OPERATION TOKOMEZA: Kuwatosa Mawaziri tu haitoshi, kamati za usalama za wilaya nazo ziwajibishwe

chambulilo

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
217
38
Binafsi naamini kuwatosa Mawaziri peke yao katika sakata hili la uonevu kwa wananchi kupitia operesheni tokemeza haitosho. Kamati za usalama zote za Wilaya ambazo maovu haya yalitokea nazo ziwajibishwe kwa uovu huu
Naomba kuwasilisha.
 
Si kamati za Ulinzi na Usalama tu za mikoa na wilaya ambako ushenzi,uhuni na upumbavu huu umefanyikia bali ni pamoja na watendaji wote walio chini ya wizara hizi za kisekta ambako hawa mawaziri husika wameamua kutema asali na maziwa...unga na vyeo vyao!!

Hebu chukulia mfano kama Waziri wa mambo ya ndani Dr Nchimbi na Waziri wa Ulinzi na usalama Bw. Vuai Nahodha wameondoka ambao kiukweli hawa ndiyo key figures wa sakata lote hili kwani polisi na wanajeshi wako chini yao na wao ndiyo waliosimamia unyanyasi na utesaji wa raia kwa kushindwa kuona kwa macho mapana iwapo walio chini yao wanatekeleza hicho kilichopewa jina OTU na OKOA TEMBO kwa kuzingatia taratibu,sheria na Katiba ya nchi hii.

Chini ya hawa jamaa kuna Mkuu wa Mjeshi, Mkuu wa Jeshi la Polisi,Makamanda wa polisi wa mikoa na wilaya,Wakuu wa Mikoa na Wilaya na ambao sasa nafikiri ndio kamati hizi za ulinzi na usalama ziko chini yao. Swali ni kuwa hawa bado wanafanya nini kuachia ngazi iwapo mabosi wao (Mawaziri) wameachia ngazi??? Haiingii akilini eti eeh?......Mimi nasema si tu hawa jamaa wafukuzwe kazi mara moja bali washtakiwe kwa uhalifu wa kibinadamu!!...Ni lazima sasa ifike wakati watu wanaopewa nafasi ya kuutumikia umma wajue kutenda na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria za nchi ambayo ni KATIBA!!

Hebutujaribu kufikiri kidogo, watu askari chini ya RPC au OCD wanapewa jukumu la kwenda kuzuia uhalifu flani,sheria zinazowaongoza kufanya hivyo zipo wanazo vichwani mwao na mikononi mwao na wamefundishwa hata kabla hawajapewa jukumu/kazi hiyo wanayolipwa nayo mshahara ktk vyuo walikosomea. Wanakamata watu wanaowadhania ni wahalifu badala ya kufuata taratibu za kisheria kuwafungulia mashtaka wanaanza kuwatesa na wengine kuwaua!!

Hivi inakuwaje mtu mzima ktk nchi huru analazimishwa kufanya mapenzi(ngono) mbele ya watoto wake eti tu anatuhumiwa kwa hili au lile? Inakuwaje mtu alazimishwe eti kufanya ngono na mti? Ili iweje?..... Hivi hawa watu askari wetu na viongozi wao waliokuwa wanasimamia zoezi hili (tunafahamu ni baadhi tu,si wote) walikuwa na akili timamu au walikuwa wamebugia viroba na value ktk kutekeleza majukumu yao nyeti waliyopewa?

Hebu,chukulia mfano wa diwani yule wa Sakasaka huko MEATU mkoa wa Shinyanga(Simiyu?) aliyeteswa na askari hawa wehu mbele ya wananchi wake kwa kuning'nizwa kichwa chini ------ juu kama mbuzi anayechunwa aliwe nyama choma. Hivi kisa ni nini? Si walishakamata kwa kumtuhumu kama JANGILI? So what was the next step? Torture or to be taken to the court?......Hii mambo tunaisikia DRC tu kwa ma M23 na kule Rwanda enzi za vita ya wenyewe kwa wenyewe hata kuletekeza Genocide na si katika Tanzania yetu hii ambayo watawala wa CCM wanatuaminisha kila siku kwamba ni KISIWA cha AMANI!!....Ni wazi haya ya Meatu kule Sakasaka na huyu diwani yamefanyika chini ya OCD na DC na RPC na RC wa eneo husika na matokeo yake watu wasio husika kina Hamisi Kagasheki,David Mathayo, Emmanueli Nchimbi na Vuai Nahodha wamepoteza kazi zao kwa ushenzi na uhuni wa watedaji wa chini!!....Wanafanya nini hawa mpaka sasa

Ndugu yako nakuunga mkono kabisa ktk hoja yako hii. Binafsi nimeumia sana na hakika tulikuwa tunasikia tu watu wakiilalamikia hii operesheni huku watawala wakiwa wameziba masikio wakiwa wamewaamini sana waliowatuma kwenda kuteleza zoezi hili kwa vitendo. Wakawabeza waliokuwa wanawaambia kuwa mambo hayako sawa pamoja na kuwa leno la operesheni kuwa zuri kabisa. Ni wakati wa viongozi wetu wa magogoni na wizara mbalimbali kufuatilia kila kitu kinacholetwa katika meza zao kama taarifa kwa wao wenyewe kwenda field. Waige utendaji wa Raisi mwasisi wa taifa hili Baba wa taifa Hayati Mwl J.K.Nyerere!.

Kwa maoni yangu, tutabadilisha sana sura za mawaziri iwapo MFUMO wa uendeshaji wa mambo yetu ktk nchi yetu hautabadilika. Hebu cheki waziri kama David Mathayo au Kagasheki katika hili ni kama wamesombwa tu na mfumo. Mathayo amelalamika sana wakati anajibu hoja za wabunge kwa sababu yeye askari wauaji na watesaji hawako chini yake, eti tu ni kwa sbb ameruhusu ng'ombe (mifugo) wafe na pia hakuweka utaratibu wa wafugaji kulisha mifugo yao kana kwamba yeye anahusika na upangaji wa maeneo(ardhi). Pia alisema huwa hapewi pesa za bajeti ktk wizara yake sawasawa na maombi yake. Hata hizo kidogo ambazo huwa anaidhinishiwa mpaka mwaka wa fedha unaisha hata nusu tu huwa haziji!!
 
Back
Top Bottom