Open university na ada za walala hoi

Stephano

Member
Dec 30, 2008
27
4
wadau kuna taarifa toka kwa wadau ambao wanataka kujiendeleza katika chuo chetu kikuu huria cha Tanzania kwa madarasa ya jioni kuwa mkuu wa chuo hicho ametoa maelekezo kuwa wanafunzi wanaoanza kozi ya masters ambao hawataweza kulipa ada yote ya mwaka wasiruhusiwe kuingia madarasani. kuna yoyote anaelijua hilo?

kuna mapendekezo ya chuo kingine ambacho walalahoi ambao wanafamilia na wanajisomesha wanaweza kwenda ambapo watakubaliwa kulipa kwa awamu?
 
ndugu stephano sasa hivi karibia vyuo vyote wanataka pesa, nilienda kufanya registration pale UDSM juzi nikakuta hawakubali ada nusu wanataka ya mwaka mzima,uzuri wa pale unaandika barua kwamba utalipa kiasi fulani cha pesa then hizo zilizosalia utamalizia lini? then ukisha jicommit utaruhusiwa kufanya registration. Hakuna kwenye uafadhali sasa hivi ni kulipa tu kwa sababu elimu ni kwa ajili yako na pia watu hawalalamiki wakichangia vitu kama harusi, elimu ni yako na itakusaidia wewe, na pia nafikiri mpaka ukaamua kwenda kwenye masters ina maana ulijipanga na suio kukurupuka, so ilibidi jamaa waweke kiakiba kidogo kidogo, leo hii wasingelalamika
 
Gudboy mi pia nilikuwa na wazo kama lako na nikajenga hoja kuwa ukiandika barua ya kujicommit kuwa utalipa hakuna mtu ataekataa na hiyo ni kwa vyuo vyote duniani, wadau wakasema barua hizo hazikubaliki open university ya Tanzania.
 
ukiona umekataliwa sehemu, tafuta sehemu nyingine. inategemea jamaa wenyewe wako wapi, kama wako mikoani inabidi walipe tu, kama haiwezekani kabisa (hata kukopa!) WAPIGE CHINI.
 
Me nilishawahi kuomba masters (MBA) ya OUT nikafanikiwa kufanya registration na malipo ya awali! Lakini bahati mbaya nilipata misukosuko katika huo mwaka wa kuanza ! Nikaandika barua ya kuomba kuahirisha mwaka wangu wa masomo ili mwaka unaofuatia ndio nianze! Lakini cha kunisikitisha sikuweza kujibiwa ombi langu....Kwenda pale chuoni barua yangu hamna..... hela zangu almost 3 HT zikapotelea huko... hapo ndo mpaka leo najiuliza ndio mbinu wanayotumia kujipatia fedha au system yao ipo shaghalabaghala kwa kweli nimekosa imani kabisa na OUT
 
wadau kuna taarifa toka kwa wadau ambao wanataka kujiendeleza katika chuo chetu kikuu huria cha Tanzania kwa madarasa ya jioni kuwa mkuu wa chuo hicho ametoa maelekezo kuwa wanafunzi wanaoanza kozi ya masters ambao hawataweza kulipa ada yote ya mwaka wasiruhusiwe kuingia madarasani. kuna yoyote anaelijua hilo?

hamna mkuu, bila 1.5 ada ya mwaka hakuna registration
 
Back
Top Bottom