dvj nasmiletz
JF-Expert Member
- Jul 23, 2018
- 2,020
- 2,157
Dah.ndo maana sipendag story za humuMhuni tu guyu jamaa mama eeeh
Dah.ndo maana sipendag story za humuMhuni tu guyu jamaa mama eeeh
Angesema mapema basiImebaki ya kulipia ada eti
Buku mbili tu mkuu
Kifaa kilikuwa na shida kidogo, leo ndo nimerudi hewani mkuu.Walisema watu
Wakaonekana wanafiki
Umeeleweka vyema mkuuPole Sana kama huwa nakukwaza hadi uone naringa kiasi hicho!!
Pia nisamehe kwa maringo yangu yanayokukwaza!!.
Tazama sehemu ya tatu jana nimejitahidi kuiposti saa saba usiku nadhani utaelewa kwa nini iwe huo muda wewe ukiwa umelala.
Lakini nisamehe pia kwa kuwa huwa naipeleka whatsapp wakati wewe unataka usome bure kabisa bila hata kunitumia vocha ya kukwangua nijiunge ili usome!!
Lakini pia naomba nikuulize upo nchi gani ambayo huwezi kupata mia tano tu (500) ya kununua riwaya mwanzo mwisho?.
Huna whatsapp tumia email, huna email tumia whatsapp..
Nchi yoyote Duniani unaweza kunitumia na nikapata mia tano tu, au elfu moja ikizidi sana huwa elfu mbili.
Na mwisho nikukumbushe kuwa hii ni kazi kama kazi zingine wala si kufurahisha watu bure, ndo mana ili uandike lazima ufanye utafiti kwa kina ikibidi usafiri mkoa au nchi kutafuta ukweli wa kile unachotaka kuandika.
Nadhani umeona kuna mdau huko juu kanitisha kwamba naandika vitu deep sana, unadhani nikiandika kwa kukurupuka bila tafiti nitapata vitisho hivyo ambavyo watu wanakuja hadi pm kuniomba nipunguze ukweli katika riwaya zangu hizi? Unajua garama inayotumika hadi naandika kitu kinachokuvutia bila kukutoa kwenye reli ya usomaji?.
Lakini dada yangu nikwambie kitu, duniani hakuna kitu cha bure na ndo mana hapa Jf unanunua vocha na bado google wanakulipia ili uingie bure kwa kuwa wanamlipa Melo. Kama wasingekuwa wanamlipa basi tungeingia kwa kulipia kama zilivyohuduma zingine duniani za kupata habari!!!
Narudia tena kukuomba radhi kama nimekukwaza ama nimekwaza yeyote kwa utaratibu wangu huu, ila hii ni kazi kama kazi zingine na ndo mana ina hati miliki kila kazi unayoona naweka hapa na huko pia nalipia ili kulinda kazi yangu.
Hivyo nisamehe bure kwa maringo yangu yanayokukwaza lakini jifunze kuheshimu kazi za watu bila kutoa lugha ya kuudhi ama kukera. Wapenzi wa riwaya hawana lawama wanajua ugumu wa kazi na faida wanazopata kwa kusoma kazi za wengine!!.
Afu mi niko poa Sana sema gubu lako tu, mimi wengi nimekuwa nawapa bure kama hawana pesa!! Waniomba kistarabu tu nawaelewa!!
Wapo hapa labda watakupa ushuhuda wa vile nilivyo.
Lakini pia kuna wezi wa kazi za watu, ukiweka hadi tamati anachukua na kuwek kwenye page yake au blog na kuuza! ....
Nimeamua kukujibu kirefu ili unielewe na wengine wenye kuniona nina maringo nao wajue kwa nini ipo hivyo!! Hakuna mwandishi anaetoa bure siku hizi,hii ni kazi kama kazi zingine!!
Nisameheni wote niliowakwaza!!
hahahah...nini tena mkuu?we jamaa una roho mbaya sana