Opposition parties jipangeni - achianeni Majimbo ya uchaguzi

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,460
Wana Jf, This is just a Reminder to all opposition parties.

Ningependa Vyama vya upinzani wasiwe maadui, wakae pamoja waangalie majimbo yate ya uchaguzi waweke tathimini ili wayagawane na msaidiane kupiga kampeni, hii itasaidia kupata viti vingi ya ubunge.

Mnajenga nyumba moja sasa kuna haja ya kugombea fito, kwa nini msikubaliane? kwa mfano Mrema anakubalika vunjo kwa nini chadema au NCCR mkampa support? Dr Slaa karatu sasa hakuna haja ya vyama vingine kupoteza nguvu pale bora wazielekeze sehemu wanayokubalika. Njia hii itasaidia kuinyon'gonyeza CCM.

Sisi watanzania shida yetu si chama gani kitawale dola, shida yetu tupate haki zetu za msingi kama wananchi wa nchi yetu, mkiwa nusu kwa nusu bungeni hapo hata hii miswaada isiyo ya tija kwetu kamwe haitapita ovyo ovyo.

Onyesheni upendo na mshikamano nyie wenyewe kwanza pia support mtapata toka kwetu. tumechoka na malumbano, kunyanganyana wanachama na kusemana semana tu tunaondoa imani kwa wananchi. mfano mwanachana anatoka chama A cha Upinzania anahamia chama B then anaanza anatoa kashfa ya chama chake cha zamani.

Msipofanya hivyo itakuwa ngumu sana kwa watanzania kuwaamini mkizingatia watanzania karibu 80% wapo vijijini na CCM ni rahisi kuwazoa wote.

Pia kitendo cha kila chama kuweka mgombe kiti cha uraisi mimi huwa sioni mantiki yake, labda kama mtu anataka aingie kwenye kumbukumbu tu kuwa naye alishawahi kugombea urais wa nchi yetu.

Kama hamtataka kuweka mgombea mmoja basi Wenyeviti wote wa Vyama vya upinzani naomba mrudi majimboni mgombee ubunge ili tuongeze idadi ya uwakilishi kwanza, urais utakuja tu kadri tunavyoisogelea CCM.
 
Wana Jf,

Ningependa Vyama vya upinzani wasiwe maadui, wakae pamoja waangalie majimbo yate ya uchaguzi waweke tathimini ili wayagawane na msaidiane kupiga kampeni, hii itasaidia kupata viti vingi ya ubunge.

Mnajenga nyumba moja sasa kuna haja ya kugombea fito, kwa nini msikubaliane? kwa mfano Mrema anakubalika vunjo kwa nini chadema au NCCR mkampa support? Dr Slaa karatu sasa hakuna haja ya vyama vingine kupoteza nguvu pale bora wazielekeze sehemu wanayokubalika. Njia hii itasaidia kuinyon'gonyeza CCM.

Sisi watanzania shida yetu si chama gani kitawale dola, shida yetu tupate haki zetu za msingi kama wananchi wa nchi yetu, mkiwa nusu kwa nusu bungeni hapo hata hii miswaada isiyo ya tija kwetu kamwe haitapita ovyo ovyo.

Onyesheni upendo na mshikamano nyie wenyewe kwanza pia support mtapata toka kwetu. tumechoka na malumbano, kunyanganyana wanachama na kusemana semana tu tunaondoa imani kwa wananchi. mfano mwanachana anatoka chama A cha Upinzania anahamia chama B then anaanza anatoa kashfa ya chama chake cha zamani.

Msipofanya hivyo itakuwa ngumu sana kwa watanzania kuwaamini mkizingatia watanzania karibu 80% wapo vijijini na CCM ni rahisi kuwazoa wote kirahisi.

Pia kitendo cha kila chama kuweka mgombe kiti cha urahisi mimi huwa sioni mantiki yake, labda mtu aingie kwenye kumbukumbu tu kuwa naye alishawahi kugombea urais.

Kama hamtataka kuweka mgombea mmoja basi Wenyeviti wote wa Vyama vya upinzani naomba mrudi majimboni mgombee ubunge ili tuongeze idadi ya uwakilishi kwanza, urais utakuja tu kadri tunavyoisogelea CCM.

Heshima kwako ELNIN0,

Haya ni maombi ya kila mwananchi anayeipenda Tanzania.Hili limekuwa tatizo la upinzani kwa muda mrefu wameshindwa kuungana wakati wa uchaguzi .Uchaguzi wa mwaka 2005 kuna baadhi ya majimbo ya uchaguzi upinzani ulishinda lakini kwasababu ya kugawa kura walijikuta wanatoa mwanya CCM kushinda.Mfano mzuri ni Vunjo kura walizopata wapinzani zilikuwa nyingi kuliko walizopata CCM hivyo hivyo kwa jimbo la Arusha mjini CCM pamoja na kuiba kura bado TLP ikifuatiwa na CHADEMA walikuwa na kura nyingi.
 
Back
Top Bottom