Chromium
JF-Expert Member
- Apr 17, 2008
- 589
- 185
Ni wazi kile kikundi kilichopata kuwa maarufu cha Orijino Komedi kinachorusha vipindi vyake kupitia TBC1 kiko muflisi. Kwanza hawaonekani kuwa na mvuto wowote tena kama walivyokuwa enzi za Ze Comedy ya EATV. Pili wanaonekana kutumika kupotosha ukweli wa mambo kuwapata wananchi wasio na uelewa alumradi wanaganga njaa zao.
Hivi sasa wanaendelea na kipindi chao ambapo tayari wameonyesha tukio la yule DC mchakachuaji kule Igunga katika muktadha unaompendelea moja kwa moja. Wametaka ieleweke eti DC alikuwa kwenye mkutano wa kuratibu amani wilayani hapo na "wahuni" wa CDM walimvamia tu pasi na sababu.
Ninaandika haya nikielewa kuwa haikuwa sahihi kwa wale wanaodaiwa kuwa mashabiki wa CDM kumtia kashikashi DC yule na wakati huo huo nikiyalaani kwa nguvu zote matangazo haya yanayokusudia kuwadanganya wananchi.
Nailaani TBC1 inayowatumia vijana wenye njaa kuwapotosha wananchi wasioelewa.
Nawalaani vijana wanaotumia vipaji vyao isivyo. Namlaani msomaji anayekubaliana na upuuzi huu.