Operesheni Haki: Kampeni za kimataifa kuwafikia Diaspora. Mbowe, Lissu, Mnyika kuhutubia

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,373
217,435
Baada ya kukamilisha Operesheni Haki kwenye kanda 10 za Tanzania kwa mafanikio makubwa, sasa ni zamu ya Kimataifa, Tundu Lissu, John Mnyika pamoja na mwamba mwenyewe Freeman Mbowe kuunguruma kidigitali.

Wote Mnakaribishwa.

Baada_ya_Operation_HAKI_kwenye_kanda_10_za_Chama_Tanzania_sasa_ni_zamu_ya_Chadema_Diaspora.%0A...jpg
 
EeeeNHeeee!

Mkienda kidigitali hivyo, hakika hata walioziba masikio watayafungua na kuwasikiliza.

Kazi kubwa kwenu katika kutumia njia hii, ni namna ya kufungasha (package) ujumbe ili uwe rahisi kuutafuna na kuuchengua (digest?).

Hapa nawapa pointi stahiki yenu, ni kazi nzuri.

Lakini kumbukeni, 'innovation' haiwezi kuwa mbadala wa sera zinazokubalika na wengi. Akili zenu siku zote, zielekezeni huko.

Kwa maoni yangu, hapo ndipo palipobaki, mkiweza kuzipolish vizuri sera zenu zieleweke na wananchi, kazi ya kumsukuma mlevi shimoni itakuwa rahisi, kama a ba cha, da
 
Huo udiasporani sawa ila huku Bongo marufuku,Tzn tunataka wawekezaji sio wababaishaji kama hao uliowataja
 
Safi sana diaspora na wadau wa maendeleo wafahamu hali halisi ya kisiasa, kijamii na kiuchumi katika siku 100 zilizopita za awamu ya 6.
Wadau wa maendeleo hawana shida na siasa za kuwazuia wapinzani ila Wana shida ya kuzuiwa maslahi yao.

Kama sera za biashara na uchumi ziko poa nani atahangaika na kelele zisizowasaidia Wazungu kupata chochote kitu?
 
Back
Top Bottom