Operesheni okoa nchi ina kuja 2020

mcoloo

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
918
1,401
Kwa mujibu wa ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali iliyo ibua wizi na madudu mengi katika uongozi huu wa awamu ya tano , niwazi kabisa kuwa mwana siasa atakaye kuja na slogan ya operesheni okoa nchi 2020 atatikisa na huwenda hata akabadili mtizamo wa wapiga kura wengi.
Ukweli ni kwamba ufisadi ulio fanyika katika serikali hii ya awamu ya tano, utabaki kuwa kumbukumbu katika historia ya nchi yetu.
Wenye akili walianza kuona dalili mbaya pale manunuzi ya vitu mbali mbali vilipo nunuliwa hata bila ya kufuata taratibu za kimanunuzi tulizo jiwekea kama taifa.
Hata fedha zilipo tolewa kwenye bank ndogo ndogo na kupelekwa Bot ,hapo napo wenye jicho la kuona mambo chanya , wakaona tatizo lipo.
Ufunguaji wa miradi mikubwa mingi bila hata ya kuweka vipaumbele, nalo likafungua milango ya wizi wa fedha za umma. Ukiukwaji wa taratibu za kibajeti zilizo pitishwa na bunge nayo ikawa shida.
Yote tisa ngoma ikaja pale alipo teuliwa jamaa mmoja anayeitwa Dotto James na kuwekwa katika idara nyeti inayohusu fedha, hapa napo viona mbali wakagundua kuwepo kwa utaratibu wa kuzichota fedha za umma bila ya utaratibu.
Ripoti cag imeibua upotevu wa hela nyingi sana, na huwenda ndio maana wanatamani sana atoke kwenye nafasi hiyo. Madudu ni mengi sana.
Na ndio maana nasema atakaye kuja 2020 na slogan ya operation okoa nchi atatikisa awe anatokea ndani ya CCM au hata kwa wapinzani.
Imefikia wakati ambao kama taifa tu ungane kulikomboa taifa letu kwa njia ya kupiga kura ( kwenye debe ) kutoka katika mikono iliyo jaa damu, wizi, unyang'anyi na dhuluma, nchi ambayo mbaya zaidi huru wa vyombo vya habari unazidi kuminywa ili wananchi wasipashwe yanayo endelea ndani ya nchi yao.
Mwenyezi Mungu tunakuomba sasa utuangalie wananchi wa nchi hii ili utuletee viongozi wenye hofu yako na wanyenyekevu 2020.
Ila kubwa ninatubu kwa niaba yao kuwa kwa umoja wetu kama taifa tume kutenda dhambi tusamehe na uikibali dua hii. Amina.
 
Hii inchi upepo utakuja kubadilishwa na kundi ambalo si wanasiasaa au mtu mmoja, maana mambo yanayoendelea watu wanaumia na hawajui wapi pakusemea sasa ipo siku tu litatokea tukio moja dunia mzima itataka kujua kipi kinaendelea tz na wanaichi wataibua hisia zao tuvumilie pengine mungu anaona hatuonewi ila siku mungu akiamua utashangaa binti wa kazi wa ndani ambaye ajulikani kabisa anaweza kuwa chanzo cha mabadiliko maana wanasiasa wote wanafiki wewe subilia ipo siku tu

Mifano ipo wazi South Africa ubaguzi wa rangi uliwatesa sana wana siasa walihangaika sana ila siku wale wanafunzi walipoandamana Soweto nakuuwawa dunia mzima ikakomaa na kinachoendelea south Africa

Misri napo yule kijana kujiwasha moto ikaibua hisia za watu

Sudan napo tumeshuhudia yule binti si mwanasiasa ni mwanafunzi tu kafanya mzee aikatae inchi

Kwaiyo hata sisi ipo siku amini si mwana siasa hata Yale mauaji ya akwelina ni Tyler bado picha itakuja tu serikali haitoamini
 
Hii inchi upepo utakuja kubadilishwa na kundi ambalo si wanasiasa ipo siku tu litatokea tukio moja dunia mzima itataka kujua kipi kinaendelea tz na wanaichi wataibua hisia zao tuvumilie pengine mungu anaona hatuonewi ila siku mungu akiamua utashangaa binti wa kazi wa ndani ambaye ajulikani kabisa anaweza kuwa chanzo cha mabadiliko maana wanasiasa wote wanafiki wewe subilia ipo siku tu

Mifano ipo wazi South Africa ubaguzi wa rangi uliwatesa sana wana siasa walihangaika sana ila siku wale wanafunzi walipoandamana Soweto nakuuwawa dunia mzima ikakomaa na kinachoendelea south Africa

Misri napo yule kijana kujiwasha moto ikaibua hisia za watu

Sudan napo tumeshuhudia yule binti si mwanasiasa ni mwanafunzi tu nafanya mzee aikatae inchi

Kwaiyo hata sisi ipo siku amini si maana siasa hapana ile ya akwelina ni Tyler bado picha itakuja tu serikali haitoamini
Inshallah
 
Back
Top Bottom