Orijino komedi: Mnaganga njaa kutangaza propaganda za magamba?

Chromium

JF-Expert Member
Apr 17, 2008
589
185
Ni wazi kile kikundi kilichopata kuwa maarufu cha Orijino Komedi kinachorusha vipindi vyake kupitia TBC1 kiko muflisi. Kwanza hawaonekani kuwa na mvuto wowote tena kama walivyokuwa enzi za Ze Comedy ya EATV. Pili wanaonekana kutumika kupotosha ukweli wa mambo kuwapata wananchi wasio na uelewa alumradi wanaganga njaa zao.

Hivi sasa wanaendelea na kipindi chao ambapo tayari wameonyesha tukio la yule DC mchakachuaji kule Igunga katika muktadha unaompendelea moja kwa moja. Wametaka ieleweke eti DC alikuwa kwenye mkutano wa kuratibu amani wilayani hapo na "wahuni" wa CDM walimvamia tu pasi na sababu.

Ninaandika haya nikielewa kuwa haikuwa sahihi kwa wale wanaodaiwa kuwa mashabiki wa CDM kumtia kashikashi DC yule na wakati huo huo nikiyalaani kwa nguvu zote matangazo haya yanayokusudia kuwadanganya wananchi.

Nailaani TBC1 inayowatumia vijana wenye njaa kuwapotosha wananchi wasioelewa.

Nawalaani vijana wanaotumia vipaji vyao isivyo. Namlaani msomaji anayekubaliana na upuuzi huu.
 
Kwani ushawahi kusikia chadema imemnunua msanii yeyote eti ndo awe chachu ya kuvuta watu mkutanoni.! Katu wasanii uchwara wanatumia chama uchwara kujiibia wenyewe kwa ka posho wanakopewa kwa kuwakatikia viuno wakubwa majukwaani
 
Ni wazi kile kikundi kilichopata kuwa maarufu cha Orijino Komedi kinachorusha vipindi vyake kupitia TBC1 kiko muflisi. Kwanza hawaonekani kuwa na mvuto wowote tena kama walivyokuwa enzi za Ze Comedy ya EATV. Pili wanaonekana kutumika kupotosha ukweli wa mambo kuwapata wananchi wasio na uelewa alumradi wanaganga njaa zao.

Hivi sasa wanaendelea na kipindi chao ambapo tayari wameonyesha tukio la yule DC mchakachuaji kule Igunga katika muktadha unaompendelea moja kwa moja. Wametaka ieleweke eti DC alikuwa kwenye mkutano wa kuratibu amani wilayani hapo na "wahuni" wa CDM walimvamia tu pasi na sababu.

Ninaandika haya nikielewa kuwa haikuwa sahihi kwa wale wanaodaiwa kuwa mashabiki wa CDM kumtia kashikashi DC yule na wakati huo huo nikiyalaani kwa nguvu zote matangazo haya yanayokusudia kuwadanganya wananchi.

Nailaani TBC1 inayowatumia vijana wenye njaa kuwapotosha wananchi wasioelewa.

Nawalaani vijana wanaotumia vipaji vyao isivyo. Namlaani msomaji anayekubaliana na upuuzi huu.
Wamedhihirisha kuwa TBC sio TV ya taifa bali ni TV ya chama flani.
 
Kaka wala usitumie nguvu kuwalaani. Hawa Mwenyezi Mungu anawaona na atawalipa kwa wayafanyayo kizazi chao hadi cha 4.
 
Mkuu nimewaona nilikuwa nimekaa na mama yangu na mke wangu, yaani wameboa ile mbaya. hatukuhitaji hata kumalizia kipindi chao. Jamaa wanajipoteza kwenye game ki-pu-mba-vu saaaaaaaana.
 
Niliacha kuangalia comedy kwa upuuzi kama huu,kimekuwa kikundi cha propaganda za ccm,baada ya vichekesho.sio siri NJAA noma!
 
The Orijino Comedi ni watumwa wanaofanya kazi ya Bwana wao, hatuna haja ya kuwaandama on individual circumstances. Tunajua wanawatumikia ccm. Lazima tukubali kuwa ukiwa ndani ya ccm hata akili yako inadumaa
 
Wanasimuliwa tu na kwenda kuigiza mambumbu wote wale njaa zinawatesa
 
maana yake ni kwamba sisi waafrica hatujui ku-maintain talent zetu kwa sababu ya upumbavu wetu
 
Jamaa hao hawana thamani tena ya kuangaliwa wamekuwa vinaraka tu sasa, bado kidogo wataanza kuzomewa mitaani
 
Hawana jipya hao full kuganga njaa hatuna mda wa kuwajadili watu kama hawa.
 
hawana jipya wale! upeo mdogo,elimu duni.Si walikuwa wanachunga mbuzi tu huko bush-contry? Unategemea wasipojikomba kwenye masaburi ya CCM watakula wapi?
 
Ukiachilia mbali hili tukio la DC....unajua jamaa walikuja juu haraka mpaka wakawa local celebrities, watoto wanaenda kijotijoti, walienda mtaani kila mtu anataka awaguse

Nadhani ipo haja ya wasanii kupata mafunzo ...maana hata bambo alibamba sana enzi zake na kuimba 'tundi' baadae ikawa kila kitu anachapia mpaka inaboa eti 'Drogbo' badala ya Drogba....wengine kukata mauno ...naamini kuna potential, they just need direction, nikiangalia vijana wa pasua wa Kenya wanavyonivunja mbavu...
 
Ccm imewadanganya Umaarufu wenu unashuka kwa kasi ya ajabu.Lakini nimefurahi sana kwani nilifikiri wasaliti wa Uhuru wa kweli wa Mtanzania ni Wasanii wa Bongn Fleva waliyoifanyia Ccm campaign 2010 kumbe na nyie Comedy,JOTI,MPOKI,MASANJA.Mtatukoma sasa we er gng there guys.
 
mmesahau usemi wa kiswahili mtumikie kafiri upate mtaji au baniani mbaya kiatu chake dawa?hawa madogo walipelekwa TBC na Manji ambae ni kada na fisadi maarufu,lazima walipe fadhila sasa
 
Back
Top Bottom