Orijino Comedi - Sasa Kwisha

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,264
8,475
Kwa wale mnaofuatilia mchezo wa kuchekesha wa Orijino Komedi unaorushwa na TBC1 kituo kinachoendeshwa na kodi zenu wa TZ mtaona kabisa kundi hili sasa linapoteza mwelekeo na kuwa chombo cha kusifia na kutetea maslahi ya kundi fulani.

Hili kundi sasa linaboa, limekuwa silaha ya kundi la mafisadi.

Hebu tuangalie kuinuka na kuanguka kwa kundi hili na nini wakifanye kwa maslahi yao ya baadae ukiachana na hali yao ya sasa 'Mtumikie kafiri upate mradi wako"
 
Kwa sasa sioni wanafundisha nini hawa wajamaa. Anyways am not funny of them since left EATV.
 
Mi nakumbuka kilipokuwa kinarushwa EATV,mida ya 12 jion Alhamis foleni ilikuwa hamna. Siku hizi hata ukikosa hujutii.
 
Kwa wale mnaofuatilia mchezo wa kuchekesha wa Orijino Komedi unaorushwa na TBC1 kituo kinachoendeshwa na kodi zenu wa TZ mtaona kabisa kundi hili sasa linapoteza mwelekeo na kuwa chombo cha kusifia na kutetea maslahi ya kundi fulani.

Hili kundi sasa linaboa, limekuwa silaha ya kundi la mafisadi.

Hebu tuangalie kuinuka na kuanguka kwa kundi hili na nini wakifanye kwa maslahi yao ya baadae ukiachana na hali yao ya sasa 'Mtumikie kafiri upate mradi wako"

Inawezekana kuwa kweli ila hoja yako imekosa nguvu. Ulichotakiwa kufanya ni kuwarekodi na kutuwekea video yao hapa ili tuone ulichoona wewe, huko ndiko kuangalia "kuinuka na kuanguka kwa kundi hili"
 
Watoto wana tamaa sana na pesa, kwanza hawana tena raha ukiangalia unaonana wanatumiwa tu!!!!
Hakuna lolote, wamekwisha kabisa wamelewa sifa
 
Dawa ni kuwepo Kundi mbadala isiyosimamia maslahi ya mafisadi na watawala, wawamalize kabisa.
 
Are they gonna blame Mengi for not being funny anymore??

Ndo maana mafisadi wanaendelea kupeta, wajua watanzania wengi wetu ni njaaaa.
 
KUWA NA KUNDI MBADALA HAISAIDII. Unajua baada ya wao kutoka EATV walienda TBC ( station inayotumiwa na fisadis) na wakapewa udhamini na Manji (Papa) Unategemea nini? Hapo ndio wamekosea wanaangalia maslahi ya muda mfupi wasijue kama wameichagua kuwa kazi yao wanatakiwa waifanye kwa miaka chungu tele.

Afadhali MIZENGWE wako juu na wale kweli wanajua wanachofanya.

WAJIREKEBISHE WANATUBOAAAAAAA!
 
Haya ni maono au mtizamo wa watu mlio kuwa mnapenda Ze commedy wawe wanarusha EAT au chanel 5 mbona vijana wapo juu na wanakula maisha na kuchekesha kama kawa mtaani wanakamata sana vichwa...nyie endeleeni na hoja zenu zaifu.
 
are they gonna blame mengi for not being funny anymore?? Ndo maana mafisadi wanaendelea kupeta, wajua watanzania wengi wetu ni njaaaa.

Kweli mkuu njaa mwanakharamu, na haina adabu..Walakini mimi
naamini sisi waTz tatizo letu kubwa ni akili. Tatizo secondary linaweza kuwa njaa lakini tatizo primary lipo akilini.

Hawa ze comedi kama wangeweza kukaa chini na kuvumilia kidogo na kuwa na mipango ya muda mrefu wasingepoteza utu na ubinadamu wao kwa mhindi fisadi. Wangeji-establish na kufanya mambo professionally, wangekuwa wananyoosha miguu ofisini dili zinawafuata hukuhuko..lakini ona sasa wanavyojiaibisha .
 
Inaonekana kuna uhusiano wa karibu ssana kati ya wanamtandao na mafisadi... Tido Mhando ni mwanamtandao aliesaidia sana kampeni za "JUMA KILAZA" (JK) alipokuwa BBC na akazawadiwa ukurugenzi kama asante toka kwa JUMA KILAZA.
 
Niliangalia kipindi cha wiki iliyopita sikuamini kwamba wanaweza kuigiza kumkashfu mgonjwa Banza Stone badala ya kutafuta namna ya kuieleza jamii namna ya kumsaidia badala ya kumzidishia machungu kwake na ndugu zake
 
"Mi nakumbuka kilipokuwa kinarushwa EATV,mida ya 12 jion Alhamis foleni ilikuwa hamna. Siku hizi hata ukikosa hujutii."

Ni kweli wamekwisha kabisa, hasa kipengele cha 'enzi za mwalimu...' ni upuuzi mtupu, wameshanyonywa akili hakuna ubunifu wowote zaidi kusubiri kuambiwa nini cha kusema...Au ni hivyo vinyumba walivyoahidiwa?

Nkawa.
 
Hii vita ya ufisadi imekuwa ni explanation ya kila kitu? Hawa ni wasanii wachanga labda mategemeo yenu makubwa ndio yamewaangusha. Ingekuwa ni ufadhiri wa Manji tu ndio tatizo wangeweza kutuchekesha kwa angle hiyohiyo pia..mbona zamani mlicheka alipokuwa anaoneshwa EL wakati huo waziri mkuu anakojoa barabarani? Ni lazima tupanue mawazo yetu kuanguka au kuanguka kwa komedi ni kukosa kwao ubunifu na si ufadhiri wao.

Kiwango chao cha kufikiri kimekwamia kusema umbeya tu na ninyi mashabiki wao mlidhani wangekuja na jipya.
 
kwa kweli nilikuwa vijana kipindi wako EATV walikuwa wako juu,MAAAASKINI walipoingia kwa TBC1 utafikiria kuku waliokatwa vichwa hawana muelekeo,FISADIS wanawatumia jinsi wanavyotaka?wanaboaaaaaaaaaaa.hawana jipya
 
Inaonekana kuna uhusiano wa karibu ssana kati ya wanamtandao na mafisadi... Tido Mhando ni mwanamtandao aliesaidia sana kampeni za "JUMA KILAZA" (JK) alipokuwa BBC na akazawadiwa ukurugenzi kama asante toka kwa JUMA KILAZA.

Pia huyo Juma Kilaza ni rafiki yake Roast ya hamu ndio maana siku hizi ze komedi hawachekeshi....Gime a break hao wanaocheka na comedy hayo hayawuhusu kabisa, mnachokifanya ni kama kuwapa sifa hao komedi wenu kama wao wanaweza ila kuna msukumo kutoka kwa mafisadi unao wazamisha. Hawa vijana wasingeweza kuendelea kubaki juu kwa sababu ya kukosa ubunifu, wanachokifanya ni kurudia yote walikwisha yafanya hapo awali aint ni funny any more...HAWANA UWEZO FULL STOP
 
Jamani tuwe wa kweli, tunaposema Comedy!, hawa sio maprofesa, mainjinia, wala madaktari! sio waandishi wa habari hawa!. Tumeona waandishi wakinunuliwa kama mitumba, maprofesa wakila rushwa , hivi hawa wana-UFISADI- PROOF gani? watashindwa nini kukubali kufuata mafisadi?? akama tuliona ndani ya EATV walikuwa moto, nakwambia Tz kuna vipaji vingi tu, ebu tuwape changamoto EATV watafute vijana wanaolipa zaidi, warudishe enzi zile, kukaa na kushindana na wenye hela tena za EPA tunapoteza muda! , wakati wakiondoka leo TBC, hakuna wa kuwapa chakula wao na wake zao tunapoteza muda! dawa ya moto ni moto! I believe wako wazuri zaidi ya hawa, EATV iwatafute, tukate mawasiliano nao, hakuna kuwaalika harusini, kwenye shughuli wala hatuendi kwenye shoo yao!
 
Manji kawaweka mikononi vijana hawa, kama utakumbuka siku ya mechi ya watani wa jadi (simba vs yanga) vijana waliburuzwa uwanjani kwenda kuishangilia yanga, sidhani kama hii ilikuwa ni kwa ridhaa yao. Vijana wanatumiwa ndivyo sivyo, kama ni issue ya kipato inatakiwa kuwa makini sana vinginevyo utajikuta unakuwa mtumwa wa kipato unachohangaikia.
 
haya ni maono au mtizamo wa watu mlio kuwa mnapenda ze commedy wawe wanarusha eat au chanel 5 mbona vijana wapo juu na wanakula maisha na kuchekesha kama kawa mtaani wanakamata sana vichwa...nyie endeleeni na hoja zenu zaifu.


wape vidonge!
 
Manji kawaweka mikononi vijana hawa, kama utakumbuka siku ya mechi ya watani wa jadi (simba vs yanga) vijana waliburuzwa uwanjani kwenda kuishangilia yanga, sidhani kama hii ilikuwa ni kwa ridhaa yao. QUOTE]

Hapo unaleta ligi nyingine, tuambie na wewe ulivyokwenda uwanjani uliburuzwa na nani? Mengi
 
Back
Top Bottom