'Operesheni Sangara' yatua Zanzibar

Mzee wa Kale

Member
Feb 7, 2009
44
0
na Mwandishi Wetu, Zanzibar


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimezindua Operesheni Sangara Zanzibar kwa kishindo na kueleza Zanzibar imekumbwa na ufisadi mkubwa wa ardhi na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Katika uzinduzi wa operesheni hiyo kwenye viwanja wa Koma wapya, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Mussa Yussuf, alisema hivi sasa misingi ya Mapinduzi ya mwaka 1964 imewekwa kando.

Alitoa mfano mwezi uliopita, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imenunua magari ya kifahari aina ya Toyota Prado yenye thamani ya mamilioni ya fedha, huku vituo vya afya na shule huduma zake zikizorota na wananchi kukumbwa na shida ya hali ya juu.

Yussuf, alisema magari hayo kila moja iligharimu sh milioni 100, fedha ambazo zingeweza kuondoa matatizo ya ukosefu wa dawa katika vituo vya afya na kupunguza msongamano wa wanafunzi katika madarasa na uhaba wa vifaa vya kufundishia na vifaa vya afya.

“Malengo ya Mapinduzi Zanzibar ilikuwa kuleta umoja kwa Wazanzibari na kuleta usawa kwa wananchi, ikiwemo kuwa na maisha bora na kuondoa ubaguzi wa aina zote,” alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.

Alisema Serikali ya Mapinduzi lazima ichukue hatua ya kuondoa tatizo la matumizi mabaya ya ardhi, kwa vile eneo hilo hivi sasa linakabiliwa na matatizo mengi na linaweza kuleta matatizo katika siku za baadaye.

“Rais wa kwanza wa Zanzibar alichukua ardhi na kuwapa wananchi, lakini mama na mwana wanachukua , hivi sasa tunasema Zanzibar kuna ufisadi mkubwa wa ardhi,” alisema.

Alieleza wananchi wa Zanzibar wanakabiliwa na matatizo makubwa yanayosababishwa na mfumko wa bei na kuathiri wananchi wengi wakiwamo wasio na uwezo.

Aidha, alisema matatizo yanayoikabili Zanzibar yanachangiwa na wawakilishi wa CCM na CUF kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Alisema CHADEMA haikubaliani na uamuzi wa SMZ kununua magari ya kifahari kwa ajili ya mawaziri, manaibu na makatibu wakuu kwa vile gharama za uendeshaji ni kubwa na hazilingani na hali halisi ya uchumi wa Zanzibar.
 
Sina uhakika na mavuno Zanzibar. Lakini ujumbe ni lazima upelekwe. Big up CHADEMA. Endeleeni kwa kasi zaidi.
 
"Malengo ya Mapinduzi Zanzibar ilikuwa kuleta umoja kwa Wazanzibari na kuleta usawa kwa wananchi, ikiwemo kuwa na maisha bora na kuondoa ubaguzi wa aina zote," alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.

Alisema Serikali ya Mapinduzi lazima ichukue hatua ya kuondoa tatizo la matumizi mabaya ya ardhi, kwa vile eneo hilo hivi sasa linakabiliwa na matatizo mengi na linaweza kuleta matatizo katika siku za baadaye.

"Rais wa kwanza wa Zanzibar alichukua ardhi na kuwapa wananchi, lakini mama na mwana wanachukua , hivi sasa tunasema Zanzibar kuna ufisadi mkubwa wa ardhi," alisema.







Alinyang'anya mali za watu
 
Back
Top Bottom