Operesheni Ya Kuondoa Wahamiaji Haramu Maporini Mpakani Karagwe imesitishwa?

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,518
8,584
Wimbi la wahamiaji haramu ambao huingia na kundi kubwa la mifugo wakitokea nchi jirani limerudi upya tena safari hii kwa kasi na kujiamini na kiburi .Wahamiaji hawa itakumbukwa walifurushwa na aliyekuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu Jakaya Mrisho Kikwete .

Wiki iliyopita Serikali ya mkoa wa Kagera inayoongozwa na Maj Gen Kijuu ilitangaza kupitia mkuu wake wa wilaya kuingia porini kuwasaka wahamiaji hawa hatari wenye silaha kali na nzito,matokeo yalikuwa mazuri na walikuta makundi hayo kama taarifa za intelligence zilivoonyesha .

Serikali ya mkoa ilitoa onyo kuwa kabla ya mwisho wa mwezi wataanzisha operesheni kubwa ya kijeshi kuusafisha mapori ya misitu hii ya mipakani..Moja ya madhara ya wahamiaji hawa wenye malengo yaliyo nyuma ya pazia ni mpango haramu wa EXPANSIONISM ambao unajulikana wazi kwenye anga za kijasusi
Wenzetu hawa wanafadhili wananchi ...wengi wao wakiwa sio wananachi wa kawaida bali askari wao wastaafu na wapelelezi kuhamia maeneo ya mipakani ya nchi hasa Tanzania na Congo ...wakishafika huko hujipenyeza katika mpango huu haramu wa kujipanua ....wakiwa na lengo la kuhakikisha miaka 10 na kuendelea wakikaa bila kusumbuliwa wanakuwa wameshajijengea uhalali, na katika kipindi hicho wanakuwa wanapenyeza silaha ...na ikifikia kuwaondoa itakuwa ni kama vita ....hii ndio pia iliyogundulika wakati wa operesheni kimbunga ....kuna maeneo Mapambano ya kuwahamisha wahamiaji yaliambatano na wao kujibu mapigo kwa kutumia silaha nzito za kubeba begani ..RPG, LMG.. na nyingine ..

KATIKA Hali inayotia shaka inasadikika kuwa mpango mzuri wa Maj Gen Kijuu na wenzake ambao ni ma DC Aliotoka nao jeshini tayari umehujumiwa kwa amri kutoka juu .
Tunaomba wanaoipenda nchi hii wawe macho na wafuatilie kwa makini haya yanayoendelea ...tunahitaji katiba mpya itakavyovipa vyombo vyetu vya ujasuri na jeshi uwezo wa kudhibiti hali kwa usalama wa taifa letu ...ili hata tukitawaliwa na "mgeni" asiwe na uwezo wa kuvuruga safu ya vyombo vyetu kwa kupenyeza watu wanaoweza kuwa tishio kwa nchi ..ingekuwa hawa wateule wanapita bungeni basi sio rahisi mtu kubadili safu namna hii ambayo inaweza kudaka taarifa za operesheni na kuzifikisha kwa adui ambaye ana uwezo wa kuwasiliana na walio juu kuzuia

Hili sio suala dogo!!
 
Hii sehemu ya andiko lako imenichekesha sana!

...tunahitaji katiba mpya itakavyovipa vyombo vyetu vya ujasuri na jeshi uwezo wa kudhibiti hali kwa usalama wa taifa letu ...ili hata tukitawaliwa na "mgeni" asiwe na uwezo wa kuvuruga safu ya vyombo vyetu kwa kupenyeza watu wanaoweza kuwa tishio kwa nchi.

Huyo ''mgeni'' ni nani na anapatikana vipi kwenye katiba mpya unayoipigia chapuo?

Hii katiba itakayoruhusu ''mgeni'' kuwa Rais wa Tanzania itakuwa ni katiba ya hovyo sana!

Kinachofurahisha zaidi, andiko lako limejikita kwenye hisia na majungu tu.
 
Huko "juu" amri inakotoka ndiko kwenye tatizo! Mifano iko mingi tu:
1. Unakumbuka wavuvi wetu waliuawa na askari wa Rwanda mpaka Mwigulu akafanya ziara na kuahidi kuongea na wizara ya nje ili tupate tamko rasmi la serikali ya Rwanda? Hilo likafa kimyakimya, maisha ya watanzania hawa yakapotea hivi hivi. :: Askari Wa Rwanda Watuhumiwa Kuendesha Mauaji Ya Wavuvi Wa Kitanzania Mto Kagera
2. Hujuma dhidi ya operesheni dhidi ya wahamiaji haramu sio jipya tayari thread zipo humu: Asimamishwa kazi kwa kukamata Wanyarwanda porini
3. Rwanda ndio iliyotushauri tununue ndege sio mainjinia wa ATC wala bunge!, Rwanda ndio tunaiga usafi wa jumamosi na mambo mengine ya ajabu ajabu kama kutoleana bastola bila sababu.
4. Eti wataalamu wa IT Tanzania hawapo wako Rwanda, wakati sisi tuko huku miaka kibao tunafanya IT hio hio na hao wanyarwanda tunawafundisha sisi! Mtu anataka awakabidhi mifumo ya bandari!
5. waliopinga mbinu za Rwanda kututawala kupitia bunge la EAC wanafukuzwa kwa kauli za "huyu sitaki kumsikia....sitaki mjadala" !!!

Ninaanza kuwa na wasiwasi na huyu aliye juu.....
 
mtoa mada yuko sahihi, hata trump leo hii anadhibitiwa na katiba ya marekani. Vinginevyo hali ingekuwa mbaya. Mwenendo wa mtu humuweka wazi kama ni mgeni au mwenyeji. haiwezekani wewe uwe baba wa nyumba wa A lakini kila siku unahujumu nyumba yako kwa maslahi ya nyumba B!
Na kwa taarifa yako tumeshawahi kuwa na "wageni" katika ngazi mbali mbali kuanzia uenyektii wa mitaa, ukuu wa mikoa, mpaka ubalozi. Na wote hao walipata vyeo hivyo kwa katiba hii hii inayokataza. Sio ajabu kuwa na "mgeni" katika ngazi ya juu kuliko zote.
 
Mi nilijua tu kuwa hiyo operation ni kwa ajiri ya kiondoa wasukuma na watanzania wenzetu. Na si ajabu wanyarwanda walioko kule waliriport kwa rais wao nae kumpigia simu mkuu
 
Mbona MI ya Tanzania inasifika kwa weredi wa Hali ya juu eneo la maziwa makuu
. Naamini wao wanajua zaidi yetu, hili tu linafanya kuamini hisia zako ni batili.

Binafsi sikupendezwa juzi mkuu wa wilaya ngara kutumia magari kwenye pori ambalo halina barabara kukamata wahamiaji haramu. Kwa nini tusifanye kwa kutumia chopper kama wale wasukuma wafugaji bonde la mto kilombero/selou walivyofurushwa.
Hao wahamiaji haramu na wafugaji haramu wasichekewe...
 
Hii sehemu ya andiko lako imenichekesha sana!

...tunahitaji katiba mpya itakavyovipa vyombo vyetu vya ujasuri na jeshi uwezo wa kudhibiti hali kwa usalama wa taifa letu ...ili hata tukitawaliwa na "mgeni" asiwe na uwezo wa kuvuruga safu ya vyombo vyetu kwa kupenyeza watu wanaoweza kuwa tishio kwa nchi.

Huyo ''mgeni'' ni nani na anapatikana vipi kwenye katiba mpya unayoipigia chapuo?

Hii katiba itakayoruhusu ''mgeni'' kuwa Rais wa Tanzania itakuwa ni katiba ya hovyo sana!

Kinachofurahisha zaidi, andiko lako limejikita kwenye hisia na majungu tu.
Wageni wengi tu wapo katika serikali ya nchi hii, tena hadi kwenye vyombo ambavyo wageni hawaruhusiwi kuhudumu.
 
Ni muhimu kwa vyombo vinavyohusika na DEFENCE, SECURITY NA INTELLIGENCE kufanya kazi dhidi ya hii threat kutoka Rwanda na Mtussi ni jamii ambayo wanaamini wameumbwa kutawala wabantu baada ya wazungu kuondoka na ktk vitu ambayo Serikali ya Tanganyika wamekosea sana ni kumfanya Rwanda kuwa Mdau wetu badala ya Jirani yetu
 
Huko "juu" amri inakotoka ndiko kwenye tatizo! Mifano iko mingi tu:
1. Unakumbuka wavuvi wetu waliuawa na askari wa Rwanda mpaka Mwigulu akafanya ziara na kuahidi kuongea na wizara ya nje ili tupate tamko rasmi la serikali ya Rwanda? Hilo likafa kimyakimya, maisha ya watanzania hawa yakapotea hivi hivi. :: Askari Wa Rwanda Watuhumiwa Kuendesha Mauaji Ya Wavuvi Wa Kitanzania Mto Kagera
2. Hujuma dhidi ya operesheni dhidi ya wahamiaji haramu sio jipya tayari thread zipo humu: Asimamishwa kazi kwa kukamata Wanyarwanda porini
3. Rwanda ndio iliyotushauri tununue ndege sio mainjinia wa ATC wala bunge!, Rwanda ndio tunaiga usafi wa jumamosi na mambo mengine ya ajabu ajabu kama kutoleana bastola bila sababu.
4. Eti wataalamu wa IT Tanzania hawapo wako Rwanda, wakati sisi tuko huku miaka kibao tunafanya IT hio hio na hao wanyarwanda tunawafundisha sisi! Mtu anataka awakabidhi mifumo ya bandari!
5. waliopinga mbinu za Rwanda kututawala kupitia bunge la EAC wanafukuzwa kwa kauli za "huyu sitaki kumsikia....sitaki mjadala" !!!

Ninaanza kuwa na wasiwasi na huyu aliye juu.....
Uko sahihi. Hima Empire ishatimia
 
Mkuu wa wilaya alikosea sana, inakuwaje unafanya operation bila ya kuwa na ramani kamili ya kuanzia na kutokea, mbona wakati vita ya uganda walikuwa wanatumia ramani, anafanya operation kuwaondoa wahamiaji haramu ambao wana mifugo mingi wakati wilayani kwake hakuna kiwanda cha kusindika nyama au maziwa. angewetengea maeneo na kuwapatia uraia ili mifugo yao izidishe pato la taifa
 
Umechafua thread nzuri kabisa kwa kuleta mizaha kwenye suala nyeti.
 
Umechafua thread nzuri kabisa kwa kuleta mizaha kwenye suala nyeti.
Mzaha uko wapi, au lengo ni uchochezi kwa watu wamchukie kiongozi mkuu,utaweza vipi kumfukuza mwenye mali na wewe huna mali
 
Kwa mtiririko wa mambo unavyoenda kuna haja ya kuchunguza uraia wa pale juu. Wananchi tunaanza kuwa na wasiwasi kwa haya makatazo kuanzia kuuawa kwa wavuvi wetu mpaka kusitishwa kwa hii operesheni.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom