Operesheni tokomeza: Mh. Assumpta Mshana awaponda upinzani wenye nia mbaya na serikali ya CCM

Mbunge huyu mama akichangia ameshindwa kabisa kuzuia itikadi zake na kuelekeza mashambulizi yake kwa chama cha upinzani huku akinyoosha kidole kwa wabunge wa (CHADEMA) ndio wamewatuma watu kufanya Operesheni Tokomeza na kupiga na kuua watu, ili watawale nchi hii. Zomea zomea zikaanza ikabidi spika Makinda aingilie kati na kumwambia mbunge huyu Mshana ajikite kwenye hoja iliyopo mezani.

halafu anatumia kodi ya hao wanaouawa shame on her and the one who appointed her
 
Ole Madeye alitaka kuinuka kwenda kumvamia Lema eti tu kwa sababu kaitwa "KIPINDUPINDU" wa ukabila kule Arusha kuhusu kuwachukia wale wote wasio wazawa wa jiji la Arusha.

Ole medeye ni kipindupindu atake asitake.....!!!Huyo Zambi nae mzigo tu,jaman Sugu yupo wapi??Mnyika,Halima mdee
 
Ole Madeye alitaka kuinuka kwenda kumvamia Lema eti tu kwa sababu kaitwa "KIPINDUPINDU" wa ukabila kule Arusha kuhusu kuwachukia wale wote wasio wazawa wa jiji la Arusha.

Ni noma! Tunataka bunge km hili!
 
Mkuu Leo siwaoni Hawa pro-Ccm kwenye hili jukwaa!

Juzi na Jana tuwaona wakimshambulia sn Mh Mbowe Kwa mambo Yake binafsi!

Mh Zambi na yeye anapingilia msumali! Anataka Hawa Wote wajiuzuru!

Ingawa nae huyo Zambi ni mzigo
 
Huyo mbunge kazima atakuwa bado hajapona. Manake hata CCM wenzake wanatetea hoja.
 
Teh teh teh, hao ndo wabunge wanaotokana na vyupi ni shida sana, yaani wamemezeshwa kitu kimoja tu kuisifia ccm na kuwaponda wapinzani basi!
 
asilimia kubwa kubwa ya wabunge wa CCM ni wanafiki na wanatafuta kiki,kama kweli wanauchungu kwa huu uovu wapige kura ya kutokuwa na imani ya serikali(impeachment) maana wao ni wengi na ndo wanapaswa kuongoza wenzao kwa idadi yao
 
Wabunge wakiweka nguvu kubwa Kama hii kwenye masuala ya uchumi basi uchumi wetu ungekua na Kasi ya ajabu Zaidi ya Husein Bolt!

Yani wangekua wanateua wizara mbili tu kila Mwaka Na kuzifatilia Kwa nguvu Yani tungekua mbali sn
 
Wanao paswa kujiuzuru
-Nchimbi na naibu wake
-Nahodha na naibu wake
-Mkuchika na naibu wake
-Kagasheki na naibu wake
-Waziri wa Sheria na naibu wake
 
Back
Top Bottom