Operesheni Vua Gamba Vaa Gwanda (M4C) yazoa Tarime, Newala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Operesheni Vua Gamba Vaa Gwanda (M4C) yazoa Tarime, Newala

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hiraay, Aug 15, 2012.

 1. H

  Hiraay Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Operesheni maalumu ya 'Vua Gamba Vaa Gwanda inayoongozwa na CHADEMA imetikisa wilaya ya Tarime mkoani Mara, baada ya zaidi ya wanachama 3,500 wakiwamo viongozi wa CCM kujiunga na Chadema.
  Wanachama hao wakiwemo viongozi wa CCM, wamejiunga rasmi na Chadema mwishoni mwa wiki, wakati wa mkutano wa hadhara wa chama hicho, uliofanyika mjini Sirari kisha kuhutubiwa na mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa wa chama hicho John Heche.

  Miongoni mwa viongozi wa CCM waliorudisha kadi kisha kukabidhiwa za Chadema mkutanoni hapo, ni pamoja na mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Sirari, masha Vicent na mkewe Veronika Masha.

  Wakati huo huo, M4C limeendelea kukichanganya Chama cha Mapinduzi wilayani Newala, na kufanikiwa kuzoa wanachama 276. Katibu wa Chadema, wilaya ya Newala, katika taarifa yake iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, alisema kuwa wananchi mbalimbali wengi wao wakitokea CCM, walifanikiwa kujiunga na chama hicho baada ya kufanya mikutano ya ukombozi kwenye kata tano na vijiji vyake vipatavyo 32.

  Aliwataja baadhi ya vigogo ndani ya vijiji waliojivua gamba kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Azimio, na Mwenyekiti wa Kijiji cha Samora, aliyefahamika kwa jina la Mzee Mpoto.

  Source: Tanzania Daima la Jumatano 15/08/2012
   
 2. M

  Magesi JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  M4c twanga kote kote mpaka magamba wakimbie nchi
   
 3. C

  Concrete JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Speed yenu inatisha mbaya. Ile operation yetu iliyokuwa inaongozwa na Nape sijui imezimikia wapi?

  Any way hii sio issue sana kwetu kwani mlichovuna ni tone tu kutoka kwenye mtaji wetu mkubwa.
   
 4. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hakuna kulala mpaka kieleweke makamanda.

  Heche hakikisha unafika Nyamongo uwavue magamba na kuwavisha magwanda, usisahau kuibua madudu yaliyopo Mgodoni kama nilivyomsikia cku moja Tundu akisema hawajalipwa fidia baada ya kunyang'anywa aridhi yao.
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,198
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  CCM waje na propaganda nyingine tena ya CHADEMA wanawapa pesa wanao jiunga nao.
   
 6. j

  jiwe gumu Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kazi nzuri ya CDM.Hakuna kulala mpaka kieleweke.Sasa sijui Nape atajitetea nini.Maana huyu bwana kwa propaganda ndo mwenyewe.CCM wamebanwa kila pembe..bungeni,vijijini,mijini,kwenye umaskini,elimu,afya nk.Nape kazi unayo.Kipimo cha mambo yote 2014 wakati wa uchaguzi wa serikali za vitongoji,mitaa/vijiji.Matokeo yake yatatupa mwanga mkubwa wa 2015.
   
 7. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  taarifa zenyewe TANZANIA DAIMA? gazeti la mbowe unavyofikiri habari zake zitakuwa za kuiponda chadema au kuifagilia?
   
 8. Lawrence Luanda

  Lawrence Luanda JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  M4C kanyaga twende
   
 9. T

  Tewe JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Nguvu ya umma haijawahi kushindwa
   
 10. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  ulitaka aandikwe na gazeti la uhuru au gazeti la fahamu sio
   
 11. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  bwana heche tunakukubali sana ila kuwa makini kuna watu huko mikoani si wazuri wanatafuta viongozi wa chadema kwa udi na uvumba hata kuwachafua na ccm sasa ina mawakala hata ndani ya chadema kuweni makini
   
 12. commited

  commited JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Jana sijakuona kabisa katika ule uzi wa Tundu Lissu kuanika uozo wa majaji.Pole zako, kila chenye mwanzo kina mwisho.
   
 13. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ahhhhh sasa nimeelewa kwanini CCM wameanza kumzonga huyo dogo. Dogo wakomoli hao kisawasawa.
   
 14. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Nape mbona ccm hamji kuhamisisha hapa shinyanga????? ccm tunawamiss sana maana mlizoea kila kiongozi wa juu enzi zenu alitaka kuja ziara shy na mwz, siku hizi mmenyuti, duuuuuuuuuuuuuuuuuuu kazi kweli
   
 15. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  mwanzo mwisho
   
 17. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,696
  Trophy Points: 280
  go chadema go.....
   
 18. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #18
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,695
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Punguza ukali wa maneno ccm nao ni watu
   
Loading...