Opposition MPs to lead key Bunge committees: Lowassa in; is this a positive move?

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Habari hii iko kwenye gazeti mahili la ThisDay. Je, uamuzi wa kubadilishwa na kuwekwa kipengele kama hiki 113 (10) katika kanuni za Bunge kuna ubora gani au kuna athari gani kwenye kambi za upinzani Tanzania?!

Kuna wengi walipinga na kuhoji kwa nguvu pale Mh. Zitto alipoteuliwa kwenye kamati ya madini (report inasubiriwa kwa hamu), na kuna wengi pia walipinga na kuhoji uteuzi wa Mh. Mwakyembe kwenye kamati ya Richmond kabla ya matokeo yake kutolewa na kusababisha kuporomoka kwa baraza la mawaziri kwa vile tu alikuwa anatoka chama tawala. Sasa je hoja kama hizi zitumike hapa pia?...

Opposition MPs to lead key Bunge committees

-Zitto, Slaa, Cheyo, Hamad Rashid all named as front-runners

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

A NUMBER of leading opposition members of parliament are set to be given chairmanship positions in sensitive parliamentary sub-committees following the adoption of new National Assembly standing orders which give the opposition camp in parliament an exclusive mandate to head such committees.

According to THISDAY's findings, high-riding opposition MPs now in line for chairmanships in some of the committees include Zitto Kabwe (Kigoma North - CHADEMA), Dr Wilbrod Slaa (Karatu-CHADEMA), John Cheyo (Bariadi East-UDP), and Hamad Rashid Mohamed (Wawi-CUF).

The new parliamentary standing orders as prescribed under section 113 (10) require that opposition MPs head committees that deal with monitoring public expenditure, public institution and local government accounts.

Names which are being particularly singled out include that of Kabwe, touted to chair the newly-established Public Organizations Committee (POC) which will deal with institutions like the Bank of Tanzania (BoT), the National Social Security Fund (NSSF), and others.

Dr Slaa is a frontrunner to head the Parliamentary Local Authorities Accounts Committee which will scrutinize how all regional and district councils make use of taxpayers' monies.

Meanwhile, a tug-of-war is building up between Cheyo, the incumbent parliamentary Public Accounts Committee chairman, and Hamad Rashid who is now vying for the seat.

According to well-informed observers interviewed by THISDAY, Hamad Rashid is seen to be in a good position to wrestle the PAC chairmanship from Cheyo, who is believed to have become less avid in questioning irregular government expenditure in recent times.

The House Speaker, Samwel Sitta, confirmed to THISDAY yesterday that opposition MPs will indeed head the three powerful committees following adoption of the new standing orders.

Sitta said House rules endorsed by parliament at the last session have become effective and are applicable from today, when the committees start meetings in Dar es Salaam.

''The parliamentary standing orders are already in place and take effect when the parliamentary committees begin their meetings for the elections of chairpersons for various committees,''' he said.

Yet another fierce battle is expected when outspoken CCM legislator Anna Kilango Malecela (Same East) takes on the former good governance minister Wilson Masilingi (Muleba North-CCM)) for the chair of the Parliamentary Ethics and Privileges Committee.

Ms Malecela is touted as favourite to win the seat.
Source link: http://www.thisday.co.tz/News/3679.html

SteveD.
 
Steve naona ume raise issue nzuri sana. Unajua bado tuna ile akili ya kuona watu wa CCM watatetea ufisadi na watu wa upinzani ni wababaishaji, au wengine wanaona kama ni kuwapa edge ya kupunguza nguvu ya CCM. Lakini hii ya Mwakyembe imeonesha hali tofauti, kwamba uzalendo kwa nchi ni muhimu kwanza, chama kinafuata baadaye kama uzalendo umelindwa.
Mimi naona hata opposition wanaweza, as long as wana uzalendo kwa nchi na uwezo.
 
Kwanza naomba kujua, nguvu ya Mwenyekiti wa hizo Kamati ni kubwa kiasi gani na wigo wa kutumia hiyo nguvu yake ni mpana kiasi gani? Baada ya kujua hayo ndipo tunaweza kujadili kwa mapana na marefu.

Lakini hata hivyo, kwa Bunge ambalo liko dominated na chama kimoja hata Mwenyekiti awe na nguvu kiasi gani bado kunaweza kuwa na matatizo kwenye kupitisha hoja nzito na hasa kama wabunge wa chama tawala hawataki hoja hiyo ipite. Mwenyekiti anaweza kujikuta yeye na wajumbe 10 tu wanataka hoja ipite wakati wajumbe wengine 70 wanasema NO. Kwenye mazingira kama hayo bado kuna ugumu wa kutosha.

Kanuni kama hiyo ni nzuri na inasaidia sana kama Bunge liko balanced kwenye idadi ya wabunge na kwenye kamati. Bunge lililopita la Kenya, kuna baadhi ya mambo serikali ilikuwa inagoma yasifanyike lakini Kamati zilikuwa zinalazimisha kwa kuwa wapinzani walikuwa na numbers kwenye hizo kamati. Sasa kamati za Bunge la Tanzania wapinzani ni wachache sana na hivyo wanakosa sauti/nguvu ya kulazimisha jambo lifanyike. Maana demokrasia inasema hoja ikiwa moto kura ipigwe ili uamuzi ufanyike, na kama mchuano ukiwa droo ndipo Mwenyekiti anatumia "busara" ama kura yake ya turufu. Kura ya turufu haina nguvu kwa upande wa upinzani kwenye Bunge la Tanzania kwa kuwa idadi ya wapinzani ni ndogo.

Ukombozi wa kweli kwa watanzania utakuja kwa kuongeza kwanza idadi ya wabunge kutoka upinzani na hilo ndiyo litapandisha joto la kudai katiba mpya na hatimaye tutakuwa na uchaguzi huru na wa haki, madaraka ya rais yatapungua na mambo mengine mengi mabaya yaliyo kwenye katiba yatafanyiwa marekebisho kwa maslahi ya watanzania na siyo kwa maslahi ya serikali iliyo madarakani.
 
Kwanza naomba kujua, nguvu ya Mwenyekiti wa hizo Kamati ni kubwa kiasi gani na wigo wa kutumia hiyo nguvu yake ni mpana kiasi gani? Baada ya kujua hayo ndipo tunaweza kujadili kwa mapana na marefu.

Lakini hata hivyo, kwa Bunge ambalo liko dominated na chama kimoja hata Mwenyekiti awe na nguvu kiasi gani bado kunaweza kuwa na matatizo kwenye kupitisha hoja nzito na hasa kama wabunge wa chama tawala hawataki hoja hiyo ipite. Mwenyekiti anaweza kujikuta yeye na wajumbe 10 tu wanataka hoja ipite wakati wajumbe wengine 70 wanasema NO. Kwenye mazingira kama hayo bado kuna ugumu wa kutosha.

Kanuni kama hiyo ni nzuri na inasaidia sana kama Bunge liko balanced kwenye idadi ya wabunge na kwenye kamati. Bunge lililopita la Kenya, kuna baadhi ya mambo serikali ilikuwa inagoma yasifanyike lakini Kamati zilikuwa zinalazimisha kwa kuwa wapinzani walikuwa na numbers kwenye hizo kamati. Sasa kamati za Bunge la Tanzania wapinzani ni wachache sana na hivyo wanakosa sauti/nguvu ya kulazimisha jambo lifanyike. Maana demokrasia inasema hoja ikiwa moto kura ipigwe ili uamuzi ufanyike, na kama mchuano ukiwa droo ndipo Mwenyekiti anatumia "busara" ama kura yake ya turufu. Kura ya turufu haina nguvu kwa upande wa upinzani kwenye Bunge la Tanzania kwa kuwa idadi ya wapinzani ni ndogo.

Ukombozi wa kweli kwa watanzania utakuja kwa kuongeza kwanza idadi ya wabunge kutoka upinzani na hilo ndiyo litapandisha joto la kudai katiba mpya na hatimaye tutakuwa na uchaguzi huru na wa haki, madaraka ya rais yatapungua na mambo mengine mengi mabaya yaliyo kwenye katiba yatafanyiwa marekebisho kwa maslahi ya watanzania na siyo kwa maslahi ya serikali iliyo madarakani.

Kwa kuongezea alichoandika Keil, Bunge la Tanzania ni bado Bunge ambalo limetawaliwa na CCM, hivyo kama wenyekiti wa kamati hizi kama hawatapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wabunge wa CCM hawatafanikiwa chochote na mwishowe CCM itarudi kwa wananchi na kurusha lawama za utendaji mbovu wa kamati hizo kwa vyama vya upinzani, maana mafanikio ya kamati hizo ni mafanikio ya vyama vya upinzani na wanaweza kabisa kuyatumia mafanikio hayo kujipigia debe katika uchaguzi ujao. Kitu ambacho kinaruhusiwa kabisa. Tusubiri tuone mwelekeo wa hili.
 
Habari hii iko kwenye gazeti mahili la ThisDay. Je, uamuzi wa kubadilishwa na kuwekwa kipengele kama hiki 113 (10) katika kanuni za Bunge kuna ubora gani au kuna athari gani kwenye kambi za upinzani Tanzania?!

Kuna wengi walipinga na kuhoji kwa nguvu pale Mh. Zitto alipoteuliwa kwenye kamati ya madini (report inasubiriwa kwa hamu), na kuna wengi pia walipinga na kuhoji uteuzi wa Mh. Mwakyembe kwenye kamati ya Richmond kabla ya matokeo yake kutolewa na kusababisha kuporomoka kwa baraza la mawaziri kwa vile tu alikuwa anatoka chama tawala. Sasa je hoja kama hizi zitumike hapa pia?...


Source link: http://www.thisday.co.tz/News/3679.html


SteveD.

SteveD,

Mimi ni miongoni mwa hao uliowataja hapa kuwa tuliuliza maswali mengi sana kuhusu (soma kuwa tulipinga) uteuzi wa Zitto kwenye kamati ya madini kama ule wa Mwakyembe kwenye kamati zote mbili.

Naomba nikuhakikishie kuwa maswali na mijadala mikali kwenye issuez kama hizi lazima yawepo na kwa kweli huu ni mjadala mkali sana hapa ambao unaweza kupelekea utendaji mzuri kwenye hii issue kama hii story ya Thisday itawekwa kwenye vitendo.

Kwa kuanzia tu, inawezekana kuwa hili ni wazo zuri na ukianza na mfano wa bunge la kenya, Kamati muhimu ya business huwa inakuwa na wabunge sawa kutoka serikalini na upinzani bila kujali idadi ya vyama bungeni. Nadhani huu ni mwanzo mzuri ingawa pia itategemea ni kina nani wanakuwa kwenye hizo kamati.

Asante kwa mada hii!
 
Kuwaweka Lowassa na Msabaha kwenye kamati za Bunge ni usanii wa hali ya juu. Hawastahili kupewa hata ujumbe wa nyumba kumi kumi.

Ex-PM picked for House defence committee
JAFFAR MJASIRI
Daily News; Tuesday,March 18, 2008 @19:01

FORMER Prime Minister and Monduli MP (CCM) Edward Lowassa and former East African Co-operation Minister and Kibaha Rural MP (CCM) have been selected to the Parliamentary Foreign Affairs, Defence and Security Committee.

In the elections for various parliamentary committees held in Dar es Salaam today, Opposition legislators Dr Willbrod Slaa (Karatu-Chadema) and Zitto Kabwe (Kigoma North-Chadema) were elected chairpersons for the Local Government Accounts Committee and the newly formed Public Corporation Accounts Committee respectively.

Mr Lowassa and Dr Msabaha resigned from their positions last month after being mentioned in the report tabled by a parliamentary select committee that probed the Richmond power supply deal. The committee revealed that there were gross irregularities in awarding the multi-billion-shilling emergency power supply contract to Richmond Development Company.

Five former ministers have also been picked for Parliamentary Committee for Industry and Trade. These include former energy and minerals minister and Bukoba Rural MP Nazir Karamagi, former deputy minister for finance Abdisalaam Issa Khatibu and Makunduchi MP and former home affairs minister and Mufindi North MP Joseph Mungai. Mr Khatibu would also chair the committee.

Mr Karamagi also resigned following the tabling of the Richmond report. The former minister for public safety and security and MP for Tanga, Mr Bakari Mwapachu, and the former Minister for Industry, Trade and Marketing and Rombo MP Basil Mramba were also appointed members of the committee.

Igunga MP Rostam Aziz, who was also mentioned in the Richmond report, was also picked industry and trade committee member. Same East MP (CCM) Anne Kilango Malecela was elected chairperson of the non-portfolio Justice and Ethical Committee in addition to serving as vice- chairperson of the Infrastructure Committee.

Meanwhile, speaking to the ‘Daily News’ shortly after being elected, Dr Slaa vowed to continue spearheading the war against embezzlement of public funds especially in projects established in rural areas. He explained local government officials were taking advantage of ignorance of rural population to squander funds in rural areas.

“Of course they collude with some contractors and construct substandard schools, dispensaries and other facilities,” he lamented. Dr Slaa said the current effort undertaken by donors and Civil Society Organisations of introducing Public Expenditure Tracking System (PETS) in rural areas was the right step in the right direction.

“The rural communities ought to be empowered to question the value for money for whatever projects undertaken in their areas,” he charged. The Bunge office today will hold a seminar for the MPs to discuss the proposed bill for Petroleum and Electricity Supply. Last month, a similar seminar was stopped halfway when MPs led by Mrs Malecela demanded debate of the Richmond report first before discussions could start on the proposed bills.
 
Ni Tanzania au nchi za Afrika pekee ambapo Majambazi hupongezwa kutokana na kuiba kwao kwa kupewa nafasi nyingine nyeti katika jamii ili waendelee kuiba na kula posho za bure. Yaani haingii akilini kabisa, tena unakuta mijitu mingine hapa hapa JF iko tayari kukesha kwenye internet ikiwatetea hawa majambazi na yule bwana wao Rostam Aziz. Hawa watu wako tayari waone nchi inabakwa rasilimali zake na mapato yake lakini hawa majambazi wasiguswe na wala wasifikishwe mbele ya sheria. Kumpa jambazi Lowassa cheo chochote ni sawa na kuwatukana Watanzania wote. Hii inakuwa kama ni kuhamasisha wengine waendelee kuiba au wajifunze kuiba ili mradi tu uwe mwanachama wa Chama Cha Majambazi(CCM)basi hakuna mtu atakayekugusa na utakuwa rewarded.

Najua Lowassa na majambazi wenzako mtakuwa mnajipongeza kutokana na kuchaguliwa kwenu kuzidi kuwaibia watanzania, Lakini kumbukeni iko siku yenu ambapo yale machozi ya masikini wote wa Tanzania ambao wanaathiriwa kila siku kutokana na vitendo vyenu yatakuja kuwadhuru. Najua ni furaha tele kwenu mkiwa mnazunguka kwenye gari zenu za kifahari zenye viyoyozi huku mamilioni ya watanzania wakishindwa kununua hata baiskeli au kuweka chakula mezani kwa familia zao kutokana na ugumu wa maisha. Iko siku yenu Majambazi wa CCM na wapambe wenu wote ambao wako hapa wakijaribu kuwatetea usiku na mchana ili muendelee kuiba.
 
Mapendekezo yangu kwa Zitto na Dk slaah
Kataeni kabisa hao watu kuwa kwenye kamati zenu kama inawezekana, kwa sababu hao ni Mafisadi na watawaharibia kazi zenu
Hao wananuka na wamekulia katika mazingira ya kuiba pesa za walalahoi
Kama ikishindikana nawaomba muachie huo uwenyekiti wa hizo tume teuli, ili kuepuka kufanya kazi na Mafisadi, ili kulinda heshima yenu katika jamii na taifa.
Naomba kutoa pendekezo
Zitto usimsikilize huyu,

Ukipewa hela KULA.

Dawa ya moto si moto tena, wakiingizwa kwenye kamati ulimo kaa nao na waambukize u-anti-ufisadi. Wanaweza kubadilika.

Hakuna wa kuwaharibia kazi zenu, jaribu kuangalia maslahi ya taifa na mara zote mtangulize Mungu katika kazi zenu. Mkifanya ufisadi wa aina yoyote (uchafu nikimaanisha) hatutawaonea huruma kisa ninyi ni kina flani. Tutawaandika laivu ili watanzania wawajue. Jifunze kuwa wasafi na Mungu mwenye Upendo atawatangulia daima. Mna mapungufu yenu lakini msikubali yachukue nafasi zaidi ya taifa lenu.

Dada Tina
 
1. Heshima kwa Spika kwa kuwapa kazi nzito mashujaa wetu wa taifa Zitto, Dr. Slaa, na Mama Malecela, nahisi bunge lijalo litakuwa na moto wa kuotea mbali.

2. Wakuu Bubu, Bob, na Mazee Geeque, mmesema yote hakuna cha kuongeza, it is pathetic na haielezeki ila only in Tanzania,

However, ninajua kwa taratibu za bunge, ex-PM, huomba in personal kwa Spika nafasi kweye kamati anayotaka, meaning kwamba hapa Lowassa ameomba kuwemo kwenye kamati ya wizara ya rafiki yake wa damu, Nchimbi, je anataka nini huko?
 
Wakuu, hivi kama ndio utaratibu wa bunge kuwa ex-PM anaweza kuomba nafasi katika kamati anayotaka, sasa je spika ana uwezo wa kumkatalia? Kama anao kwanini hakufanya hivyo? Kama hana, kwanini?
 
Only in Tanzania.......

kulikuwa na hii pia:


Lowassa nje kamati za Bunge


Spika Sitta apata kigugumizi kufafanua



na Irene Mark



SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta, amemwacha nje ya kamati za kudumu za Bunge hilo, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kwa madai ya kutojaza fomu.
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima umebaini kwamba, Lowassa ni miongoni mwa wabunge wasio na madaraka serikalini kwa sasa, ambao wameachwa nje ya kamati zote 17 zilizotangazwa na Spika Sitta wiki iliyopita.

Taarifa ambazo gazeti hili limezipata kutoka ndani ya Bunge zinaeleza kuwa kwa kawaida wabunge wote wasio mawaziri wanapaswa kuwa wajumbe katika moja ya kamati hizo za kudumu na kabla ya kufanya hivyo hutakiwa kuomba kwa kujaza fomu maalumu.

Kwa mujibu wa habari hizo, kujaza au kutojaza fomu kwa mbunge bado hakuwezi kumzuia spika kumtea mbunge katika kamati yoyote ambayo anaamini mhusika atafaa kutokana na uzoefu au utaalamu alionao katika eneo husika.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana jioni, kuhusu kutokuwamo kwa Lowassa katika orodha ya wajumbe wanaounda kamati hizo za Bunge, Sitta alisema wakati wabunge wengine wanajaza fomu hizo, Lowassa alikuwa waziri mkuu, hivyo hakutakiwa kujaza.

“Ni kwa sababu wakati wabunge wengine wanajaza fomu katika mkutano ule za kuomba kuwa wajumbe wa kamati mbalimbali, yeye (Lowassa) alikuwa waziri mkuu hivyo hakustahili kuzijaza.

…Sasa, yalipotokea ghafla akajiuzulu, akaenda jimboni kwake, hakuweza kujaza. Baada ya hapo aliporudi Bunge nalo likawa limemaliza muda wake.

Mmmh, hakuna tatizo lakini anaweza kujaza wakati wa mkutano ujao,” alisema Sitta na kumaliza mazungumzo hayo kwa kukata simu.

Aidha, Februari 7, mwaka huu wakati wa kikao cha Bunge, Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, alitangaza kujiuzulu baada ya Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyopewa dhamana ya kuchunguza mkataba tata wa kuzalisha umeme wa Kampuni ya Richmond Development uliodaiwa kugubikwa na vitendo vya rushwa na ufisadi, Dk. Harrison Mwakyembe, kumtaka awajibike.

Lowassa, alijiuzulu katika nafasi ya uwaziri mkuu baada ya kuhusishwa na kashfa ya ufisadi kwenye mkataba dhalimu unaliolisababishia taifa hasara ya sh bilioni 172.9.

Kutokana na mkataba huo, taifa linaendelea kupata hasara ya sh milioni 152 kila siku kwa kuilipa Kampuni ya Dowans Holdings iliyorithi mkataba huo, mapema mwaka jana.

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, waziri yeyote haruhusiwi kuwa mjumbe wa kamati za Bunge, kwa kuwa ni mwakilishi wa Serikali.

Hata hivyo wakati, Sitta akisema hayo, baadhi ya waliokuwa mawaziri waliotangaza kujiuzulu pamoja na Lowassa ambao ni Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha, wamo kwenye kamati mbalimbali za Bunge hilo.

Kama hiyo haitoshi, mbali ya hao wabunge wengine kadhaa waliokuwa mawaziri kabla ya mabadiliko ya hivi karibuni na baadaye wakaachwa nje ya Baraza jipya la Mawaziri lililoteuliwa Februari 12 mwaka huu, wamo ndani ya kamati za kudumu za Bunge ambazo leo zinatarajia kuchagua wenyeviti wake.

Baadhi yao na kamati zao kwenye mabano ni Kingunge Ngombale-Mwiru (Kanuni za Bunge), Anthony Diallo (Fedha na Uchumi), Nazir Karamagi, Basil Mramba, Joseph Mungai na Bakari Mwapachu (Viwanda na Biashara).

Wengine ni Dk. Ibrahim Msabaha (Ulinzi na Usalama), Zakia Meghji (Ardhi, Maliasili na Mazingira), Charles Mlingwa (Kilimo, Mifugo na Maji), Daniel Nswanzugwanko (Nishati na Madini), Zabein Mhita na Juma Ngasongwa (Hesabu za Serikali za Mitaa).

Kuwamo kwa wabunge hao, kunaifanya hoja ya Sitta kusema kuwa Lowassa hakupata fursa ya kujaza fomu hizo kuibua maswali.

Hata hivyo habari zinaeleza kwamba, Lowassa mwenyewe pamoja na kuwa na muda wa kutosha kujaza fomu, hakufanya hivyo, huku Spika Sitta ambaye kimsingi anayo mamlaka ya kumteua katika moja ya kamati naye akiamua kuliacha kando jina la waziri mkuu huyo aliyejiuzulu.

Wakati hilo likitokea kwa Lowassa, taarifa nyingine zinaonyesha kuwa tayari kumeibuka mvutano mkubwa wa kimakundi katika uteuzi wa wenyeviti wa kamati hizo.

Kuanza kutumika kwa kanuni mpya za Bunge kifungu cha 111 (10) kinachoainisha kwamba, kamati tatu za Bunge zinatakiwa kutoa wenyeviti wake katika kambi ya upinzani, kumeanza kuleta wasiwasi wa kuibuka kwa mgawanyiko.

Katika hali hiyo, baadhi ya wabunge wa kambi ya upinzani leo wanatarajia kuchuana vikali kuwania nafasi ya uenyekiti wa kamati tatu za Bunge ambazo ni Hesabu za Serikali, Hesabu za Mashirika ya Umma na ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa.

Kamati inayoelezwa kuwa na upinzani mkali kwa upande wa nafasi hiyo ni ile ya Hesabu za Mashirika ya Umma, ambapo Mwadini Jecha na Mwanawetu Zarafi (wote wa CUF), Halima Mdee na Kabwe Zitto (CHADEMA), watachuana.

Habari ambazo Tanzania Daima ilizipata jana jioni zinaeleza kuwa, wakati tayari Zitto alikuwa ameshaanza kuonyesha dalili za kushinda, mwenzake Jecha naye alionekana kutoa upinzani mkali kwake.

Katika Kamati ya Hesabu za Serikali, watakaochuana ni John Cheyo (UDP), Seveline Mwijage na Muhammmad Sanya (CUF) wakati CHADEMA ikiwakilishwa na Mhonga Said.

Aidha, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa inawakilishwa na Ania Chaurembo (CUF), Grace Kiwelu na Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA).

Kuundwa kwa kamati mpya za Bunge kunatokana na mabadiliko ya kanuni, hivyo hata kuwapo kwa waliokuwa mawaziri kwenye baadhi ya kamati hizo kumesababishwa na kuvunjika kwa Baraza la Mawaziri.

http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/3/18/habari2.php
 
Mkuu Babah,

Heshima mbele mkuu, huo wako sio uzalendo, tuko hapa JF kwa ajili ya taifa na sio vyama, Zitto na Dr. Slaaa ni wanachama hai hapa, wao tunawategemea zaidi kwenye kuyatekeleza mawazo kichwa kutoka hapa, sasa wakikataa nafasi influencial kama hizi walizopewa mabadiliko yatakujaje?

Kumbuka hizo nafasi wamepewa Six, ninaamini kwa makusudi ili wamkome nyani, maana sasa baada ya Six kuteswa sana Lowassa ndani ya bunge, sasa haya ni malipo halali maana malipo ni hapa hapa duniani, anyways mkuu wangu punguza kidogo hiyo tone ambayo ni very dividing, sisi ni taifa moja regrdless ya vyama vyetu na itikadi. Tuangalie taifa kwanza, maana Zitto na Slaa wataleta mabadiliko makubwa sana kwenye hizo nafasi, waliyoyafanya wakiwa nje ya hizo kamati sio madogo, sasa iweje wakiwa ndani?

Taifa Mbele, itikadi nyuma.

Ahsante Mkuu.
 
Mh. EL katika utetezi wake siku ile pale Bungeni alisema kuwa ametumia busara zake kumuandikia JK kuwa anajiuzuru U-PM kwa sababu ya kuhusishwa na ufisadi. Sasa sijui kama hizo busara alikuwa nazo siku hiyo tu au vipi kazisahahu Monduli maana angeweza kutumia the same busara kumwambia Spika kuwa kulingana na tuhuma zile asingeweza ku-hold nafasi yoyote katika chombo au kamati ya Bunge hadi hapo tuhuma hizo zitakapota suluhisho ingawa sijui na lini hilo suala litapelekwa Mahakamani. Hata hii vilevile ingewagusa na hao mawaziri wengine waliojiuzuru, nao wangetumia busara zilezile.
Na kama Sam Six katoa nafasi hizo ili kuwapoza hao mafisadi ili alete mshikamano ndani ya chama chao kwa kweli si kwamba Kachemsha bali KATOKOTA. Mashambulizi kwa mafisadi hayarudi nyuma hadi wasafishwe kwenye ngazi zote. JF kaza BUTI, wembe ni uleule hatujali kama ni Mwenyekiti au mjumbe wa kamati ya Bunge. Kama ni fisadi lazima afisadukuliwe.
 
Kwanza kabisa nipende kuwapongeza kwa serikali kuona umuhimu na umakini wenu katika kufanya kazi zenu, hapo kwa hilo watanzania tuko pamoja
Laniki sitakuwa na fadhila kwa watanzania nikikaa kimya kwa hili ambalo limetokea leo katika uchaguzi wa members wa kamati mbali mbali. Nayasema haya kwa sababu haingii akili kufanya kazi na mwizi mkubwa kama Lowassa, karamagi na wengineo wengi tu
Inawezekana wezi wako wengi katika serikali yetu, lakini hatuwajui, hivyo wanaendelea kutesa tu, lakini hata ambao tuwajua tuna sababu ya kufanya nao kazi jamni?

Mapendekezo yangu kwa Zitto na Dk slaah
Kataeni kabisa hao watu kuwa kwenye kamati zenu kama inawezekana, kwa sababu hao ni Mafisadi na watawaharibia kazi zenu
Hao wananuka na wamekulia katika mazingira ya kuiba pesa za walalahoi
Kama ikishindikana nawaomba muachie huo uwenyekiti wa hizo tume teuli, ili kuepuka kufanya kazi na Mafisadi, ili kulinda heshima yenu katika jamii na taifa.
Naomba kutoa pendekezo

Zito kama unatusikia tunakuomba usikilize maoni ya Watanzania. Lowassa na Msabaha wanahusika moja kwa moja na ufisadi wa Richmond hivyo siyo tu hawastahili kuwemo kwenye hizo kamati, pia hawastahili kuendelea kuwa wabunge. Najua bungeni wabunge wa upinzani mko wachache, lakini ombeni hawa waondolowe kwenye hizo kamati ama nyinyi msikubali kuwemo kwenye hizo kamati. Watanzania tulio wengi tuko nyuma yenu, maana sasa huu ni upumbavu wa hali ya juu! Juzi juzi tu wote hawa walikuwa wanastahili kufukuzwa kazi, lakini JK kwa kuwaogopa akawapa mwanya wa kujiuzulu, leo tena wanapitishwa mlango wa uani na kupewa nafasi kwenye kamati za Bunge! Hivi CCM hawana Wabunge wengine wanaoweza kuingizwa kwenye kamati hizo!? :confused:
 
1. Heshima kwa Spika kwa kuwapa kazi nzito mashujaa wetu wa taifa Zitto, Dr. Slaa, na Mama Malecela, nahisi bunge lijalo litakuwa na moto wa kuotea mbali.

2. Wakuu Bubu, Bob, na Mazee Geeque, mmesema yote hakuna cha kuongeza, it is pathetic na haielezeki ila only in Tanzania,

However, ninajua kwa taratibu za bunge, ex-PM, huomba in personal kwa Spika nafasi kweye kamati anayotaka, meaning kwamba hapa Lowassa ameomba kuwemo kwenye kamati ya wizara ya rafiki yake wa damu, Nchimbi, je anataka nini huko?


Kazi hizo hawajapewa na spika, wamegombea. Na hajashinda kwa hiyari ya wabunge wa SISIEMU, kanuni mpya za bunge zimeelekeza wenyeviti wa kamati hizo lazima wawe wapinzani

Asha
 
Zito kama unatusikia tunakuomba usikilize maoni ya Watanzania. Lowassa na Msabaha wanahusika moja kwa moja na ufisadi wa Richmond hivyo siyo tu hawastahili kuwemo kwenye hizo kamati, pia hawastahili kuendelea kuwa wabunge. Najua bungeni wabunge wa upinzani mko wachache, lakini ombeni hawa waondolowe kwenye hizo kamati ama nyinyi msikubali kuwemo kwenye hizo kamati. Watanzania tulio wengi tuko nyuma yenu, maana sasa huu ni upumbavu wa hali ya juu! Juzi juzi tu wote hawa walikuwa wanastahili kufukuzwa kazi, lakini JK kwa kuwaogopa akawapa mwanya wa kujiuzulu, leo tena wanapitishwa mlango wa uani na kupewa nafasi kwenye kamati za Bunge! Hivi CCM hawana Wabunge wengine wanaoweza kuingizwa kwenye kamati hizo!? :confused:

Kila mbunge lazima awepo kwenye kamati si kwa hiyari yake wala matakwa ya spika. Ni lazima ya kikanuni. Mbunge hawezi kuondolewa na Zitto, anaondolewa kwa kufa, kujiuzulu, kupoteza mahakamani ama kufukuzwa uanachama wa chama chake. Kwa hiyo, elekeza nguvu zako kwa halmashauri kuu ya CCM iliyojaa mafisadi itakayokutana Dodoma iwafukuze uanachama mafisadi wenzao

Asha
 
Hii ndo Danganyika bwana,watu tuliowatuumu ndo twawakabidhi kamati.

Any labda ndo strategy iyo"mdokozi mkabizi mali zako"
 
hii ni aibu ya hali ya juu. kwanza serikali ilitakiwa kuwasimamisha uwajibikaji wa ndani ya kamati kwa wabunge ambao wamejihusishwa na mambo ya kifisadi mpaka majina yao yatakaposafishwa kisheria.
na huyu Lowassa kwa sheria za tz hafai kuitwa Waziri mkuu mstaafu wala waziri mkuu wa zamani, kwa vile hajatumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka mitano.
aidha kisheria, bwana Lowassa hatakiwi kulipwa marupurupu (allowances) za mawaziri wakuu wastaafu.
sasa kumpembejea na kumuenga enga lowassa ni uvunjaji wa kanuni za sheria za tanzania.
 
Karamagi ndani, Lowassa Ndani, Msabaha ndani, kweli tutafika? Ni lini sheria zetu zitalenga katika kumletea Mtanzania Maendeleo? Kama kuna kipengele kama hiki kwa nini kisifutwe? Na je ina maana mapendekezo ya bunge ya kuchukuliwa watu hatua yameisha wekwa kapuni?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom