Wananchi wanawachora tu kuna watu wazima na wanakufa ghafla usingizi. Wanatukana wakunga na uzazi ungalipo.

Hata CCM yenyewe haielewi damage inayopata kwa kubeza afya ya Lowasa na kufanya kama kitu cha kujivunia maana hata wapambe wao walio kwenye msafara wa Magufuli na Samia wanatumia maneno ya kejeli kuhusu Afya.
Namfahamu jamaa mmoja ambaye ilikuwa hata nimwambie nini kuhusu CCM na Magufuli alikuwa haelewi kitu, lakini nyumbani kwake ana Baba yake mzazi ni mgonjwa alipata stroke kama mwaka sasa na anaendelea na matibabu. Majuzi Lusinde sijui akiwa wapi akakebehi afya ya Lowasa na majigambo chungu nzima.
Toka maneno yale yule jamaa amekidharau hicho chama na wagombea wake kwa kukubali kupigiwa upatu kwa kukashifu afya za wengine. Jee ni wangapi wataidharau ccm kwa kauli za kuwadharau watu kwa afya zao?
 
Suala la afya ya mtu sio chambo la kufanyia maigizo hata kidogo.
Orijino Komedy imebaki jina tu lakini ni kikundi ambacho kwa sasa hakina tena mvuto wowote na wala hakina ushawishi wa namna yoyote ile kwenye kampeni hizi za Uchaguzi.
 
Mm nashangaa na kisikitika kuongelea afya ya mtu, hiv nan anyejua hatma ya mtu kama si mora pekeee jamani, ss tunataka mabadiliko so kuhusu afya ni mbele huko tutjua bana, kosa kubwa sana kumuongelea mtu mara hoooo!!!! Afya imekuwaje?
 
hawajielewi hawa wanatumika bila wao kujijua wafanye kampeni za kumnadi mgombea wao na si kubeza afya ya mu hamna anayejua kesho ataamka vipi
 
Nimewatoa maanani sana hawa watu kwanza kuchekesha yenyewe hawajui tena wanatumia uzoefu tu saiv
 
Wasanii kuishabikia siasa in a wrong manner ni jambo litakalowaletea matatizo makubwa mbele. Mwenye sikio na asikie, mwenye akili na atafakari
 
Back
Top Bottom