Organic Farming Agenda in Tanzania,is it too little to late?

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
10,627
2,000
Kwa muda mrefu tumekuwa tukipiga kelele kuhusu ubaya wa inorganic farming(mimi nakiita kilimo mfu!),hasa matumizi ya mbolea za viwandani na viwatilifu vya aina mbali mbali bila kusahau madawa ya hospitali na kemikali zingine mbali mbali ambazo nazo zinaanaangukia kwenye kundi la sumu.Tuli-itwa majina mengi na wala sina haja ya kuyarudia kwa kuwa yaliuma hasa kwa kuwa nia yetu ilikuwa njema na tulikuwa tunasukumwa na dhamira njema kwa watanzania wenzetu ambao wangeathirika na matumizi ya mbolea hizo,madawa ya hospitali na kemikali mbalimbali.

Nani kwa mfano asiyejua ubaya wa Glyphosate kwenye wadudu wa ardhini(soil macro and micro flora) na afya za watu,lakini mpaka leo ipo kwenye maduka ya pembejeo?Nadiriki kusema wengi wanaotetea na waliokuwa wanatetea matumizi ya kemikali hizo i.e.mbolea,
viwatilifu na kemikali zingine,walikuwa wanasukumwa na faida binafsi za muda mfupi na mrefu na pia faida za makampuni ya kibepari wanayo yatumikia.

Kwa bahati mbaya yale tuliyokuwa tunataka yasitokee kwa wananchi wetu,ndio kilio cha wananchi
walio wengi leo.Wote tu mashahidi jinsi magonjwa mbali mbali yasiyo na tiba yakiwemo saratani mbali mbali,kisukari nk.nk.yanavyo watesa watu wetu.Nani wa kulaumiwa?

Naomba niwe mkweli na muwazi.Kwa jinsi hali ilivyo kwa sasa,ni vigumu sana kuondokana na janga hili,ambalo tumejitumbukiza au kwa kujua au kwa kutokujua!It is simply too complex.

Nikiangalia kwa haraka haraka, vyakula vya madukani na vinywaji mbali mbali vyote vina-angukia katika kundi la vyakula na vinywaji visivyofaa (junk foods and drinks),bila kusahau madawa ya hospitali.Tunaanzia wapi?Hali ni mbaya sana.Kwanza Watanzania hawatatuelewa.Watadharau tu na kusema mlikuwa wapi miaka yote hiyo wakati
watu wamesha athirika kiasi hiki?Kwa mara nyingine tena nasema,tumeshachelewa sana.


Ni hivi majuzi tu nimesikia mpango wa kilimo hai,huku serikali ya Ufaransa ikiahidi kutoa fedha kwa ajili ya mpango huo.Hata hivyo mimi huwa siamini ufadhili wa
nchi za magharibi,kwa kuwa nchi hizo huwa siku zote hazina nia njema na nchi maskini.Nia yao mara nyingi ni kuwaibia kwa hiyo hutumia muda mwingi siku zote kubuni mbinu na tekinolojia za kutekeleza adhma yao hiyo ovu kabisa.

Sawa tunaanzisha mpango wa kilimo hai
, na jee kuhusu vyakula vya madukani na madawa yanayotengenezwa nchini na ya kutoka nchi za nje ambayo yanatumia tekinolojia ya nchi za magharibi? Mbaya zaidi hizo tekinolojia
za nchi za magharibi hata hatuna uwezo wakuzifanyia uchunguzi kama hata ni rafiki kwetu au laa.Tusisahau pia kwamba mavitu mengi wanayotuletea nchi za daraja la tatu wanatusukumia tu,wao wenyewe hata hawatumii.

Hivi tunajua kweli kwamba Bill Gates watoto wake hawatumii chanjo, lakini anazisukumia kwetu?Ndio maana nimesema tunayofanya sasa is too little too late,watu wamesha athirika sana.Hii ni sawa sawa na lile swala la kupiga marufuku mifuko midogo ya plastic,wakati plastic nyingi inabaki kwenye mazingira yetu.Hapana nadh
ani tunahitaji kufanya mambo yetu vizuri zaidi,ilivyo sasa sio
.

NB:Glyphosate ni kiwatilifu kilichoko kwenye dawa ya kuulia magugu.Mwenye patent ya Glyphosate ni mzee wa utata na kutengeneza sumu Monsanto.Zamani jina la kibiashara ya dawa hiyo lilikuwa Roundup.Siku hizi yapo makampuni mengi yanayotengeneza dawa zenye kiwatilifu cha Glyphosate.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom