Operation M4C: Moto kuwashwa Kesho Vijibweni Kigamboni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Operation M4C: Moto kuwashwa Kesho Vijibweni Kigamboni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Maranya, Sep 15, 2012.

 1. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Salam wadau,
  Kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam hasa pande za Kigamboni na maeneo ya jirani, kesho kutakuwa na mkutano wa hadhara utakaofanyika Vijibweni na kuhutubiwa na makamanda kadhaa kutoka Makao Makuu pamoja na majimbo jirani na Kigamboni.

  Pamoja na shughuli za kuimarisha Chama lakini pia wananchi watapata fursa ya kuzungumza na viongozi wetu juu ya masuala mbalimbali ya kijamii yanayowasibu yanayohitaji msukumo wa kipekee ili kufanikisha utekelezaji wake. Bila shaka suala la malipo kwa wananchi wanaotakiwa kuhama kupisha mji mpya wa kigamboni na wale wanaotakiwa kuhama kupisha upanuzi wa bandari, ambao kwa bahati mbaya serikali imeshindwa kuwalipa stahiki zao ili wahame yatakuwa ni mojawapo ya mambo yatakayojitokeza, kwani kwa takribani miaka minne wananchi wale wameshindwa kufanya shughuli yoyote ya kimaendeleo wakisubiri kulipwa stahili zao.

  Shughuli itaanza saa nane kamili mchana.
   
 2. eumb

  eumb Senior Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tutakuwepo, hilo pick-up tumeliona linamwaga matangazo, nawashauri viongozi yule kijana aliyeshindwa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi Wa udiwani na Selemani Mathew, kamwe wasimuache njia, his very very potential for CDM!!!
   
 3. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,246
  Likes Received: 3,812
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu, karibuni sana kwetu M4C,

  Ni viongozi gani (kwa majina) watakuwepo kesho?
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mwita Waitara na Ally Chitanda ni confirmed.
  Halima Mdee bado kuconfirm (ana ratiba tight kidogo huko jimboni kwake). Na mimi mwenyewe nitakuwepo...!!!
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kamanda yuko pamoja sana na wanakigamboni na hata mkutano huu ameshiriki kwa kiwango kikubwa sana kuufanikisha.
   
 6. Sordo

  Sordo JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Vipi polisi CCM wamewapa kibali au tujiandae na kesho kusikia mauaji mengine?
   
 7. MR. ABLE

  MR. ABLE JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,476
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mshitueni yule gamba wa kawe apeleke malalamiko yake, aache kumlalamikia mdee.
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wameshapewa notice ya mkutano na wamesema wako tayari kutupa ulinzi. Kwahiyo amani iko tele.
   
 9. c

  chama JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kamanda Mwita kila la heri una uhakika kibali umepata? Hatutaki kusikia maafa yanayoweza kuepukika

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 10. k

  kisimani JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 553
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Safi sana kila la kheri, samahani jamani najua hapa sio sehemu yake, kama kuna mtu ame-copy list ya watu walioweka fedha nje ya nchi (uswiss) naomba ani PM, nilikuwa nimelala nikapitiwa. Please please....
   
 11. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Msingi wa maisha ni kufanya kazi, kuepuka siasa za kukata tamaa na kusonga mbele, kushindwa kwangu mimi leo ni changamoto, kwangu mimi nitajitahidi kutengeneza njia kwa ajae asipate ugumu kama nilioupata ktk uchaguzi ule, karibuni kigamboni watz wenzangu. M4C daima
   
 12. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kamanda unachekesha sana, naomba mchango wako wa one bag of cement nimalizie ofis ya kata, M4C Daima
   
 13. A

  Aristides Pastory JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila la heri MAKAMANDA...
  Msalimieni Kamanda MAGERE....
   
 14. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Magere atakuwepo, karibu na wewe kamanda
   
 15. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Kamanda Mwita Maranya,pia msisahau kuzungumzia swala la mafisadi ku-hold maekari maelfu kwa maelfu bila kuendeleza wanaacha mapori tu mfano wa watu wanaocha mapori ni akbaru,mzee chacha(kaanza kuchoma moto wiki iliyopita),Hussein Mwinyi etc tunaomba mlipeleke hili kwa mama tibaijuka hawa watu ndio wanaorudisha nyuma maendeleo maeneo wanayaacha mapori tu bila kuyaendeleza kama hawayaitaji wakate viwanja vyo robo heka wayauze kwa wananchi.
   
 16. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  tunaomba more evidance
   
 17. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mambo yameshika kasi.
  Sasa Kamanda Isaya Charles aliyegombea udiwani katika uchaguzi mdogo wa vijibweni anatoa neno la shukrani kwa wananchi, kwa kura walizompigia.
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Isaya; Amemuonya waziri magufuli aache ubabe katika mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni. Wananchi watakaohama kupisha ujenzi wa daraja ni lazima walipwe haki zao kikamilifu bila kufanya ujanja ujanja wa kuwadhulumu au kuwapunja.
   
 19. M

  Molemo JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Tunashukuru sana Mwita endelea kutupa updates! Ni viongozi gani wamehudhuria?
   
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  Sep 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kamanda Stephano mwanasheria kitaaluma ametoa salamu za peoples power kwa askari polisi wanaolala kwenye vijumba vya hovyo na visivyo na thamani lakini wanakubali kutumiwa na ccm kuwapiga raia wasio na hatia risasi za moto na kuwalipua mabomu na hatimaye kuwaua!
   
Loading...