Opras

MPINGE

Member
Apr 20, 2013
43
4
Ndugu wana jf kwa yeyote aliye na elimu ya namna ya kujaza fomu za taarifa za mwalimu juu ya utendaji wa kazi ulio wazi serikalini kwani tumeletewa huu mfumo ambapo serkali haijato elimu ya kutosha nini cha kujaza katika hizo fomu.
 
[QUOTE=nyamatarekwetu;80158:teeth:
Kamuone afisa utumishi wako kwa msaada zaidi maana kila idara kuna tofauti kidogo kwenye ujazaji wake.
 
La msingi ni watumishi kuwajibika, ila naona tafrisri yake imegeuka kujaza mifomu isiyoeleweka!
 
Kujaza fomu ni sawa na kujibu maswali ya mtihani. Unataka ufundishwe hata kujaza jina lako? Kweli shule za kata balaa...!
 
Ndugu wana jf kwa yeyote aliye na elimu ya namna ya kujaza fomu za taarifa za mwalimu juu ya utendaji wa kazi ulio wazi serikalini kwani tumeletewa huu mfumo ambapo serkali haijato elimu ya kutosha nini cha kujaza katika hizo fomu.

Ni kitu kizuri theoretically, lakini hakitekelezeki, karatasi zinapotea bure.

OPRS form: http://www.utumishi.go.tz/index.php?option=com_docman&task=doc_download&gid=386&Itemid=0

GUIDELINES: http://www.tanzania.go.tz/egov_uploads/documents/OPRAS-Guidelines_Rev_September_2011_sw.pdf
 
Opras ni kitu kisichotekelezeka ingawa kinang'ang'aniwa na wizara husika, tangu tulipoanza kuisikia sijashuhudia Taasisi iliyoweza kutekeleza utaratibu huu. Kinadharia kinaonekana ni kitu rahisi na chenye kuondoa kupendeleana na kuoneana ingawa kupo palepale kwani mnakaa wawili mpimaji na mpimwaji, na uwezekano wa kuyapoza mambo yanayoonekana kumzidi mmoja wao upo, kwani ni suala la kuelewana ki ukanjanja kanjanja na mambo yanaenda. Bora turudi tulikotoka.
 
wewe bwana na halmashauri yako ya Mbozi nenda ukaonane na viongozi wako watakusaidia!!
 
Kujaza fomu ni sawa na kujibu maswali ya mtihani. Unataka ufundishwe hata kujaza jina lako? Kweli shule za kata balaa...!

Kama kitu hukifahamu,si lazima kuchangia,unapita tu!Hizo form unaonekana huzijui ni bora ukanyamaza,kwa taarifa yako sio mtihani kama unavyodhani.Unajaza form yako pamoja na kiongozi wako,kwa mwl atakuwa mwl wake mkuu.Kiufupi zile form ziko hivi,mfano katika familiya ina malengo fulani kwa mwaka hayo ni malengo ya baba,watoto wanachukua yale malengo ya baba bila kubadilisha kitu basi wanagawana yanakuwa ndiyo malengo yao kwa mwaka na wanatakiwa kuyakamilisha na kutaja sababu za kutokamilika endapo hayatatimia.Kwa hiyo huwezi kuzijaza hizo fomu peke yako,ni lazima mshirikiane na bosi wako na wafanyakazi wote kwa ujumla ili kuhakikisha malengo yenu kama yalivyoainishwa kwenye mpango mkakati wenu wa mwaka ndiyo yanayoorodheshwa na yanatimizwa
 
We acha wogaa, kama hujapewa semina utajaza nini, -----? Jf isingekuwepo ungeuliza wapi? Mwenyewe n mwl na hizo form nilipewa tangu 2011 bila maelekezo ya namna ya kuzijaza, niliziweka kabatini hadi jana nilipopekua nikakuta zimetafunwa na panya,lkn mbona daraja nmepanda mwaka huu bila kujaza Opras? Tatizo letu walimu woga umezidi ila niombeeni mungu nataka kuanzisha harakati kupigania haki za walimu nchi nzima. Siogopi kung'olewa kucha!!!
 
Back
Top Bottom