Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,160
- 1,492
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan maono yake ni kuhakikisha Watanzania wanapata huduma zilizo bora , Mh Rais amekuwa akipigana usiku na mchana kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma za Afya, Maji, Umeme, Watoto wote wenye umri wa kwenda Shule wanaenda shule bila ada, barabara zinazopitika wakati wote pamoja na huduma nyingine muhimu.
Katika kusaidia kupatikana kwa huduma zilizo bora kwa Watanzania na kufikia malengo na matamanio ya Mheshimiwa Rais, OR- TAMISEMI iwekeze katika kuimarisha Idara za Mipango, Takwimu na Ufiuatiliaji katika Halmashauri zote Nchini.
Idara za Mipango, Takwimu na Ufiuatiliaji ni engine inayoweza kutoa dira wa utoaji wa huduma kwa Wananchi, ndio inayoweza kutoa muelekeo wa kufikia malengo ya Halmashauri katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri, utoaji wa huduma kwa Wananchi, utekelezaji wa miradi ya Maendeleo na kuweza kuitafsiri Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo.
Halmashauri ziweze kuweka bajeti ya kuhakikisha inatenga bajeti ya kuwapeleka Watalaamu wa Idara za Mipango katika mafunzo ya muda mfupi ili kuongeza ujuzi na weredi katika kuibua miradi mipya ya maendeleo, kujifunza namna ya kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuanda bajeti bora zinazotekelezeka.
Halmashauri zote zimekuwa zikiandaa Mpango Mkakati wa Halmashauri wa miaka 5 ( Strategic Planning), SP ni roho ya kila Taasisi katika utekelezaji wa Taasisi zote (Iwe Taasisi ya Serikali au ya Mtu binafsi), Watalaamu wa Idara ya Mipango wawezeshwe kwa kupewa mafunzo namna bora ya kuandaa Mpango Mkakati unaotekelezeka, hii itasaidia sana Halmashauri zote kujiwekea malengo. Bila kuwapeleka Wataalamu hawa wa Idara za mipango kwenye mafunzo ya muda mfupi, Halmashauri zitaendelea kutekeleza bajeti zile zile kila mwaka japokuwa kuna ufanisi lakini tunaweza pata ufanisi zaidi kwa KUZIWESHA HALMASHAURI KUWA NA WATAALAMU WENYE UELEWA NA UZOEFU MKUBWA KATIKA MAMBO YA MIPANGO.
OR-TAMISEMI, Idara ya Mipango ina Watalaam wazuri na bobezi katika mambo ya uandaaji wa Mpango Mkakati, Watumike kutoa elimu kwa Watalaam wa Halmashauri ili kila Halmashauri iwe na Mpango Mkakati unaotekelezeka, hili litawezekana kama Halmasahuri zitaweka bajeti ya Uwezeshaji mafunzo haya kwa Watalaamu wake.
Ukitembelea Taasisi za Elimu (VYUO VIKUU) vina Wataalamu special kwa ajili ya kusimamia Mpango Mkakati wa Taasisi zao, Taasisi za Elimu zinafanikiwa katika utekelezaji wa Mipango Mikakati yao kwa Sababu Wamewekeza katika Idara za Mipango.
Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu Mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
KAZI IENDELEE