Operation UKUTA:Sera ya Viwanda itakaposhindwa,watasingizia Political Unrest

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Kinachoendelea mpaka sasa ni majigambo kama yale ya mabondia na kelele za kila kikucha majukwaani lakini uhalisia hakuna na hata dalili za uhalisia kuhusu kutekeleza sera ya viwanda hazionekani.

Miezi 9 inakatika sijui ukiwaambia wakupe orodha ya wafanyabiasha /wawekezaji wanaotaraji kuja kuwekeza hapa nchini watakuwa nayo sana sana watakuja na ahadi za Waziri Mkuu wa India na mambo ya aina hiyo.

Hivyo basi, iwapo operation UKUTA itatekelezwa na yakatokea ya kutokea, sitashangaa wakija na propaganda kuwa hali mbaya ya kisiasa ndio imefukuza wawekezaji na wanaweza kusema kabisa hii ndio agenda ya CHADEMA kumbe yamewashinda.

Inashangaza sana kuona watu wanaohubiri amani lakini wakiitwa kwenye vikao vya maridhiano hawatokei huku wakitoa sababu zisizo na mashiko.

Tusubiri muda ndio msema mkweli.
 
Unataka ndani ya miezi tisa kuwe na viwanda vingapi?
Mwezi uliopita PM aliweka jiwe la msingi la kiwanda kikubwa cha nondo kibaha,unataka nikuambie kingine kinachojengwa?
 
Mbona hilo liko clear ni taifa gani limestawi kukiwa na political unrest, Hivyo viwanda vitakuja kwa watu kutojishughulisha?
Serikali ikishindwa sio jambo la kufurahi na kushangilia, kuna watu kuta kuchwa mawazo yao ni kusubiria kuona wenzao wakiboronga ili hali mkijua kuwa atakayepata shida sio yeye peke yake, hata 2020 ikiingia chadema Magufuri and his team mates wataendelea kula pension nzuri tu, Lakini vipi walalahoi wa nchi yetu??? Kushindwa kwa serikali nikushindwa kwa wananchi na inapaswa kuwa aibu kwetu sote
 
Unataka ndani ya miezi tisa kuwe na viwanda vingapi?
Mwezi uliopita PM aliweka jiwe la msingi la kiwanda kikubwa cha nondo kibaha,unataka nikuambie kingine kinachojengwa?
Watu wana mambo, wakati ukianza kupima hata utekelezaji wa mambo binafsi nyumbani kwetu unaona ni shida, viongozi ni taswira ya jamii yetu ilivyo, wamelelewa na kukua miongoni mwetu, Mengi wanayoyafanya ndivyo wengi tulivyo sema kwa kuwa sisi hatujapata nafasi basi macho yetu yanaona vibanzi vya wenzetu vizuri sana bila hata ya msaada wa miwani
 
Kinachoendelea mpaka sasa ni majigambo kama yale ya mabondia na kelele za kila kikucha majukwaani lakini uhalisia hakuna na hata dalili za uhalisia kuhusu kutekeleza sera ya viwanda hazionekani.

Miezi 9 inakatika sijui ukiwaambia wakupe orodha ya wafanyabiasha /wawekezaji wanaotaraji kuja kuwekeza hapa nchini watakuwa nayo sana sana watakuja na ahadi za Waziri Mkuu wa India na mambo ya aina hiyo.

Hivyo basi, iwapo operation UKUTA itatekelezwa na yakatokea ya kutokea, sitashangaa wakija na propaganda kuwa hali mbaya ya kisiasa ndio imefukuza wawekezaji na wanaweza kusema kabisa hii ndio agenda ya CHADEMA kumbe yamewashinda.

Inashangaza sana kuona watu wanaohubiri amani lakini wakiitwa kwenye vikao vya maridhiano hawatokei huku wakitoa sababu zisizo na mashiko.

Tusubiri muda ndio msema mkweli.
Kwani maandamano yanazuia vipi Magufuli kuanza kujenga standard rail gauge kwenda Mwanza-Kigoma from Dar?
 
Unataka ndani ya miezi tisa kuwe na viwanda vingapi?
Mwezi uliopita PM aliweka jiwe la msingi la kiwanda kikubwa cha nondo kibaha,unataka nikuambie kingine kinachojengwa?

Kiuchumi serikali ya Rais Magufuli ina chini ya miezi mitatu.
 
Unataka ndani ya miezi tisa kuwe na viwanda vingapi?
Mwezi uliopita PM aliweka jiwe la msingi la kiwanda kikubwa cha nondo kibaha,unataka nikuambie kingine kinachojengwa?
Hata miaka 2 ikikatika bado mtasema muda hautoshi.Hamtakosa visingizio.
 
Back
Top Bottom