Operesheni Tokomeza: Serikali kuwafukuza mawaziri wanne kazi haitoshi…!

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuwaachisha kazi mawaziri wanne Ijumaa, juma lililopita, umemsaidia kuiokoa serikali yake dhidi ya kupigiwa kura na wabunge ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu wake.

Kama asingechukua hatua hiyo, Rais angekabiliwa na tatizo la au kuvunja serikali yake au yeye mwenyewe kupigiwa kura hiyo na hivyo kulipeleka taifa katika uchaguzi mkuu wa kuchagua serikali nyingine.

Mawaziri ambao Rais alitengua kuendelea kusimamia wizara zao ni aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, bwana David Mathayo, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, bwana Shamsi Vuai Nahodha, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, bwana Emmanuel Nchimbi na aliyekuwa Waziri wa Mali asili na Utalii, Balozi Hamisi Kagasheki.

Hata hivyo bwana Kagasheki ambaye ni mwanadiplomasia kwa taaluma, anaelekea ‘alitonywa' na Rais kuwa ataondolewa hivyo akatumia mahusiano yake hayo ya karibu na Rais kutangaza kujiuzulu kwake bungeni kabla Rais hajatangaza uamuzi wake wa kuwaondoa mawaziri wengine watatu Ijumaa hiyo.

Pengine jambo la kusikitisha ni utetezi uliofanywa bungeni na aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, bwana Mathayo ambaye alidiriki kudai kuwa anaonewa!

Huyu ni Waziri ambaye alipewa maagizo tisa na rais mwaka 2006, lakini mpaka alipoachishwa kazi Ijumaa alikuwa hajatekeleza hata agizo moja!

Kwa kujitetea kwake bungeni, Waziri huyo ameonyesha bayana kwanini hakupaswa kupewa kazi ya uwaziri! Katika utetezi wake bungeni, bwana Mathayo, alidai kuwa Wizara yake kuanzia mwaka 2006 imekuwa ikipewa fedha kidogo tofauti na zile ambazo ilikuwa ikiomba.

Lakini kwa bahati mbaya hakuonesha ni kwa namna gani amekuwa akitumia fedha hizo kidogo katika kutatua moja ya maagizo hayo tisa aliyopewa na rais! Hata hivyo, uamuzi wa Rais kuwaondoa mawaziri hao wanne hautakuwa na tija kama hatawaondoa pia viongozi wa Vyombo vya Dola ambavyo vimelaumiwa Ijumaa na wabunge kwa kuhusisha uvunjaji wa haki za binadamu; vitendo ambavyo vinafanana na vile ambavyo vilikuwa vikifanywa na makaburu wa serikali ya kibaguzi ya Afrika Kusini!

Viongozi wa Taasisi hizo wanaopaswa pia kufutwa kazi ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Kujenga Taifa, Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Mkugurugenzi wa Usalama wa Taifa na Kamanda wa Askari wa Wanyamapori.

Viongozi hao toka Taasisi nne nilizotaja, wanapaswa pia kuwajibishwa kutokana na usimamizi wao mbaya wa Vyombo vya Dola vilivyohusika moja kwa moja na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.

Serikali pia inapaswa kuwashughulikia Makatibu Wakuu wote na wakurugenzi wao wa Wizara nne husika, pamoja na ile inayosimamia Utawala Bora, Wizara ambayo pia inasimamia Usalama wa Taifa.

Hata hivyo serikali pia inapaswa kuchunguza kwa kina yale ambayo yamekuwa yakiendelea, hususan katika Wizara ya Mali asili na Utalii, hasa katika eneo la vitalu vya uwindaji na kadhalika. Kumekuwa na madai lukuki ya rushwa katika eneo hili!

Ikumbukwe pia kuwa ni viongozi waandamizi wa wizara hiyo hiyo waliodaiwa kuhuhusika na utoroshaji wa wanyamapori kwenda Jamhuri ya Kifalme ya Uarabuni, UAE, mwezi Septemba, mwaka 2010 wakati umakini wa viongozi wa nchi ulikuwa umemezwa na shughuli za uchaguzi mkuu!

Kadhalika ni viongozi hao hao wambao walidaiwa kuhusika, kwa namna moja au nyingine na kashifa ya kuitenga Loliondo na kakabidhi sehemu nyeti ya eneo hilo kwa waarabu chini ya mkataba tata!

Suala la Liliondo linalokaliwa na mtoto wa mfalme wa UAE linapaswa kutafutiwa ufumbuzi sasa kwani wakati utakuja wakati Rais wa Tanzania wakati huo atapaswa kuwajibika!

Swali ambalo tunapaswa kujiuliza ni; Kwanini viongozi waandamizi katika wizara hii wana kiburi cha kutisha cha hata kutompa ushirikiano aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Balozi Kagasheki?

Wabunge siku ya Ijumaa walihoji Usalama wa Taifa walikuwa wapi wakati yote haya yalikuwa yakitokea. Mimi nauliza, Waandishi wa Habari na Vyombo vya Habari walikuwa wapi? Tutafakari!

- See more at: Operesheni Tokomeza: Serikali kuwafukuza mawaziri wanne kazi haitoshi…! | Fikra Pevu | Kisima cha busara!
 
Ni kwa ugoro kama huu ndio nasema Watanzania hatutaendelea mpaka kiama.

Mawazo kama haya nasema ni mufilisi kwa vile yako centered on revenge-you scratch my back -I scratch yours.

Mtoa mada hii hajeleza popote the core issue, issue ya kuokoa wanyama pori wanaoteketezwa na wananchi hso hao wanao watetea.

Nasema ni msimamo wa kijinga kwa vile hso mawaziri wameondoka, so what?

Tatizo lipo pale pale!

Nawashangaa sana wabunge katika hiki maana wso wanataka mawaziri nyoro nyoro.

Ningewaelewa wabubge kama wangesema walioua kwa makusudi wapelekwe mahakamani, ili mkondo wa sheria uchukua hatima yake.
Hakuna mtu katumwa kuua, hilo liko wazi.

Mimi naomba rais asikie kilio changu na amchague Lembeli kuwa Waziri wa Misitu na Wanyamapori na aongoze operation ya Tokomeza Phase II.
 
Zenji walishapigwa risasi watu kama kuku sikusikia hata kwi, mie naona bora waachiwe tuu hao wanajeshi maana walikuwa wanachapa kazi....Ajali kazini :cool2:
 
niukweli usiopingika kama viongozi wa juu/mawaziri wamewajibishwa basi na wale wote waliohusika kwa namana moja au nyingine nao wawajibishwe ili kuleta heshima ya nchi,ikiwa kweli Taifa linaheshimu utawala wa sheria.
 
Jukumu namba moja la serikali yoyote halali Duniani ni kulinda raia na mali zake.Kuacha kulinda raia na mali zake ni kupoteza uhalali wa kutawala,operesheni tokomeza ujangili,imeua raia,mbaya zaidi ni operesheni ya kijeshi kwenye nchi ya kiraia.

Haitoshi mawaziri kujiuzulu,kwa kiwango ambacho wananchi wamedhalilishwa,wameteswa,wameuwawa,sio swala la mawaziri kujiuzulu tu,hivi kiwango cha wanawake kubakwa na wanajeshi 3,adhabu yake ni waziri husika kujiuzulu?hivi uhai wa mtanzania umekuwa na dhamani ndogo kiasi hiki?hivi taifa limefika mahali ambapo UTU wetu hauna dhamani?

Mawaziri wote ambao wamehusika na oparesheni hii wanapaswa kufikishwa mahakamani,na sio kujiuzulu,haiwezekani raia wauwawe tena wanauwawa na silaha zilizonunuliwa kwa kodi zao,eti waziri ajiuzulu kasha sote tunyamaze,au tuishie kuwataka wajiuzulu.Mawaziri na wote waliohusika wanapaswa kushitakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu,Natoa wito kwa wananchi kwa asasi mbalimbali kuwafungulia mashitaka. Imefika mahali kama wananchi tuchore mstari

Sehemu ya ripoti ya kamati teule ya Bunge
Kamati ilifanya mikutano mbalimbali katika baadhi ya maeneo ilikofanyika Operesheni Tokomezakwa lengo la kuwasilikiliza waathirika na kubaini mambo yafuatayo:-

Watuhumiwa kupekuliwa, kudhalilishwa na baadhi kutojulikana walipo

i. Mheshimiwa Spika, badhi ya wananchi wakiwemo viongozi, Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji na Watumishi wa Serikali walikamatwa na kudhalilishwa mbele ya wananchi wanaowaongoza. Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa walikuwa hawajulikani walipo hadi Kamati ilipozuru maeneo hayo. Mfano; Vijana watatu wa Kijiji cha Osteti, Kata ya Chapakazi, Wilayani Kiteto, walituhumiwa kujihusisha na biashara ya Meno ya Tembo. Vijana hao ni Nyafuka Ng'onja, Ng'onja Kipana na Mswaya Karani.

ii. Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa walidai kudhalilishwa mbele ya wanafamilia kwa kupewa adhabu wakiwa uchi na wanawake kushikwa sehemu za siri bila ridhaa yao. Mfano; ndugu Ali Nyenge (38) wa Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga alidai kuvuliwa nguo, kumwagiwa maji yaliyochanganywa na chumvi na kuchapwa viboko huku mwanae wa kiume (11) akishuhudia.

Pia alidai kulazimishwa kuchora picha ya Chatu kwa kutumia wembe kwenye paja lake. Vilevile, Bi. Neema Moses wa Babati alidai kuvuliwa nguo na kulazimishwa afanye mapenzi na wakwe zake na pia kuingizwa chupa sehemu zake za siri.

Aidha, baadhi ya akina mama walidai kubakwa na kulawitiwa. Mfano; katika Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga, mwanamke mmoja alidai kubakwa na Askari wawili (2) wa Operesheni Tokomeza Ujangili mida ya usiku. Vilevile, mama mmoja mkazi wa Kata ya Matongo Wilayani Bariadi, alibakwa na askari watatu (3) wa Operesheni Tokomeza Ujangili huku akiwa ameshikiwa mtutu wa bunduki

iii. Watuhumiwa waliokamatwa walifanyiwa upekuzi bila kuhusisha viongozi wa Serikali za maeneo husika na kutokuwepo kwa mashahidi na hati za upekuzi.

Mfano; Ndg. Abdallah Pata na Bi. Flora Mwarabu wa Kata ya Iputi Wilayani Ulanga na Ndg. Elias Cosmas Kibuga wa Gallapo Babati, walipekuliwa bila kufuata utaratibu.

Ukatili na Udhalilishaji katika Kambi za Mahojiano
iv. Mheshimiwa Spika, baadhi ya watuhumiwa waliopelekwa katika kambi za mahojiano walidai kuteswa kwa adhabu zinazokiuka haki za binadamu. Mfano; Diwani wa Kata ya Sakasaka wilaya ya Meatu Ndg. Peter Samwel, alidai kuadhibiwa akiwa mtupu kwa kupewa adhabu za kijeshi kama kuning'inizwa kichwa chini miguu juu, kupigwa kwa vyuma na kulazimishwa kufanya mapenzi na mti.

Mheshimiwa Spika, kutokana naukatili uliopitiliza, baadhi ya kambi za mahojiano zilipewa majina kama vile Guantanamo (Ruaha), Goligota (Ngorongoro), Duma na Andajega (Serengeti).
 
2.JPG

Mkuu wa Majeshi Nchini, Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema nao wametakiwa

kujiuzulu kutokana na uozo uliobainika katika ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili, iliyosababisha Rais

Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa mawaziri wake wanne.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katibu wa madiwani wa jiji hilo, Julian Bujugo

alisema wakuu hao wanapaswa kujiuzulu kwa kuwa wao ndio wanaotoa amri kwa askari wao na siyo mawaziri.

"Nao wanatakiwa kuchukua uamuzi wa kujiuzulu kama hatua ya kuonyesha uwajibikaji wao, askari wao

wamefanya maovu makubwa," alisema. Alisema kama wakuu hao wa watakaidi agizo la madiwani watalipeleka

suala hilo kwa Rais Kikwete.

"Watendaji wa Serikali ndio chanzo cha uonevu, hata mawaziri 'mizigo', nao wanatakiwa kujiuzulu. Alimtolea

mfano Waziri wa Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, Bujugo alisema ameshindwa kuwasimamia wakulima

na kusababisha mvutano na vurugu katika Sekta ya Kilimo.(P.T)

Chiza alitajwa kama waziri 'mzigo' na Kamati Kuu ya CCM iliyokutana wiki mbili zilizopita chini ya uenyekiti wa rais Kikwete.

Bujugo ambaye ni diwani wa Kata ya Magomeni alisema mbali na wakuu hao wa ulinzi na usalama, pia wakuu

wote wa wilaya waliohusika kusimamia operesheni hiyo nao wanapaswa kuwajibika kwa kuwa walijua na

waliona wazi vitendo vichafu walivyofanyiwa wananchi lakini walikaa kimya.

Ripoti ya tume ya kuchunguza Operesheni Tokomeza Ujangili ilisomwa bungeni mjini Dodoma mwishoni mwa

wiki iliyopita na mwenyekiti wa Kamati hiyo, James Lembelii na kuwango'a mawaziri hao.

Waliong'olewa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk

Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga

Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, huku Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa njia panda kutokana na wabunge

kuendesha mpango wa chini chini wa kupiga kura ya kutokuwa na Imani naye kwa maelezo kuwa ameshindwa

kuwasimamia mawaziri wake.

Chanzo:
Mwamunyange, Mwema wajiuzulu - Kitaifa - mwananchi.co.tz

In Protocol sense Nchi itakuwa unstable na Mapinduzi yanaweza kutokea...

Kwa kifupi ni JESHI HALIONGOZI na RAIS LINASHIRIKIANA NA RAIS KUIONGOZA NCHI - RAIS akiwa KIONGOZI WAO MKUU
 
Sio kujiuzulu mkuu katika utawala wa sheria wanapaswa kufukuzwa na kisha hatus za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
 
Ni kwa ugoro kama huu ndio nasema Watanzania hatutaendelea mpaka kiama.

Mawazo kama haya nasema ni mufilisi kwa vile yako centered on revenge-you scratch my back -I scratch yours.

Mtoa mada hii hajeleza popote the core issue, issue ya kuokoa wanyama pori wanaoteketezwa na wananchi hso hao wanao watetea.

Nasema ni msimamo wa kijinga kwa vile hso mawaziri wameondoka, so what?

Tatizo lipo pale pale!

Nawashangaa sana wabunge katika hiki maana wso wanataka mawaziri nyoro nyoro.

Ningewaelewa wabubge kama wangesema walioua kwa makusudi wapelekwe mahakamani, ili mkondo wa sheria uchukua hatima yake.
Hakuna mtu katumwa kuua, hilo liko wazi.

Mimi naomba rais asikie kilio changu na amchague Lembeli kuwa Waziri wa Misitu na Wanyamapori na aongoze operation ya Tokomeza Phase II.

Waambie bro, hawa sio wanasiasa kama mawaziri, huwa hawateuliwi ila wanapandishwa vyeo na kuwa walipo. Hivyo, hakuna askari anaejiuzulu. Labda aache kazi, afukuzwe, astaafu au kustaafishwa. Sasa wanaosema washtakiwe kwa kosa gani? Hawakuwapa askari kondom, fimbo au chupa. Hayo yalifanywa na askari kwa utashi wao " kama kweli yalitokea".
 
Kutokana na madudu waliyofanya wanajeshi kutesa na kudhalilisha raia kwa nini kwenye kuwajibika inakuwa ni waziri wa ulinzi ambaye hana kauli ya juu kwa jeshi hilo? embu wadau chambueni haya
 
Ni kwa ugoro kama huu ndio nasema Watanzania hatutaendelea mpaka kiama.

Mawazo kama haya nasema ni mufilisi kwa vile yako centered on revenge-you scratch my back -I scratch yours.

Mtoa mada hii hajeleza popote the core issue, issue ya kuokoa wanyama pori wanaoteketezwa na wananchi hso hao wanao watetea.

Nasema ni msimamo wa kijinga kwa vile hso mawaziri wameondoka, so what?

Tatizo lipo pale pale!

Nawashangaa sana wabunge katika hiki maana wso wanataka mawaziri nyoro nyoro.

Ningewaelewa wabubge kama wangesema walioua kwa makusudi wapelekwe mahakamani, ili mkondo wa sheria uchukua hatima yake.
Hakuna mtu katumwa kuua, hilo liko wazi.

Mimi naomba rais asikie kilio changu na amchague Lembeli kuwa Waziri wa Misitu na Wanyamapori na aongoze operation ya Tokomeza Phase II.

very sound, ningetamani watanzania walijue hili, mimi ninawalaumu sana hawa wanajeshi wanatumwa wakalinde pori badala yake wanaenda kubaka na kuua watu( na majitu yasiokua na utu na uzalendo kwa nchi na watu wake,)

ningekuwa na uwezo hawa watendaji wachache waliohusika kubaka na kutesa wangetupwa kuzimu watuachie nchi yetu
 
Jukumu namba moja la serikali yoyote halali Duniani ni kulinda raia na mali zake.Kuacha kulinda raia na mali zake ni kupoteza uhalali wa kutawala,operesheni tokomeza ujangili,imeua raia,mbaya zaidi ni operesheni ya kijeshi kwenye nchi ya kiraia.

Haitoshi mawaziri kujiuzulu,kwa kiwango ambacho wananchi wamedhalilishwa,wameteswa,wameuwawa,sio swala la mawaziri kujiuzulu tu,hivi kiwango cha wanawake kubakwa na wanajeshi 3,adhabu yake ni waziri husika kujiuzulu?hivi uhai wa mtanzania umekuwa na dhamani ndogo kiasi hiki?hivi taifa limefika mahali ambapo UTU wetu hauna dhamani?

Mawaziri wote ambao wamehusika na oparesheni hii wanapaswa kufikishwa mahakamani,na sio kujiuzulu,haiwezekani raia wauwawe tena wanauwawa na silaha zilizonunuliwa kwa kodi zao,eti waziri ajiuzulu kasha sote tunyamaze,au tuishie kuwataka wajiuzulu.Mawaziri na wote waliohusika wanapaswa kushitakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu,Natoa wito kwa wananchi kwa asasi mbalimbali kuwafungulia mashitaka. Imefika mahali kama wananchi tuchore mstari

Sehemu ya ripoti ya kamati teule ya Bunge
Kamati ilifanya mikutano mbalimbali katika baadhi ya maeneo ilikofanyika Operesheni Tokomezakwa lengo la kuwasilikiliza waathirika na kubaini mambo yafuatayo:-

Watuhumiwa kupekuliwa, kudhalilishwa na baadhi kutojulikana walipo

i. Mheshimiwa Spika, badhi ya wananchi wakiwemo viongozi, Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji na Watumishi wa Serikali walikamatwa na kudhalilishwa mbele ya wananchi wanaowaongoza. Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa walikuwa hawajulikani walipo hadi Kamati ilipozuru maeneo hayo. Mfano; Vijana watatu wa Kijiji cha Osteti, Kata ya Chapakazi, Wilayani Kiteto, walituhumiwa kujihusisha na biashara ya Meno ya Tembo. Vijana hao ni Nyafuka Ng'onja, Ng'onja Kipana na Mswaya Karani.

ii. Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa walidai kudhalilishwa mbele ya wanafamilia kwa kupewa adhabu wakiwa uchi na wanawake kushikwa sehemu za siri bila ridhaa yao. Mfano; ndugu Ali Nyenge (38) wa Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga alidai kuvuliwa nguo, kumwagiwa maji yaliyochanganywa na chumvi na kuchapwa viboko huku mwanae wa kiume (11) akishuhudia.

Pia alidai kulazimishwa kuchora picha ya Chatu kwa kutumia wembe kwenye paja lake. Vilevile, Bi. Neema Moses wa Babati alidai kuvuliwa nguo na kulazimishwa afanye mapenzi na wakwe zake na pia kuingizwa chupa sehemu zake za siri.

Aidha, baadhi ya akina mama walidai kubakwa na kulawitiwa. Mfano; katika Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga, mwanamke mmoja alidai kubakwa na Askari wawili (2) wa Operesheni Tokomeza Ujangili mida ya usiku. Vilevile, mama mmoja mkazi wa Kata ya Matongo Wilayani Bariadi, alibakwa na askari watatu (3) wa Operesheni Tokomeza Ujangili huku akiwa ameshikiwa mtutu wa bunduki

iii. Watuhumiwa waliokamatwa walifanyiwa upekuzi bila kuhusisha viongozi wa Serikali za maeneo husika na kutokuwepo kwa mashahidi na hati za upekuzi.

Mfano; Ndg. Abdallah Pata na Bi. Flora Mwarabu wa Kata ya Iputi Wilayani Ulanga na Ndg. Elias Cosmas Kibuga wa Gallapo Babati, walipekuliwa bila kufuata utaratibu.

Ukatili na Udhalilishaji katika Kambi za Mahojiano
iv. Mheshimiwa Spika, baadhi ya watuhumiwa waliopelekwa katika kambi za mahojiano walidai kuteswa kwa adhabu zinazokiuka haki za binadamu. Mfano; Diwani wa Kata ya Sakasaka wilaya ya Meatu Ndg. Peter Samwel, alidai kuadhibiwa akiwa mtupu kwa kupewa adhabu za kijeshi kama kuning'inizwa kichwa chini miguu juu, kupigwa kwa vyuma na kulazimishwa kufanya mapenzi na mti.

Mheshimiwa Spika, kutokana naukatili uliopitiliza, baadhi ya kambi za mahojiano zilipewa majina kama vile Guantanamo (Ruaha), Goligota (Ngorongoro), Duma na Andajega (Serengeti).
HIvi na wao wanavyodhalilisha tembo, mnaona sawa?? Wawataje na hao vigogo wanaoshirikiana nao...Baada ya kuona wanajulikana wahusika wote, wanageuza kibao na kushikilia bango la haki za binadamu. Pole saana Kagasheki....
 
Mwaka 1976 mauaji yalifanyika kwenye operesheni moja iliyoendeshwa na Wazara ya Mambo ya ndani iliyokuwa chini ya ndugu Ali Hassan Mwinyi.

Uchunguzi ulipofanyika kama huu wa Operesheni Tokomeza Ujangiri, waliojiudhuru walikuwa watatu yaani Waziri Ali Hassan Mwinyi, Mkuu wa Security ndugu Abdalah Natepe na mkuu wa mkoa nadhani wa Shinyanga ndugu. Siyovelwa.

Rashid Kawawa kwa sababu si executive-prime Minister kama wa Britain hakuguswa na hivyo Pinda hapaswi kuguswa kwa hili la juzi.

Leo operesheni kama hii hadi sasa, wameondoka mawaziri tu! Lakini executive level yaani watendaji hawajawajibika. Hivyo, kuna kila haja kwamba hata viongozi wakuu wa ngazi ya kitendaji kuwajibika kwa hili.

Jadili
 
Back
Top Bottom