Opinio Poll: Je, unaunga mkono mgomo wa madaktari?

Je, unaunga mkono mgomo wa madaktari?

  • Total voters
    174
baada ya kusema NDIYO kwa kweli wananchi tujue, mgomo ni kwa faida yetu. Nchi imechelewa, madokta wangeamua wasingefanya kazi nchini, wanaelewa, 1. mwalimu hafundish bila chaki,kalamu 2. mhandisi hajengi bila simenti 3. hakimu haamui bila ushahidi 4. mlinzi halindi bila silaha 5. dereva haendeshi bila bima na taa 6. polisi bila dola? 7. mtangazaji bila kuwa on air! 8. duka bila bidhaa, duka gani? 9. utachezaje bila ngoma,mpigaji? 10. mining bila vifaa? 11. mkulima bila mbegu,zana? 12. mchumi bila data 13. mhasibu bila fedha zenyewe 14. mwanamipango bila mipango yenyewe mwisho Watanzania tumechelewa sana.
 
Madaktari wamegoma for a 'cause". Je unawaunga mkono? Toa maoni yako tafadhali

Naunga mkono, madai yao ni ya msingi......mbali na kuwa na mapato duni kutokana na udaktari mazingira yao ya kazi ni magumu mno, kuna taarifa kuwa hata hiyo huduma ambayo wamekuwa wanatoa inatokana na ku' improvise " vifaa kadhaa ili vitumike hata mahali pasipo pake. kuna zana na vifaa tiba vya msingi ambavyo havipo mahospitalin ambavyo ni lazima kwa kurahisisha kazi zao. Nimesikia kuna wakati huwa wanatoa hata senti zao kidogo zilizopo mifukoni ili kuwasadia wagonjwa kununulia dawa ambazo kwa muda mrefu zimekuwa adimu kwenye hospitali za serikali.
Naunga mkono hoja!
 
Naunga mkono madaktari.

Wananchi tumekuwa kanunguyeye kwq kutokuibana serikali kutuhakikishia matibabu mazuri huku ikitumia pesa zetu kwa anasa za kipumbavu kama posho za kukaa, posho za kulala, posho za ufunguzi wa disco, washa, semina na utalii, ununuzi wa magari ya anasa, vx, v8, n.k. Wake up Tanzanians, ni nani kawaroga?
 
well, the truth is 3.5 ni pesa ambao wanastahili, lakini la msingi zaidi ni hali ya hospital zetu. Ni hatari kama hamna hospital ya serikali nchini saiv ambayo ina machine ya citi scan ( this is very bad shame on the government), bei ya citi scan ni kama vx moja tu!! How stupid is that. Madai ya madaktari kutaka xray machine kila hospital ya wilaya mzee, iyo iko very reasonable. Kuna vitu vingine watanzania inatakiwa tuwe makini navyo, tusibabaike tutafute ukweli kwanza!!

3,500,000/= sio mshahara halisi,kodi yake ni 30%+ 103,000, nssf 10%+ michango mbalimbali ya kisheria, anachobaki nacho daktari ni kama 1,497,000 hivi. Hizi ni pesa nyingi? Tatatizo ni kuwa urais wa tanzania unahitaji mtu mwenye uwezo wa kuvaa kiatu namba 10,lakini rais kikwete(kwa bahati mbaya sana) uwezo wake ni wa kuvaa kiatu namba 8. Miguu yake inapwaya
 
Toka mgomo huu ulipoanza, nimekua nikijiuliza maswali mengi kadiri siku ziendavyo. Lazima nikiri kwamba na mimi nilitumbukia katika mtego wa kulaumu upande mmoja wapo kabla ya kujiuliza vizuri... Ama baada ya kutafakari kwa kina, nikagundua kwamba kwa vyovyote vila itakavokua, tunaoathirika ni sisi wananchi, bila kujali tunaunga mkono madaktari au serikali.

Nilianza kujiuliza hivi: Hawa wanasiasa wanaotupiana mpira, mara CHADEMA, mara CCM, bila kujali vyama vyao, wanatibiwa wapi kwa kawaida? Hawa kwani hawana madaktari maalum ambao wanawalipa binafsi? Hivyo basi, huyu kiongozi anayesema fukuza, hakutani na daktari wake binafsi ambaye huenda anatugomea sisi wananchi? Mimi mwananchi wa kawaida ambaye sijuani na daktari na wala sina pesa, nani atanitibia?

Je, nikisema serikali ifukuze madaktari wote, nani atanitibia? Nikisema pia wagome, kwani nikienda hospitali wataniuliza kama nawaunga mkono ili wanitibie? Au ndio yale ya "naunga mkono mgomo", lakini kwa sababu mimi sina jamaa daktari, au sio daktari, basi sina wa kunitibia. Lakini wao wanasema wananisaidia, ilihali wananiacha nateseka na wao wakitibia ndugu na marafiki zao!

Baada ya kuangalia hali yangu na hao viongozi wa siasa, bila kujali vyama vyao, nikajiuliza maswali mengine: Je, miongoni mwa madaktari wanaogoma, hawana wateja wao binafsi ambao ndio hao hao mawaziri wanaowatuhumu kufisidi sekta ya afya? Je, mawaziri hawa wakienda katika clinics zao binafsi wanawagomea? Je, ni kweli kwamba madaktari wote wanaoshiriki mgomo, hakuna hata mmoja ambaye aliwahi kwa njia moja au nyingine kushiriki katika kufisidi sekta ya afya, iwe kwa kuiba panadol au vifaa vya malaki au hata mamilioni? Je, na wao wanahaki ya kusema kwamba wanagoma kwa sababu ya ukosefu wa vifaa?

Sikuishia hapo tu... nikajiuiza tena: vipi sisi wenyewe, ambao tunashangiia au kushabikia ama serikali kufukuza madaktari, au madaktari kugoma: Hakuna miongoni mwetu walioshiriki kuziibia hospitali zetu? Je, ni haki, kwa mwananchi mwenzetu, ambaye naye ameshiriki kufisidi hospitali, kunyoosha kidole, au kushabikia akisema serikali ifukuze, au madaktari wagome, wakati huyo naye ni sehemu ya tatizo?

Bado nikajiuliza maswali zaidi: Hivi tunaposikia serikali na madaktari wameshindwa kuafikiana, tunayachukua hivyo hivyo tu, au tunauliza kwa kina ni kwa nini wameshindwa? Tunaposikia serikali au madaktari wanasema wako tayari kwa majadiliano, tunawauliza ni hatua gani wanazichukua kwa ajili ya majadiliano, wakati upande mmoja unaendelea kufukuza na mwingine unaendelea kugoma? Tunapozikosoa taarifa zao, ni kwa sababu tumeamua kuchukua upande mmoja, au tunajua madhara ya mgomo huo kwetu sisi?

Maswali haya mengi yamenileta katika swai moja muhimu... Sisi wananchi, tusio wanasiasa, wala tusio madaktari au walau na ujamaa na daktari - tumekua tunatoa maoni yenye kuleta suluhu, au yenye kuchochea mgogoro? (bila kujali uko upande gani)

Watanzania wenzangu, katika hili, tunahusika wote. Kwa wale wanaosema madaktari wasigome, wasiishie tu hapo, watafakari sababu za matatizo ya sekta ya afya. Na kwa wale wanaosema wagome, wajiulize swai moja tu: Je, sababu kwamba ukosefu wa huduma bora kwa miaka kadhaa umesha sababisha vifo fingi, ni kisingizio haswa cha mgomo ambao na wenyewe pia unasababisha vifo na mateso?

Mimi na wewe tunafanya nini ili kurudishiwa huduma ya afya? Tuendelee kupiga siasa? au tutoe maoni ya suluhu?
 
Asante mkuu.
You can always tell a true Tanzanian at heart from paid politicl parrots.
Wewe una uchungu na nchi hii na watu wake!
 
Siungi mkono
1. Mahakama ilizuia, walipaswa kuheshimu au wakate rufaa
2. Kuboresha mazingira ya kazi ni jukumu la mwajiri, siyo mwajiriwa
3. Mshahara wa 3.5m kama kima cha chini kitaleta pengo kubwa kati ya madaktari na watumishi wengine.
Mengine nitaongeza baadaye

Polisi inaonesha ulisoma darasa moja na Dr. Photogenic a.k.a baba nanihii! Hamna tofauti namna mnavyochukulia mambo na hata reasoning yenu inafanana!
 
Naunga mkono,make sijaona kazi inayomfanya mbunge kupewa ela yote ile kuliko mtu mwenye taaluma
 
naunga mkono na kuwashauri na jamaa wa vyumba vya kuhifadhia maiti nao waungane na madaktari katika harakati hizi mpaka watskspo wataja wanaomiliki mapesa kule uswis na wakimtaja kagoda ni nani?
 
Maoni ya watanzania walio wengi wanaunga mkono mgomo, huo ndio ukweli
 
mimi naunga mkono hoja zao za kutaka huduma ziboreshwe lakini siungi mkono mgomo kwa sababu innocent lives zinapotea bila sababu. Sasa hivi tu hawa madaktari na wasaidizi wao wana viburi wanatukana na kujibu vibaya wagonjwa sasa wakianza kulipwa million tatu si watakua wanatemea mate hao wagonjwa?
 
Kwanza kabisa siungi mkono hata kidogo:

Kuunga mkono ni kubariki watanzania wanyonge kufa bila sababu ya msingi hata kidogo. Hawa watanzania wanyonge wanakamuliwa kodi zao madaktari wanalipwa lakini leo wanakataa kuwahudumia wagonjwa wa kichocho (maji machafu), malaria (mbu kibao), minyoo, safura, kuhara na kuhara damu! Hawa siyo wale walioshiba yaani watoa maamuzi ambao wakaiugua ttu wanaenda Muhimbili kupata kibali cha kwenda ng'ambo kutibiwa! Leo badala ya kushughulika na hawa Madaktari wetu wanaamua kuwakomoa watu ambao wanakufa kwa kuhara tu!

Madaktari kataeni kuwapa hao watoa maamuzi vibali vya kwenda kutibiwa nje kwa pesa za kigeni. Msiwaumize wanyonge wasiokuwa na kitu.
 
Naunga mkono mgomo wa Madaktari ili taifa liweze kufanya marekebisho makubwa kwenye mfumo wa huduma za afya ili kuepuka aibu kwenye hospitali zetu na vituo vya afya kukosa vipimo muhimu na vya msingi katika karne hii kama vile X-Ray, Ultra Sound, CT Scan, ECG machines. Ili vifaa tiba vibovu ambavyo havitengenezwi kwa zaidi ya mwaka viweze kutengenezwa haraka vinapoharibika
 
siwezi kuunga mkono...kwani nchi hii sio madaktari pekeee!!!!!!!!!!

Umeongea vyema ila kabla hujaendelea tunaomba level yako ya elimu na course uliyosoma ikiwezekana na chuo kabisa na ni intake ya mwaka gani? then i will tell you something.
 
Back
Top Bottom