Operesheni KuKu (kufa kupona). riwaya ya kijasusi

Duuuuh! Unasoma huku karoho kanaenda mbio
RIWAYA; OPERESHENI KUKU (KUFA KUPONA)

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA NANE


Makomando watano walianguka sehemu moja huku komando mmoja akikosekana na alikuwa ni wa mwanzo kabisa kujirusha chini.

“Yuko wapi Pete?” Rambo alimhoji Rat.

“Nimeshuka mwenyewe na akafuatia Paroko; yeye sijamuona” Rat alijibu.

“Guys,it’s a problem!” Rambo aliwambia wenzake.

“Yah! Ni tatizo tangu tulipokuwa angani” Macho yote yakamtazama Odwe aliesema hivyo.

“Kelele zote mlizosikia napiga zilikuwa ni kumkumbusha Pete afunge vyema mkanda wake mmoja na nilipoona anadive nikajua tutamkosa!” Odwe alifafanua.

“Ooh shit!!” Kila mmoja alitamka kivyake.

“Tumjaribu kwenye simu yake!” Paroko alishauri huku akichomoa simu ya upepo kiuoni mwake na kisha kujaribu kupiga.

Wote walikuwa makini kufuatilia matokeo.

Ikawa sivyo walivyogegemea, simu ikaendelea kuonesha taa nyekundu kisha ikamulika mara tatu na kuzima kabisa.

Makomando wakaingiwa na fadhaa.

Simu ya Pete ilikuwa haipatikani.

Makomando wale walijitoa pale walipokuwa na kutambaa chini kidogo kisha wakatulia tuli huku wakitizama anga kuona kama wataona mwanga wowote wenye kuwaashiria lolote hasa kwa Pete.
Odwe bado fikira zake zilikuwa kwa Pete na aliona kabisa Pete ni kama alifanya makusudi hivi kuvaa vile na hata pale alipomwita aligeuka na kumchekea kabla hajajirusha.

“Guys,this thing was planned!” Odwe aliwambia wenzie.

“Tusifike huko wapendwa! Tupo pamoja kwa miaka mingi sana na hatujawahi kudouble cross why leo? Ni mistake tu ndogo!” Rambo alikemea huku akizungumza kwa sauti ya mamlaka.

Na mjadala ukakomea pale.

Lakini kwa nini Pete aliamua kufanya vile ni makusudi ama bahati mbaya? Na kama ni bahati mbaya kwa nini iwe ni katika misheni hii na siku huko nyuma.

Pete hayupo na hakuna wa kuwajibu.

Waliendelea kusubiri kwa zaidi ya dakika kumi bila kuona lolote likiendelea ama ishara yoyote ambayo ingeweza kuwaarifu uwepo wa Pete maeneo yale au mbali na pale.
Makomando wale watano waliona kuendelea kukaa pale ni kupoteza wakati na watakuwa ni kinyume na muda waliohitaji kuutumia kukamilisha mpango wao.

Rambo alitoa ishara kwa wenzake na wakajikusanya kwa pamoja ili wapange upya mipango yao. Waliamua kujipanga upya kwa kuwa mwenzao mmoja hakuonekana, na hawakujua alipo usiku huo. Ilikuwa ni lazima wajipange upya tena ili kuona namna ambavyo wanaweza kukamilisha misheni yao, bila kuwapo mdunguaji mmoja.

“Odwe inabidi ukae upande ule ambao alitakiwa awepo Pete na unatakiwa utumie ujuzi wako wote kuhakikisha wapiganaji walioko kwenye vidungu wanatoka;mimi na Paroko tutakuwa sambamba huku shotii ukiwa nyuma yetu kuhakikisha usalama zaidi.” Rambo alielekeza upya na baada ya hapo kila mmoja aligeuka na kuanza safari msituni.

Ilikuwa ni safari ya kimya kimya huku vizuizi vya hapa na pale wakivikwepa. Iliwapasa watumie nusu saa kufika usawa wa kambi ya waasi,ila wakiwa wamebakiza kama dakika kumi kuifikia kambi, kuna kitu Shotii alihisi nyuma yake, haraka akapiga sauti ya hisi “psii” na makomando wote kwa pamoja wakaruka kila mtu kivyake na kuangukia katikati ya nyasi kisha kila nmoja akatulia tuli, kusubiri ishara zaidi.

Shotii ambae katika msafara ule alikuwa nyuma, alikuwa amehisi uwepo wa mtu mwingine zaidi nyuma yao, ila kila alipojitahidi kugeuka na kutazama, hukuona mtu.

Lakini masikio yake bado yalizidi kuhisi uwepo wa nyayo ngeni katika msafara wao na ndipo akawapa ishara wenzake na wakachukua tahadhari kila mmoja na upande wake.

Ni Shotii tena aliesimama na kuwapa ishara wenzake ya kuwa mambo ni shwari. Lakini licha ya ushwari huo bado hakuacha kuwatahadharisha uwepo wa kiumbe nyuma yao.

Safari iliendelea kwa umakini zaidi, na kila mmoja akiwa makini sana na mlango wa sita wa fahamu.
Tofauati na matarajio yao, kila kitu kilienda sawa na hakuna sauti wala mkwaruzo uliowasumbua tena.

Licha ya utulivu wote huo, ila bado Odwe alikuwa na dukuduku moyoni. Yeye aliamini kabisa sauti iliokuwa nyuma yake,ilikuwa ni sauti ya mtu au watu na walikuwa wanawala miguu.

Walifika hadi sehemu waliokuwa wamepanga kuweka ukomo wa safari yao. Na kama kawaida ya kazi yao, mara nyingi sana wadunguaji ndio hutangulia kuangalia usalama kisha kutoa taarifa.

Rat alielewa cha kufanya; Haraka akakimbia msituni kwa kutumia kanuni maalumu za kujificha kwa adui.

Alifika sehemu alioona kwake ni sahihi kujificha, akaweka makao juu ya mti na kisha akajipaka dawa maalumu ya kuzuia kushambuliwa na wadudu wa usiku.

Akaweka sawa bunduki yake ya kudungulia umbali wa mita 1500. Ilikuwa ni silaha yake pendwa ya Sniper rifle 338 Lapua Magnum.

Silaha hii pia ilikuwa na darubini pandikizi yani eye piece lens.

Rat alitulia tuli huku akiangalia mazingira vizier na alipojiridhisha akaamua kuwaita wenzake ambao walipaswa kuingia ndani ya kambi. Akawasha simu yake ya upepo na kuwapa taarifa Rambo na wenzake, kisha akamtafuta Odwe ambae kwa upande wake nae alikuwa ameanza kucheza na uhai wa wapiganaji waliokuwa kwenye vidungu nyuma ya kambi.

Baada ya Rat kuwasiliana na Odwe; nae aliamua kuanza kazi ya kutungua wapiganaji wale ambao walikuwa wanazungusha taa za ulinzi huku na huko.

Kwenye kidungu cha kwanza na cha pili, alitumia dakika mbili tu kukamilisha kazi aliohitaji kuifanya. Tayari watu sita walikuwa hawana uhai kutoka kwenye bunduki matata ya Rat. Mdomo wa bunduki yake yenye kiwambo cha kuzuia sauti, akauelekeza upande wa kushoto kwake na akataka kuweka vyema shabaha yake, akasita.

Kuna kitu aliona.

Alimuona mtu akiwa amevaa mavazi sawa na yale waliokuwa wamevaa wao.
Akatumia darubini ya kupandikiza kukuza ili apate kuona vyema.

Akaguna.

Akarejea tena kutazama, na hapo akajiridhisha kabisa ya kuwa amemuona Pete akiwa chini ya milingoti minne iliobeba kidungu.

“Ana fanya nini tena huyu!” Rat akajiuliza huku akichukua simu yake na kutaka kupiga kwa Rambo kumpa taarifa, akasita kwa mara nyingine.

Kwa nini!!!

Kwa sababu alimuona Pete akitega bomu pale chini.
Na alikumbuka kwamba wao hawakuwa wamebeba mabomu ya moto, zaidi walikuwa na mabomu bandia yaani plastic explosive.

Kwa nini!!

Kwa sababu hawakutaka wajulikane kama ni wao ndio wameendesha operesheni ile.

“Anafanya nini huyu bwege!!” Rat akajiuliza na kabla hajachukua uamuzi mwingine tena, alama nyekundu kwenye simu yake ikapata uhai kuashiria kuna simu nyingine inaingia.

Akabonyeza kitufe ubavuni mwa simu yake.

Alikuwa anapokea ujumbe kutoka kwa Odwe; Odwe alikuwa anampa taarifa ya kuwa upande wake amemaliza kazi,hivyo alibaki peke yake ambae anatakiwa atoe ripoti na kikosi cha chini kianze kazi ya kuingia ndani ya kambi.

Haraka Rat akaweka sawa bunduki yake na kulenga wapiganaji waliokuwa wamesalia kwenye kidungu kile.
Alipomaliza akashusha tena darubini yake pale alipokuwa Pete; Hakumuona.

Yawezekana ni kosa ambalo hakujua kama analifanya,badala ya kutoa taarifa ya kile alichoona, yeye akaruhusu Rambo; Paroko na Shotii wasonge mbele kuelekea kwenye nyumba ambayo waliiwekea tageti kwa nia ya kufanya wokozi.

Rambo aliinuka kidogo na kisha akanyoosha kidole kimoja juu, hapo waliokuwa nyuma yake wakajiweka sawa kisha akachezesha mkono ulionyosha kidole mara mbili kwa kwenda mbele.
Paroko alijua ni yeye anaepewa ishara ile na haraka akaanza kumfuata Rambo.
Hatua zao zilikuwa ni zenye uhakika huku darubini pandikizi walizofunga kwenye bunduki zao ambazo zilikuwa ni Night vision goggles, zikiwasawaidia kuona mbele huku wakikabiliana na kila mpiganaji aliekatiza mbele yao.

Baada ya kuingia ndani kabisa ya kambi ya waasi; Rambo na Paroko walifika pahali ambapo sasa walihitaji kutulia kidogo na kutazama mazingira kabla ya kuvamia nyumba ambayo ilikuwa na mateka.

Walitulia kwenye vifusi vilivyotengenezwa na waasi huku chini kukiwa kuna maiti mbili za wapiganaji waliokuwa pale kabla hawajakutana na mikono ya Paroko.

Wakati wao wakiwa wametulia pale, upande wa pili alikokuwa Rat kuna jambo lilikuwa linamtokea.

Ni wakati alipokuwa ametulia mafichoni, mara simu yake ikaanza kupokea mkoromo wa ajabu kuashiria kuna simu ngeni ilikuwa inaingilia mawimbi ya simu yake.
Taa ya kijani na nyekundu zikaanza kumweka kwa pamoja.

Ilikuwa ni ajabu kidogo, ila alijua ni yawezekana kuna mawasiliano ambayo yanataka kufanyika na mtu aliekaribu yake.

Akarejesha jicho lake kwenye darubini na alianza kupitia maeneo yote ya karibu yake kwa umakini mkubwa.

Hakuona lolote la kutisha.

Lakini bado simu yake ilizidi kukoroma mithili ya radio inayokata mawimbi yake.

Akawaza kuizima kwa muda, na wakati huohuo akiweka sawa darubini yake ili irekodi picha wakati akishugulika kuizima.

Akaizima kwa sekunde kadhaa kisha akaiwasha tena.

Aliporidhika ipo sawa,akarejesha macho yake kwenye darubini pandikizi na kuyarejea matukio ilionasa.

E bana ee!!

Sura ya Pete ilikuwa imeonekana akihama eneo moja kwenda jingine.

“Huyu bwege si atulie tu na tukimaliza tumshitue!!” Rat aliongea kwa kugafilika.

Simu yake ikakoroma tena, na safari hii ikafuatia na mkoromo wa simu nyingine pale chini alipokuwa.

Haraka akatazama pale chini na macho yake hayakuamini kile alichokiona pale.

Pete alikuwa na mtu mwingine wakitizama juu ya mti aliokuwa.

Hisia mbaya zikamtambaa na haraka akakumbuka onyo la Odwe kuhusu Pete.
Rat akataka kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja; alinyakua simu yake kiuononi na kidole kikaelekea sehemu ya kupigia na huku mwili wake wote ukitaka kujitoa kwenye tawi la mti ili ahamie upande mwingine tena wa mti, lakini mguu wake wa kushoto ukanasa katikati ya maungio ya tawi mbili zilizoacha na kisha ukakwama kwenye majani mengi yaliokuwa yamejisokota pamoja.

Wakati akiwa katika mkwamo huo, tayari mkono wa kushoto wenye simu ulikuwa unakaribia kinywani kwake.

Lakini kuna jambo lingine zaidi lilimtokea akiwa katika harakati hizo za kujiokoa na kutaka kuwaarifu wenzake.
 
Tatizo akiona wafuatiliaji wamekuwa wengi anaanza kuringa, mara ana majukumu, mara anaumwa halafu baadae anasema inauzwa.
Uandishi wa riwaya ni Kazi kama Kazi nyingine hivyo naye anahitaji support inapobidi
 
Pole Sana kama huwa nakukwaza hadi uone naringa kiasi hicho!!

Pia nisamehe kwa maringo yangu yanayokukwaza!!.

Tazama sehemu ya tatu jana nimejitahidi kuiposti saa saba usiku nadhani utaelewa kwa nini iwe huo muda wewe ukiwa umelala.

Lakini nisamehe pia kwa kuwa huwa naipeleka whatsapp wakati wewe unataka usome bure kabisa bila hata kunitumia vocha ya kukwangua nijiunge ili usome!!

Lakini pia naomba nikuulize upo nchi gani ambayo huwezi kupata mia tano tu (500) ya kununua riwaya mwanzo mwisho?.
Huna whatsapp tumia email, huna email tumia whatsapp..

Nchi yoyote Duniani unaweza kunitumia na nikapata mia tano tu, au elfu moja ikizidi sana huwa elfu mbili.

Na mwisho nikukumbushe kuwa hii ni kazi kama kazi zingine wala si kufurahisha watu bure, ndo mana ili uandike lazima ufanye utafiti kwa kina ikibidi usafiri mkoa au nchi kutafuta ukweli wa kile unachotaka kuandika.

Nadhani umeona kuna mdau huko juu kanitisha kwamba naandika vitu deep sana, unadhani nikiandika kwa kukurupuka bila tafiti nitapata vitisho hivyo ambavyo watu wanakuja hadi pm kuniomba nipunguze ukweli katika riwaya zangu hizi? Unajua garama inayotumika hadi naandika kitu kinachokuvutia bila kukutoa kwenye reli ya usomaji?.

Lakini dada yangu nikwambie kitu, duniani hakuna kitu cha bure na ndo mana hapa Jf unanunua vocha na bado google wanakulipia ili uingie bure kwa kuwa wanamlipa Melo. Kama wasingekuwa wanamlipa basi tungeingia kwa kulipia kama zilivyohuduma zingine duniani za kupata habari!!!

Narudia tena kukuomba radhi kama nimekukwaza ama nimekwaza yeyote kwa utaratibu wangu huu, ila hii ni kazi kama kazi zingine na ndo mana ina hati miliki kila kazi unayoona naweka hapa na huko pia nalipia ili kulinda kazi yangu.

Hivyo nisamehe bure kwa maringo yangu yanayokukwaza lakini jifunze kuheshimu kazi za watu bila kutoa lugha ya kuudhi ama kukera. Wapenzi wa riwaya hawana lawama wanajua ugumu wa kazi na faida wanazopata kwa kusoma kazi za wengine!!.

Afu mi niko poa Sana sema gubu lako tu, mimi wengi nimekuwa nawapa bure kama hawana pesa!! Waniomba kistarabu tu nawaelewa!!
Wapo hapa labda watakupa ushuhuda wa vile nilivyo.

Lakini pia kuna wezi wa kazi za watu, ukiweka hadi tamati anachukua na kuwek kwenye page yake au blog na kuuza! ....


Nimeamua kukujibu kirefu ili unielewe na wengine wenye kuniona nina maringo nao wajue kwa nini ipo hivyo!! Hakuna mwandishi anaetoa bure siku hizi,hii ni kazi kama kazi zingine!!

Nisameheni wote niliowakwaza!!
Uko sahihi mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom