Opulukwa, mbunge wa Meatu; tetea wapiga kura wako wanaohamishwa kwa nguvu na Serikali ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Opulukwa, mbunge wa Meatu; tetea wapiga kura wako wanaohamishwa kwa nguvu na Serikali ya CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by naggy, Nov 7, 2011.

1. n

naggy Member

#1
Nov 7, 2011
Joined: Apr 27, 2011
Messages: 80
Likes Received: 17
Trophy Points: 15
Kaya zaidi ya 600 wilayani Meatu katika vijiji vya Makao, Mwangudo na Sungu wametakiwa kuondoka katika maeneo yao halali waliyokuwa wamemilikishwa na serikali ya vijiji hivyo bila fidia na bila kuoneshwa sehemu ya kwenda. Tamko hili limetolewa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambaye ni mpya katika ziara maalum iliyofanywa mwihoni mwa wiki iliyopita. Tayari polisi wameanza kwenda maeneo hayo kupiga kambi ili kutekeleza agizo hilo. Serikali inawatoa watu hawa kwa nguvu baada ya kukaidi amri ya kuondoka kwa hiyari. Wananchi wanaondolewa eneo hili ili kumpisha muwekezaji mzungu wa kampuni ya MWIBA inayojihusisha na utarii katika hifadhi ya Ngorongoro.

Mzungu huyu ametoa takrima kama ifuatavyo:
1. Mkuu wa mkoa aliyeondoka alipewa eneo kubwa kama hekari 100 hivi
2. Serikali ya kijiji cha Makao kilipewa gari na huyo mzungu
3. Polisi Meatu wamepewa piki piki tano mpya
4. Mwenyekiti wa halimashauri inasemekana alishakula milioni zake kadhaa
5. Mkuu wa wilaya nae kapewa gari ambalo mke wake anatembelea
Je, katika mazingira haya, Serikali inathamini wananchi wake? Kwa nini kama ni lazima kuondoka wasipewe maeneo ya kwenda?

OMBI:
Tunaomba mbunge wa CHADEMA mh. Opulukwa awatetee wapiga kura wake kwani aliwaahidi wakati wa kampeni zake mwaka jana kuwa hawatahamishwa bila kutengewa maeneo ya kwenda na ndiyo maana alishinda. Ikiwezekana uongozi wa CHADEMA Taifa uingilie kuwatetea hawa wananchi!

2. Mr Rocky

Mr Rocky JF-Expert Member

#2
Nov 8, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 15,186
Likes Received: 570
Trophy Points: 280
Naomba nitofautiane na wewe mtoa mada kwa kiasi kikubwa na kabla hujaleta topic kama hii ungefanya utafiti ukajua ukweli wa hali halisi iliyoko kwenye eneo kabla ya kuanza kuwasemea hao wananchi

Eneo hilo unaloliita la Makao si eneo la kijiji kimoja. Hicho unachosema Makao ni kijiji kimoja katika vijiji ambavyo viko wilaya ya meatu kata ya kimali
Eneo ambalo kwa sasa ndilo lenye mgogoro ni eneo la Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao ambalo ni karibu Hekta Elfu Sabini (70,000 Ha) ambalo ni muunganiko wa vijiji saba ambavyo ni Makao, Mwangudo, Sapa, Mwabagimu, Ginamo, Mbushi, Iramba Ndogo.

Kwa mujibu wa Kanuni za Hifadhi (maeneo ya Hifadhi za Wanyamapori) za mwaka 2005, eneo hilo lilitengwa na vijiji tajwa hapo juu kwa ajili ya kuanzisha Hifadhi ya Wanyamapori. Mchakato wa uanzishaji wa hifadhi hii ya wanyamapori ulianza kuanzia miaka ya 1998 na vijiji tajwa vilianza mchakato wa kutenga maeneo kutoka kwenye ardhi zao kwa ajili ya kuanzishwa kwa hifadhi hii. Kanuni tajwa hapo juu zinajieleza kwa kirefu juu ya namna ya kuanzisha maeneo haya ya hifadhi ya wanyamapori.

Kila kijiji kinachotaka kuanzisha Hifadhi hizi za wanyamapori (Wildlife management Area WMA) ni lazima kwanza kikae kwenye Kikao cha serikali ya kijiji kukubali kutenga eneo kwa ajili ya WMA husika na makubaliano yatakayofikiwa ni lazima yapelekwe kwenye mkutano Mkuu wa Wanakijiji wa Kijiji husika. Mkutano Mkuu wakikubali taarifa inafikishwa kwenye uongozi wa Wilaya.

Kila kijiji kina kamati ya ardhi ambayo nayo baada ya azimio hilo kupitishwa wanakutana na wataalam wa wilaya husika kutengeneza Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi (Land Use Management Plan LUP) ambayo huwa inatenga maeneo ya malisho, kilimo, makazi, msitu kwa kila kijiji husika kulingana na matumizi ya ardhi yaliyo katika kijiji husika. Kama kijiji hakina mifugo kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi hakutakuwa na ardhi kwa ajili ya mifugo au kama kijiji hakiendeshi kilimo na suala lao kubwa ni ufugaji kwenye mpango huo wa matumizi ya ardhi hakutakuwa na eneo la matumizi hayo

Mpango huo ukiwa ni pamoja na upimaji wa ardhi husika ukishamalizika ni lazima tena urudishwe kwenye Kikao cha Serikali ya kijiji kujadiliwa na kupitishwa na baadae kwenye mkutano mkuu wa kijiji. Mpango huo na ramani ya kijiji husika ni lazima upelekwe wilayani pia ambapo mpango huo ni lazima ukubaliwe na kupitishwa pia na wilaya. Ramani ya kijiji husika hapo inapelekwa kwa Director of Mapping ambapo kwa ushirikiano na wilaya watayayarisha pia Cheti cha Ardhi Cha kijiji.

Wakati mchakacho huo wa kutayarisha Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi na Ramani ya kijiji unaendelea, mchakato wa uundaji na usajili wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori unaendelea kwa kuyatarisha Katiba ya Jumuiya na kanuni za uendeshaji wa jumuiya husika. Mchakato mzima wa uanzishaji na usajili umeelezwa vizuri katika Kanuni nilizozitaja hapo juu.

Swala linalopiganiwa hapa ni kuwa wananchi hao wana haki ya kukaa katika eneo hilo.
Ieleweke kuwa mchakato wa kuanzishwa na kusajiliwa mpaka kupata haki ya Matumizi ya rasilimali (User Rights) kwa jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori na kupata usajili kwa msajili wa jumuiya wizara ya mambo ya ndani ni wa muda. Vile vile kazi ya kutayarisha Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi kwa kila kijiji na kupiotishwa na vikao vyote na wilaya husika ni wa muda mrefu. Kuianzisha jumuiya hii na kupata vibali vyote ilianza toka mwaka 1998 na mchakato mzima ulimalizika mwaka 2010 ambapo ni miaka 12.

Maeneo hayo ambayo wanavijiji hao wanalalamika sio kwamba yalikuwa hayana wenyewe ila wanavijiji wa vijiji husika walikwishayyatenga kuwa maeneo kwa ajili ya hifadhi ya wanyamapori. Kukaa kwao zaidi ya miaka kumi hakuhalalishi kuwa wao ni wakazi halali wa maeneo hayo maana yalikwishatengwa na vijiji husika kuwa ni ya hifadhi ya wanyamapori.

Walihamia na kuweka makazi wakijua kuwa haya sio maeneo ya makazi wala kulishia mifugo na ipo siku wataondolewa. Wengi wao sio wakazi wa vijijiji husika na walitoka maeneo ya mbali kama bariadi na singida na kaskazini mwa Ziwa Eyasi na wilaya nyingine za mkoa wa shinyanga kwa ajil;i ya kutafuta malisho ya mifugo na ardhi kwa ajili ya kilimo.

Kila kijiji kilitenga maeneo ya matumizi ya ardhi yake kulingana na idadi ya mifugo au wakazi wake au shughuli nyingine za kiuchumi. Vijiji hivyo kwa sasa vimelemewa na mifugo ambayo inatoka maeneo ya mbali ya wilaya hiyo na wakazi wageni ambao wanatoka mbali na wilaya husika.

Sikubaliani wala sijaufurahia uhamishaji huo ambao wanaohamishwa hawaonyeshwi sehem mbadala za kuhamia. Ila eneo hilo lilityengwa kisheria kwa makubaliano na mikutano ya pamoja na wananchi haop hao klukubali kuwa eneo hilo liwe hifadhi ya wanyamapori ya makao. Walikubali kutoa ardhi zao kwa ajili hiyo na kwa mujibu wa kanuni eneo likishatengwa hakuna mifugo au makazi yatakayoruhusiwa au kilimo kuendeshwa kwenye eneo hilo.

ningeshauri zaidi hisia za kisiasa zisiwe kwenye zoezi hili wala kusiwe na uCCM na UCHADEMA ila utaifa zaidi uwepo na busara zitumike katika kuwahamisha watu wao. Ningependelea zaidi compromise kati ya pande zote mbili kukaa pamoja na kukubaliana nini wafanye. Ikiwa ni pamoja na kupunguza hata ukubwa wa eneo la WMA la kama Hekta 30,000 na kuwapanga vyema wakazi hao kwa ajili ya matumizi yao. Naelewa ni hatua ngumu kufuata katika kupunguza eneo la WMA maana itahitajika hatua zile zile zilizotumika kulianzisha zifuatwe ila ni busara kutumia hatua ngumu kuliko kuleta uvunjifu wa amani na uharibifu wa mali.

Napenda nisiwe mjibu tuhuma ila waliotuhumiwa watajibu wenyewe ila napenda kutoa mawazo yangu hayo kwa upande wa eneo hilo la WMA ya Makao kama mdau wa uhifadhi wa mazingira na mkazi wa kijiji cha makao mojawapo ya vijiji vinavyounda WMA ya Makao.

3. M

Mr. Clean Senior Member

#3
Dec 1, 2011
Joined: Aug 7, 2006
Messages: 195
Likes Received: 1
Trophy Points: 35
Tatizo viongozi wa serikali wanaficha taarifa na kupotosha,

niliona picha zile wakati mgambo wanachoma na kuharibu mazao ya wananchi wale,,

lakini mkuu wa mkoa akatoa taarifa kuwa hakuna nyumba ilochomwa moto, na wala hakuna mtu alipigwa!

Loading...