Drone Camera
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 14,007
- 13,799
Mheshimiwa Rais pole na majukumu,
Kwanza nikupongeze kwa kazi kubwa unayoifanya ya kuliletea heshima taifa letu kwa kufanya mambo makubwa mbalimbali katika kila kona ya nchi yetu.
Tumeona juhudi zako katika nyanja mbalimbali kama uboreshwaji wa miundombinu, uboreshwaji wa huduma za afya,maboresho katika sekta ya elimu na mengine mengi japo changamoto za hapa na pale haziwezi kukosa.
Nikienda kwenye lengo kuu; Watanzania wengi tunashuhudia kinachoendelea nchini Angola chini ya serikali yake ya sasa. Kuna operation kali kwa mafisadi wakubwa wale tulioamini si rahisi kuguswa.
Tumeshuhudia familia ya Rais mstaafu Dos Santos ikiwa matatani hadi kupelekea baadhi yao kukimbia nchi na kutorokea Ulaya.
Hii leo akaunti za bidada tajiri zaidi Afrika, Isabel Dos Santos zimeshikiliwa na Serikali kwa ajili ya uchunguzi. Hii inaonesha hatua kubwa sana kwa jirani zetu wa SADC katika kupambana na ufisadi.
Mheshimiwa Rais natambua na kuheshimu juhudi zako katika kupambana na hili janga, lakini naamini bado hatujafikia ile level nyeti iliyofikiwa na hao majirani zetu.
Naamini kuna mabovu mengi yalifanywa na Serikali zilizopita ambapo impact yake tunakuja kuiona katika awamu hii ambapo baadhi yamepelekea Serikali yako kuingia matatani.
Mheshimiwa naomba muhula unaofuata uguse na huko. Naamini wapo wabaya zaidi ya hao uliowatia matatani bado wanadunda.
Wamesababisha hasara kubwa kwa taifa hadi kupelekea kuchukiwa kwa chama chako. Nina hakika ukifanya hilo tutakuwa Tanzania mpya zaidi.
Kwa leo naishia hapo.
Ndimi raia wako muaminifu,
Rob.