'Operesheni Haki' yafika Mkoa wa Kilimanjaro, mashambulizi yaongozwa na Salum Mwalimu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
87,062
2,000
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinaendelea na mkakati wake mpya wa kudai haki kwa njia ya amani kwa kushinikiza uwepo wa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi , vikao vya ndani vishaanza kurindima huku na kule ambapo sasa vimetinga Mkoa wa Kilimanjaro , huku mashambulizi hayo yakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Zanzibar Mh Salum Mwalimu.

FB_IMG_1622028819862.jpg
FB_IMG_1622028827844.jpg
FB_IMG_1622028835230.jpg


Mungu ibariki Chadema
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,198
2,000
Hatimae taifa limepata "UHURU" kutoka kwa mkoloni mweusi.

Mama Samia mungu ampe umri mrefu na wenye afya, njia anayopita hakika inaleta faraja sana kwa wananchi. Watu wanamtolea maneno maswala ya kurudisha "IKULU" ndani ya Dar ila hawaoni sababu zinazomfanya awepo Dar, wamekaa kuishi maisha kwa kukariri na wala hawajui sababu ya kwanini "Nyerere alifanya Dodoma kuwa Mji Mkuu".

Kuwepo kwake Dar sasa hivi kuna rahisisha kuonana na;

1) Wafanyabiashara wa kubwa ulimwenguni, africa na tanzania (Mfano Alhaj Aliko Dangote) ili kuwashawishi warudishe biashara nchini na wafungue viwanda zaidi, ili watanzania wapate ajira.

2) Mabalozi wa mataifa mbali mbali ambao ofisi zao zipo Dar Es Salaam, kuwashawishi walete wafanyabiashara kutoka katika mataifa yao (Mfano Mabalozi Wa Saudia jana alipokutana nao).

3) Kuifufua Dar Es Salaam kuwa "BUSINESS HUB & BUSINESS CITY" baada ya kuuliwa kwa miaka 5.

4) Kuweka mazingira mazuri na wafanyabiashara waliowekeza Dar.
 

NORTHERNIST

JF-Expert Member
Feb 10, 2021
227
250
Huo uhuru wa nyie kuzunguka na kuyasema yote ni kwa sababu mnalindwa na katiba hii hii sasa sijui mnataka katiba ya kuwaruhusu kufanya hadi uhaini muachwe? ifike mahali CHADEMA muwe na agenda za maana sio hizi drama mnazofanya now itafika mahali wananchi watawachoka hata wa kuwasikiliza kwenye mikutano mkakosa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom