Opinion: CCM Waoga Kaa Kunguru!. Wanamuogopa RA kama Mungu Mtu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,543
Wanabodi,
Ule msemo wa " Kunguru mwoga, hukimbiza bawa lake!" leo umeendelea kwa Chama Cha Mapinduzi, kumuopa kada wake RA kana kwamba ni mungu mtu, hivyo sasa kinamtishia nyau kumpeleka mahakamani!.

Uoga huo umetangazwa rasmi na Katibu Uenezi, Nape Mnauye kwa waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa TBC-1 news za saa 2:00, Nape ameonekana amelishika gazeti la Mtanzania na kutishia nyau kuwa watalifikisha mahakamani kwa madai ya kuvujisha siri za vikao vya CC kwenye gazeti hilo!.

Kutendo hicho ni ishara dhahiri ya uoga kama kunguru dhidi ya RA ambaye ni kada wao, wanamjua ndie mmiliki wa gazeti hilo, wanaogopa kumkabili na sasa kujidai kutaka kuitumia mahakama kumwajibisha!.

Nadhani CCM inawanasheria wazuri tuu ambao wangeishauri CCM against hiyo wastage of time kufungua useless case ambayo itakuwa thrown out on the first hearing!.

Nadhani CCM bado iko kwenye ile njozi ya "chama dola" hivyo inajiaminisha documents za vikao vyao ni state secrets hivyo mahakama itawalazimisha Mtanzania wafanye 'disclosure' ya source wao ili afungwe kwa possessio ya ' state secrets'!.

Ukiona chama kinakimbilia mahakamani kutafuta mchawi miongoni mwa makada wake, ujue hizo ni dalili za mfa maji haachi kutapata sasa kinataka hata kudandia chelewa ili kujiokoa!.

All the best CCM kwenye kesi dhidi ya kada wake!.

Wasalaam.

Pasco (wa jf)
 
Uoga ni sifa ya kufikiria sana kabla ya kufanya maamuzi ili kutofanya mambo kwa papara. Kwa hiyo asiwasahangae watu waoga dungu yangu
 
Wanabodi,
Ule msemo wa " Kunguru mwoga, hukimbiza bawa lake!" leo umeendelea kwa Chama Cha Mapinduzi, kumuopa kada wake RA kana kwamba ni mungu mtu, hivyo sasa kinamtishia nyau kumpeleka mahakamani!.
Mkuu wewe ni miongoni mwa mwanahabari wetu nguli Bongo,mbona habari ipo juu juu sana?
 
Mfadhiri akianza kuingilia uhuru wa nyumba yako basi kinacho fuata ana kucameron kwa njaa zako za kijinga ndo ccm hao wameshikwa pabaya.
 
sasa ulitaka wafanyaje?
watumie nguvu ya dola kuvifungia vyombo hivyo?
au vipi?
 
Wanabodi,
Ule msemo wa " Kunguru mwoga, hukimbiza bawa lake!" leo umeendelea kwa Chama Cha Mapinduzi, kumuopa kada wake RA kana kwamba ni mungu mtu, hivyo sasa kinamtishia nyau kumpeleka mahakamani!.

Pasco, nimemuona Nape TBC1 8pm news bulletin. Mambo ya ajabu kusema la ukweli. Nape analalamika kuwa kuna gazeti (nadhani ni Mtanzania) limeandika habari kwa kutumia nyaraka ambazo sio sahihi. Lakini alipoulizwa kama CCM walijadili yaliyoandikwa kwenye gazeti Nape anasema baadhi ya mambo ni kweli walijadili ila mengine yalibadilika. Inavyoelekea ni kwamba gazeti la Mtanzania lilipata waraka ambao ulikuwa kwenye 'draft' stage, hivyo final version ilikuwa na baadhi ya vitu tofauti na draft. Na hiki ndio kiini cha Nape kukutana na waandishi wa habari.

Mimi nilidhani badala ya Nape kutangaza kuwa CCM inakusudia kuchukua hatua za kisheria juu ya habari hiyo nilifikiri wangetoa ufafanuzi wa kile wanachoona sio sahihi. Huu ndio ustaarab na sio kutishia vyombo vya habari. Pia CCM wanatakiwa wawe makini zaidi. Ndani ya chama mambo sio shwari na sasa wanataka kuanzisha ugomvi na vyombo vya habari? CCM ya Nape hawachoki na mzigo wa migogoro kila kukicha? Mtanzania ni lina uhusiano na Rostam, baada ya kuzunguka mikoani akisamaka watu wanaosemekana ni mafisadi Nape na wenzake sasa wanamfuata Rostam Azizi kwa sababu wanaona ni size yake au? Kila la kheri!
 
CCM ipo kama alivyo mwenyekiti wao
a weak chairman is the source of the weak party......
 
Hivi anajua gazeti hilo la tajiri anae fadhiri chama? Mwache aendelee anajitafutia njaa.
 
Mkuu wewe ni miongoni mwa mwanahabari wetu nguli Bongo,mbona habari ipo juu juu sana?
Mtazamo, kwanza asante kwa kunidhania mimi ni miongoni mwa wanahabari nguli, binafsi sijihesabu kwenye kundi hilo kwa sababu ni siku nyingi nimeachana na kalamu.

Hii sio habari ni opinion article. Nikileta habari humu huanza kwa News Alert!.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom