Open university ni chuo kigumu kwelii kwa elimu hapana

Umenifanya nijione mimi kichwa,ninja,komando mpambanaji nimesoma hapo shahada ya kwanza na ya pili na nina mpango wakurudi tena kuchukua shahada nyingine
OUT discipline is the key hautakumbushwa kusoma unless otherwise utaahirisha miaka mpaka ukunye
 
Nimesoma vyuo tofauti lakini sijawahi kuona chuo kigumu ndugu zanguni Kama open university..........

Yaani nimeshidwa kuamini baada ya kujiunga chuo nimeambiwa hakuna kuingia darasani , Hakuna lecture, Hakuna walimu, wanafunzi hamjuani, material unatafuta mwenyewe wao wanakupa mwongozo, wewe unasubilia mitihani tuu basiii

kwa elimu hiii hapana kabisaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
KABLA HUJASOMA HAPO ULIPASWA KUJIHAKIKISHIA KUWA WEWE NI FAST LEARNER?UNAWEZA KUSOMA AU KUJIFUNZA BILA MSAADA KWA 75%? UMEWAHI KUSOMA SHORT COURSE YOYOTE ILE ONLINE UKAPATA SCORE MORE THAN 60%?

UKIWA BELOW HIZO CRIERIA, HUNA SIFA MZEE BABA! UTAPATA TABU SANA KUTOBOA, UTAPATA CARRY OVER NA SUPP ZA KUTOSHA BAADA YA KUSOMA 3 YEARS UTASOMA 6,5 AU 4 AU 8YRS.


*NILISHANGAA KUMKUTA MZEE UNASOMA OPEN HATA KUJISAJILI MTANDAONI HAJUI!*

PAMBANA TU BRO UTATOKA, ILA KAMA UMEOA MWAMBIE MKEO HALI HALISI ILIVYO TU MAANA NI TAAABU KWELIKWELI!

NB: NACHUKIA KUINGIA DARASANI AISEE MPAKA BASI
 
kwa jinsi hali ya ajira ilivyo, waajiri wengi wanatakiwa mtu mwenye cheti cha hapo apewe ajira, kwa jinsi hal ya chuo ilivyo
 
Shule sio kwa kila mtu. Kuna vitu vingi vya kufanya zaidi ya shule. Ni jambo la kuelewa tu unafaa au unaweza kuonyesha wapi uwezo wako.

Binafsi napenda kujisomea mwenyewe, tokea sekondari mie niambie topic gani, ntaenda kutafuta vitabu na kuhakikisha naelewa ipasavyo.
 
Nikupe hongera kwa kutambua elimu itolewayo hapo OUT.
Kimsingi elimu sio ngumu, kwakuwa haina utofauti na vyuo vingine katika programs zitolewazo hapo chuoni. Pengine ugumu unao semea wewe ni namna ya uwasilishwaji na upokeaji materials kwa mwanafunzi ambao haujazoeleka kwa wanafunzi wengi hapa tanzania.

OUT inamshape mwanafunzi kuwa na bidii binafsi za kujitafutia na kujisomea materials japo sehemu kubwa ya materials utaipata katika account yako ya Moodle. hali hii nitofauti kwa wanafunzi waliyo katika vyuo vingine ambao ni "full time students" ambao hutegemea sehemu kubwa kuingia kwa mwalimu darasani kisha kupokea moja kwa moja mafunzo kupitia ubaoni, au "face to face learning" ambapo mwanafunzi hupata nafasi ya moja kwa moja kuuliza swali na kujibiwa pale anapokutana na shida ya topic inayo mtatiza.

OUT wana mjenga mwanafunzi kuwa na spirit ya kujitafutia na kujisomea kwa juhudi zake mwenyewe, kitu ambacho ni tofauti na vyuo vingine, na hii ndio inapelekea chuo kuonekana kigumu au masomo kuonekana magumu.

Nini kifanyike kuepuka hili.
1. Kuwa na muda wa kutosha kufanya rejea ya masomo mbali mbali katika course yako.
2. Hakikisha masomo yanayojumuisha hesabu (calculations) unayafanyia rejea ya mara kwa mara ili kuepuka kusahau
3. Ungana na wanafunzi wenzako mnaosoma course moja kufanya majadiliano (discussions)
4. Kama unauwezo kidogo, hakikisha unafanya rejea ya lectures (Mafundisho) kupitia video zilizoko Youtube, (Za kiingereza na nyingi ni wahindi ndio wamekuwa na tabia ya kuweka videos za masomo mbalimbali).
5. Usione aibu kuuliza au kumfuata mwalimu wa somo husika hata kwa njia ya simu ili akufafanulie pale unaposhindwa kuelew.
6. Hakikisha unapitia maswali mengi kadri inavyowezekana ili uwe na uzoefu wa kujibu maswali mbalimbali hii inajumuisha ( maswali ya past papers na maswali kutoka katika vitabu mbalimbali)
7. Jiamini kuwa unaweza kujisomea mwenyewe na "unaweza" toa ile mentality kuwa bila mwalimu huwezi kujisomea.

OUT wamekuwa na mtazamo wa kuangalia mwanafunzi ameelewa nini, na sio kukariri kile kilichoandikwa na mwalimu. Napenda kukuambia kuwa mitihani ya OUT haivuji kirahisi kwakuwa
a. Msimamizi wa kituo husika hupewa password ya ku access mithani na kuprint mtihani huo dakika 5 kabla ya muda wa kuanza mtihani. (password hupewa toka ofisi ya Mkurugenzi wa masuala ya mitihani wa chuo makao makuu.
b.Afisa usalama wa taifa husimamia shughuli hiyo mpaka mtihani unapomalizika.
c. Uwezekano wa kufuja kwa mtihani ni mdogo na hivyo akili yako na maandalizi yako ndiyo yatakusaidia.
d. Swali linapokushinda kabisa tafadhari andika kile unachoelwa kulingana na swali hilo (usiache nafasi wazi).


Mwisho OUT wamejipambanua kumfundisha mwanafunzi namna ya kujisomea, kitu ambacho kinamsadia mwanafunzi katika kufanya tafiti mbalimbali bila kusimamiwa, hali hii imekuwa ikifanywa sana na mataifa yaliyoendelea. Pia hali hii humfanya mwanafunzi apende kujisomea vitabu mbalimbali kwakuwa amejengwa kujitafutia. Ndio mana utaona wenzetu "wazungu" hupenda kujisomea vitabu mbalimbali, hii ni kwakuwa wamezoea kujisomea tangu wakiwa wadogo kwa kufundishwa kujisomea .


Asante.
 
Muajiri gani anamkataa Candidate bila kumfanyia usaili (Interview)?and this is ridiculous and shame to them!!
Mim nafkiri sababu ya kuwakataa before interview ni kwamba, elimu ya chuo mara nyingi ndiyo tunayoenda kuitumia kazini. Sasa hawa jamaa wanawaza kwamba yan mtu alijifundisha yey mwenyewe na hakupata mtu anayeelewa vile vitu ili amuulize maswali sehemu ambazo hajazielewa, na wkati mwingine alifundishwa na mwalimu ambaye amebobea na anayafahamu hayo mambo. Ndipo wana conclude kwa aliyesoma openi ankuwa hajaipata elimu sawasawa kuliko aliyesoma darasani na mwalimu.
Just mtazamo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mim nafkiri sababu ya kuwakataa before interview ni kwamba, elimu ya chuo mara nyingi ndiyo tunayoenda kuitumia kazini. Sasa hawa jamaa wanawaza kwamba yan mtu alijifundisha yey mwenyewe na hakupata mtu anayeelewa vile vitu ili amuulize maswali sehemu ambazo hajazielewa, na wkati mwingine alifundishwa na mwalimu ambaye amebobea na anayafahamu hayo mambo. Ndipo wana conclude kwa aliyesoma openi ankuwa hajaipata elimu sawasawa kuliko aliyesoma darasani na mwalimu.
Just mtazamo

Sent using Jamii Forums mobile app
Anachokiongea darasa mwalimu ndio hiko hiko kilichopo kwenye notes utakazopewa sema labda mwalimu anakufafanulia zaidi

Open inawafaa watu wanaoweza kuelewa vitu kwa haraka sana yaani Fast learners pia Open inakufanya mwanafunzi uwe mdadisi zaidi zaidi pindi unapokuwa na maswali kuhusu mada ulijifunza unaweza kuko contact na lecture wa somo lako through Moodle platform pia kwa msaada wa otheronline resources such as web

Kimsingi Open Student wakakuwa well informed na kozi anazosoma sababu ya kuwasharp kuserch material kumcompare and contract facts written

Na pia Mfumo wa usahihishaji unampima MTU kwanjinsi alivyo elewa mada sio copy and paste from notes hahahahah hio inafanyika vyuo vingine .

Nakipenda hiko chuo coz kinatoa nafasi watu pia wawe bize na shughuli zingine za uzalishaji Mali at same time wqnanoa ubongo wako

Narudi Open kupiga bachelor ingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom