Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
CHADEMA itaendelea kuwa shamba la bibi baada ya wajanja kugundua kuwa njia rahisi ya kutumbua ruzuku ni kuanzisha operesheni zisizo na kichwa wa miguu. Baada ya UKUTA kuyeyuka wajinga waliambiwa kuwa kuna mazungumzo yanasubiriwa baina ya akina Mbowe na 'viongozi wa dini'. Baada ya kugundulika hakuna mazungumzo yoyote kati ya Mbowe na viongozi wa dini, wakadanganywa watulie kwa sababu UKUTA umeingia moyoni eti UKUTA umefanikiwa kwa 100%. Kilichoshangaza ni mamia ya mamilioni kutumika bila maelezo.
Sasa wanadanganywa tena, operesheni 'kata funua'. Wanahalalisha matumizi ya ruzuku huku ofisi na watumishi wa chama wakiwa hoi kifedha. Kampeni hii imeshafeli kabla ya kuanza badala yake kumekuwa na uongo kwenye mitandao ya kijamii. Na sasa CHADEMA imegeuka adui wa nchi, kupiga ramli ili nchi ipatwe na mabaya, wafuasi wake wanafurahia mabaya tu. Kwa sasa CHADEMA imejikita katika yafuatayo;

- Kufoji akauti za viongozi wa serikali katika mitandao ya kijamii na kutoa matamko halafu wanaanza kujadili wenyewe kwa lengo la kuzua tafrani.
- Kutoa nyaraka za uongo kuhadaa umma ambazo kimsingi hudumu kwa muda mfupi.
- Kupotosha hotuba za viongozi ili kutoa taswira hasi. nk nk.nk.