Ni mpuuzi na mtu asiye na uzalendo pekee atampinga Mkuu wa Mkoa katika vita hii, Ila ni werevu na wenye akili tuu watapinga mbinu/approach iliyotumika, kwani ikiwa tunaamini tutazingatia UTAWALA WA SHERIA, basi ni kuwa vita hii itashia mahakamani na kama itaishia mahakamani Criminal Procedure Act Cap 20 RE 2002, Evidence Act cap 6 Re 2002, Haki za binadamu zilizomo katika katiba, na Police General Orders zifuatwe ili kusinusuru kesi hizo zikiwa mahakamani, ukiangalia vita hii inavyoendeshwa hauhitaji kusoma sheria kujua kinachofanyika hapa kuwa kimekuwa kikiendeshwa kwa utashi wa kisiasa zaidi kuliko sheria, kuendesha vita hii kisiasa kuliko kisheria zaidi kunadidimisha na kufifisha zaidi vita hii.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.