Operesheni Sangara yagundua Unyanyasaji na Uonevu Mkubwa kwa Wananchi wa Ulanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Operesheni Sangara yagundua Unyanyasaji na Uonevu Mkubwa kwa Wananchi wa Ulanga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtanke, Aug 11, 2012.

 1. M

  Mtanke JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 282
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Operesheni Sangara pamoja na vuguvugu la mabadiliko iliyoingia katika Jimbo la Ulanga Mashariki linaloongozwa na aliyekuwa waziri wa afya Dk Haji Mponda kabla ya kutemwa kwenye baraza la sasa imegundua mambo mengi ya uonevu kwa Wananchi wa Ulanga. Baadhi ya mambo ambayo yaliyotolewa kama kero na wananchi ni haya yafuatayo:-
  1. Katika kata ya Usangule na Mtimbila akina mama wanaojifungua hupaswa kulipia Tsh 15,000/= kwa kila mtoto wa kiume anayezaliwa na Tsh 20,000/= kwa kila mtoto wa kike anayezaliwa.
  2. Wananchi wanalazimishwa kujiunga na jeshi la mgambo na wale wanaokataa hukamatwa na kulazamishwa kulipa faini ya Tsh 20,000/= bila ya risiti
  3. Baadhi ya wafugaji wa Kisukuma walipigwa faini ya Tsh 1,000,000/= kila mmoja bila ya risiti kwa tuhuma za ng'ombe wao kuharibu mazingira wakati wakiwa wanalima.
  4. Mkuu wa Wilaya na OCD wameweka kituo cha kukusanya ushuru wa mazao kwa wakulima wa Tsh 3700/= kwa kila gunia la mpunga ambapo hupitia makusanyo kila weekend.
  5. Kuna tuhuma za askari kuwapiga wananchi hadi kuwaua
  Dk Mponda saidia wananchi wa Jimbo lako yasije yakakukuta ya Madaktari jimboni:eek2:
  Leo Operesheni inafanyika katika Kata 8 za Jimbo la Ulanga Magharibi na sasa Makamanda ndio wameingia Mahenge. Kesho itakuwa ni kata 4 za Ulanga Mashariki na 4 za Ulanga Magharibi
   
 2. A

  Aristides Pastory JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila la kheri M4C endeleeni kuwafumbua macho watu hao...

  N.B: ....''Watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa...''
   
 3. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  mtoto wa kike ni precious baby lazima ulipe zaidi! Si utamuuza! This is tz our country ambayo kila unapokanyaga pana mbuga,madini,gas,mafuta nk. Hongera nyinyiemu kwa kutesa wananchi mpaka watakapojitambua.
   
 4. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Halafu kiongozi aliyefanikiwa kuwatesa, kuwadhulumu na kusababisha pengine mauaji kwa raia kwa makusudi wanapongezwa na mkuu wa kaya kwa kuwateua kuwa mawaziri, Dc, Rc na mabalozi ughaibuni, hii nini maana yake?
   
 5. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,839
  Trophy Points: 280
  safi sana m4C bomoa ngome za CCM mpaka kieleweke mwaka huu....ELIMU vijijini ni kitu cha msingi sana
   
 6. M

  Mnyonge Namba1 JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Samahani mkuu:Dr Mponda ni wa ULANGA MAGHARIBI(lupiro, iragua, itete, mtimbira, sofi na Malinyi) na SIYO MASHARIKI(mahenge).
   
Loading...