Open University Kunani Pale?

Msongoru

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
306
24
Naandika haya kwa masikitiko makubwa. Sijui nimwandikie John Malecela au nimwandikie Mwete! Hali inayoendelea katika chuo hicho sio mswano kabisa. Assignment kupotea na maitihani kutoonekana imekuwa ni jambo la kawaida.

Mitihani yenyewe kusahihihshwa inachukua muda mrefu kupita kawaida. Hali hiyo imepelea hivi majuzi wakatangaza kusogeza mwaka mzima kwa wanafunzi wa kozi ya msingi(Foundation Course). Yaani bila hata woga wakatangaza kuwa kutokana na 'uvivu' wa kusahihisha basi watajoin degree mwaka 2009! hii ni kinyume na prospectors yao, na sioni kama wanalielewa hilo.

Mwaka huu wameongeza malipo kwa kitu walichokiita ada ya mtihani ambapo hapo mwanzoni hakikwepo. Kwa kweli kuna hali ya kusikitisha sana kwani inaoneka ni ufisadi tu na hakuna nia ya dhati ya kuwapatia elimu watanzania.

Mpaka naandika hapa sijajua vizuri hadhi na wajibu wa mkuu wa chuo mheshimiwa Malecela. Lakini kunakiwa kufanyike kitu fulani, la sivyo hali itazidi kuwa mbaya. Hela wanazopata ni nyingi sana na sijui zinavyotumika kwa sababu hakuna service wanayotoa.
 
Last edited by a moderator:
Du Afadhali Umesema Kwani Hali Ni Mbaya Pale Ni Kupotezeana Muda Bwette Binafsi Kichwa Lakini Pale Naona Panamshinda.
 
Sasa PEZZO, unafikiri tunaweza kufanya nini? Hali ni mbaya kuliko maelezo. Tatizo ni nini hasa?
 
Sasa PEZZO, unafikiri tunaweza kufanya nini? Hali ni mbaya kuliko maelezo. Tatizo ni nini hasa?

Tunahitaji kupata information zaidi, wenye nazo tafadhali changieni. Any Open Univ. scholars in the house?
Hii issue nimeona ikilalamikiwa mara kadhaa..
 
Unapo Ongea Nao Wanakituza Chuo Kwamba Ni Vyuo Kama Vingine Lakini Kuna Kadhalau Wanacho Wako Pale Kukomba Taito Ili Kupandisha Cv Zao Lakini Kazi Hakuna,nilitegemea Akina Shemweta Wangeleta Chachu Mpya Lakini Wapi,walimu Wengi Wa Nje Wanakidai Chuo Sasa Hata Assingment Zao Hawajaleta Chuo Hawataki Tena Kuwa Sehemu Ya Chuo Cha Ajabu Siyo Chuo Akina Pesa,kuna Pesa Za Kutosha But Planning Is Poor;umeniuliza Tufanyeje,bado Hatuwezi Kuorganise Out Door Studies Kama Out ,je Wafahamu Ngos Kubwa Kubwa Hapo Zina Ongozwa Na Wakenya Nenda Pathfinder Na Nyingine Nyingi ,so Tuwaite Wenzetu Watuzaide Dr Tole Bwete Ina Tosha Cv Ya Vc Imemleesha Chalinayo Hana Anachofanya Aende Mbeya Milimani Akababaishe Ubunge,katengeneza Cv Inatosha Tuite Wakenya ,wafanye Kazi, Wewe Mipeza Yote Ya Out Hana Plan, Tatizo Alilo Nalo Ni Family, Hawezi Kutulia Wakati Wife Wa Kichaga Anampeleka Puta Ni Mtu Wa Mitungi Tu Sasa.
 
Kinachotokea ni kwamba, wanafunzi wanafanya assignment, wakirejesha mwalimu aliyesimamia asipolipwa basi anachana assignment. Hii ilishatokea hata kwa mithani, ilichanwa na bwana mmoja aliynyimwa hela yake waqnafunzi wakakadiriwa matokeo!!! yaani hakuna quality education kama motto wao ulivyo bali ni ubabaishaji tu.

Kwa sasa ndicho chuo chenye wanafunzi wengi kuliko vyote Africa Mashariki na kati! Lakini ukiangalia mambo yalivyo utashangaa! Huwezi kuamini eti watu wanapumzishwa kukaa nyumbani mwaka mzima kisa wasahihishaji hawapo!!!! Mwaka mmoja inakuwa miwili kisa ni wasahihishaji kuchelewa!! AJABU KWELI
 
Kuna Masomo Ambayo Nilicha Apo Yakiboreshwa Hadi Leo Hayana Vitabu Yani Wapo Wanajivutavuta Tu,ebu Amkeni Wekeza Hizo Pesa Kwa Miladi Ya Maana Wewe Cha Pombe,du Taifa Kama Limelaaniwa Kila Kitu Ovyo Watu Ni Title Crezzy Hawa Derive Ma Sabstance Wawape Wakenya Waendeshe Kwa Muda Hilo Chuo Mtaona,tunataka Mtu Shupavu Siyo Bishow, Mzee Mmari Aliweka Mafaundation Ya Nguvu Wao Wamekalia Talk Show Kwenye Luninga,
 
Mpaka naandika hapa sijajua vizuri hadhi na wajibu wa mkuu wa chuo mheshimiwa Malecela. Lakini kunakiwa kufanyike kitu fulani, la sivyo hali itazidi kuwa mbaya. Hela wanazopata ni nyingi sana na sijui zinavyotumika kwa sababu hakuna service wanayotoa.

Sina kumbukumbu ya mzee Malecela kufanya kitu cha maana katika siku za karibuni, ukianzia pale jitihada zake za mwanzo za kuwania Urais zilopovurugwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere. Kwa hiyo hapo ni kama wamempa mahali pa kupumzikia tu. bahati mbaya hapo panahitaji wachapa kazi, sio wachapa usingizi. Tatizo la mweshimiwa Mbwete yeye ni mjasiriamali na mbabaishaji mzuri tu, muda wote anawaza kamradi haka au kale. Yeye sio mtu wa mavisheni na mastrateji. ukimdai hayo utakuwa unamwonea. yeye anatakiwa kuwa "Director of Projects" kitu kama hicho kama ni lazima umweke pale chuoni, basi mpe posti kama hiyo lakini sio kumkabidhi usukani wa lichuo kama hilo. sasa ukiunganisha na mzee wa kupumzika Malecela, sidhani kama utakuwa na Chuo kikuu, hata kama ni "OPEN".

lakini pamoja na hayo sidhani kama ufumbuzi ni kuwapa "WAKENYA". hili ni jipu na inabidi lipasuliwe. wapo watanzania wengi tu wanaoweza kuchapa kazi, kama inavyojulikana mzee Mmari alivyokuwa pale. dawa ni kumpa presha JK afanye mabadiliko yanayotakiwa pale OUT (Open University of Tanzania) ili kieleweke. namna nyingine ni kuendeleza ubabaishaji tu. MBWETE OUT!!
 
......wana Ndugu Pale Wala Hapashiki Ni Kumwachia Mungu......

Hamna Tatizo Lolote Zaidi Ya Pesa:::::::::::mbwete Na Yeye Kapewa Pale Ndio Anatakla Nkumake Kama Manji::kazi Kwelikweli!!!!!!!!!!!!!!!
Walimu Ukiwaluliza Wanakujibu Kabisa Hawajatulipa Kabisa Na Sahauuni Kupata Matokeo Yenu Angalia Kuna Watu Wamefanya Mitihani 15 Matokeo Ya Juzi Wametoa Wamefanya Masomo 5...utawafanya Nini Hawa Zaidi Ya Kuwaweka Maombini......mungu Awarehemu..ila Mlio Pale Kazi Mnayo Mkapata Digiriiiiiiiiiiiiiii Kaizkwelikweli!!!!!!!!!!!
Ciao
 
Nilifikiri Mbwete analinda CV yake kumbe anaiunguza tu. Lakini hata hivyo chuo chochote kikiwa na walimu wengi wa kutoka nje lazima kila kitu kiwe hovyo. Chuo ni watendaji. halafu sidhani kama kuna mtu yeyote anayeweza kuchana makaratasi ya wanafunzi eti kanyimwa pesa hili ni kosa la jinai nafikiri kwa kufanya hivi na chuo kikakaa kimya hii ni hatari sana.

Kwa maana nyingine nafikiri OUT ni sehemu ya kupata vyeti na si chuo. Hakuna chuo mtu anaweza kufanya hivi, nafikiri hata Mbwete mwenyewe amekaa ktk vyuo anajua taratibu za kulinda heshima ya chuo.

Mtihani wowote ktk chuo ni sawa na PESA BoT. Hii ndo taaluma yenyewe.
 
Bado Natetea Utendaji Wa Wenzetu Wa Kenya Ndiyo Tunao Watanzania Wengi Tu, Ambao Wanasherekea Vyeti Wala Si Utendaji,sishangai Elimu Yetu Haitujengi Kutenda Kwa Kuwajibika Bali Huwa Tunaandaliwa Kijibu Mitihani,mbete Ni Dr Asiye Na Strategi Mpe Paper Utaumia Mpejukmu Kama Hilo Pale Shida Si Pesa Kuna Pesa,shida Hakuna Vision Ni Tatizo Tulilo Nalo Kila Sehemu,si Jk, Si Pinda, Just Mention, Pale Tuweke Wakenya Uraisi Tuwape Wachina.
 
ni kweli pale out uongozi ni issue. hata hivyo kazi ipo pale. wazee waliostaaf watafanyaje mambo makubwa? chuo kina wanafunzi wengi mno. ingetakiwa kuwa na manpower ya kutosha tena fresh blood

kwa wanafunzi nao. waliosoma pale wanajua. wakiona mtihani mgumu ama wanaandika majina na namba za uongo. au wanaurudia mtihani mwakani. sasa matokeo yakitoka anakuambia siyo hayo. basi ni vurugu tu.

pia hii technologia aliyoingiza mbwette inaweza kusaidia. kwa sasa wanafunzi wote wanaingia kwenye database (internet database) hivyo popote walipo wanaweza kuona matokeo ya mitihani yao. na wanaweza kuwasiliana na utawala kwa mitihani yenye matatizo. hivyo mwishowe wanafunzi wataweza kumlink staff mzembe na akishughulikiwa tatizo litapungua.
 
Wawape Wakenya Waendeshe Kwa Muda Hilo Chuo Mtaona,tunataka Mtu Shupavu Siyo Bishow, Mzee Mmari Aliweka Mafaundation Ya Nguvu Wao Wamekalia Talk Show Kwenye Luninga,

mh! mwisho utasema wapewe wa-india. kuna kitabu kinaitwa Capitalist Nigger - pengine ni muhimu kwako kukisoma
 
Bado Natetea Utendaji Wa Wenzetu Wa Kenya Ndiyo Tunao Watanzania Wengi Tu, Ambao Wanasherekea Vyeti Wala Si Utendaji,sishangai Elimu Yetu Haitujengi Kutenda Kwa Kuwajibika Bali Huwa Tunaandaliwa Kijibu Mitihani,... Pale Tuweke Wakenya Uraisi Tuwape Wachina.

Naelewa uchungu wako, kwamba una hamu kubwa tusonge mbele na umetazama huku na kule, unaona ubabaishaji tu hamna la maana. lakini ndugu yangu nataka nikuhakikishie kwamba hao hao watanzania unaowabeza, huko nje wakipewa majukumu wanafanya la maana. hata hapa kwetu, kama ukimpa mTz majukumu na kumpa mshahara mzuri na kumfanyia close monitoring, atafanya vizuri tu. tunachotaka ni kujenga misingi ya kuchapa kazi, kama ilivyokuwa zamani.

huu ubabaishaji ni ugonjwa tu unaoweza kutibiwa ingawa matibabu yake yanachukua muda mrefu. lakini ni afadhali kuingia katika kutibu watanzania, kuliko kufanya "organ transplant" ya kuleta wakenya au wahindi au wachina. hao wenyewe wamejitibu wenyewe ndio maana umeona vinaelea ukasahau kwamba inabidi viundwe. ukiwajaza hapa utazalisha matatizo mengine maana kama ujuavyo, watahamisha kila kitu na wewe utabaki kuwa mpagazi tu.

Imarisha elimu yako hapa, watoto wapate elimu bora sio bora elimu. mtu akiboa azomewe kwa nguvu zote, mafisadi wazomewe na kukemewa, sio kupokelewa kwa mbwembwe kisa ati wametuchinjia ng'ombe na kuandaa mapilau. Watanzania tujenge tabia ya kuthamini vitu vidogo hivi vya kawaida tu kama heshima kwa jamii, kutoibia wengine, kuthamini wengine, kufanya kazi na kujituma, kutopenda vya bure. yaani ni vitu vidogo tu lakini vya muhimu sana. sasa utakuta watanzania tunamhusudu sana mtu akifanya kitu bila hata kujua pesa kapata wapi. tunathamini sana zali la mentali. watu namna hiyo wakikemewa, wakionekana hawafai katika jamii, tutakuwa tunajenga taifa la watu wanaowajibika na ambao tutapenda kuwa nao.

kwa hiyo ndugu yangu tusikate tamaa. tusikimbilie wakenya, tudeal na hawa hawa watanzania wetu mpaka kieleweke. ALUTA CONTINUA!!
 
haya ni mambo ambayo uongozi wa chuo unaonekana huwa hawafanyi tafiti kwa ajili ya kutatua matatizo ya chuo bali hufanya tafiti zile ambazo zinahusisha malipo ama vipato vikubwa siwezi amini chuo kilichoanzishwa na vision na mission kinakuwa na wakati mgumu wa kutekeleza malengo yake kulingana na wakati uliopo na kwa mtizamo endelevu mimi nitapenda kuingia ndani zaidi ya chuo ambayo bado wapo katika muundo wa kulazimisha watu kutumia vitabu hata vya kiswahili vilivyoandikwa na wanaisimu wa kiswahili kutoka Kenya sina maana ya kukataa kuwa wenzetu wa Kenya hawawezi kuandika lugha hii kwa ufasaha lakini nina maana vyombo vyetu tunavikuza vipi ???????

MIMI NAYAONA MATATIZO YAFUATAYO
1. Vitabu vinavyonunuliwa kwa gharama kubwa kutoka Nairobi university bila ya kuwa na uandishi wa kisasa na vinaendelea kununuliwa ni aheri kama ndivyo ilivyo vitolewa kuwa njia ya soft copy na wanafunzi walio wengi bado wanaweza kuprint hard copies zao kuliko kusoma poor quality text books from Nairobi university

2. kucheleweshwa ama kutokua na utaratibu mahsusi wa kusasahisha test na assignment za chuo bila ya kupoteza na kurejesha majibu kwa wakati sijui tatizo nini ?? Hivi ina maana chuo kina wanafunzi wengi kuliko wale wanaomaliza kidato cha nne na darasa la saba mbona hawa mitihani haipotei ama haiachi kusasahihishwa au chuo wanafurahia kufungua matawi mapya ya mikoa na kanda mbali mbali bila ya kuwa na rasilimali watu ya kutosha je tatizo nini ?????

3. kuna hii faculty ya FBM ingekuwa ni ruhusa yangu wangemfuta kazi dean wa faculty husika na kufunguliwa mashtaka ya ufisadi wa kisaikolojia kwa wanachuo wa faculty hii kwani huyu ni mmoja kati ya watu wanoiba wizi wa muda wa wanachuo kuacha kusoma na kupoteza muda wa kufuatilia majibu yao chuoni na haswa walio mkoani anawasababishia gharama isiyo ya msingi jamani kuwa fisadi siyo lazima uibe mali ya umma hata kuifanya system isifanye kazi ipasavyo ni ufisadi uliotukuka hivyo namwomba aungane na mafisadi wengine katika kujiuzulu na afunguliwa mashtaka ya kuiba muda wa wanachuo wote wa mwaka wa kwanza mpaka wa sita ???

jirekebishen haraka !!!!!!!
 
Wewe Mwalimu Unasikia Anafanyakazi Bot,,ttcl,,bima,,,ndc,,,jf Unatarajia Nini Kwake?????????huyu Ndie Mwalimu Wa Open
 
Kuna Chanzo Nimewasiliana Nacho Jana Wanasema Huduma Zipo Dar Tu Mikoani Hali Ni Ngumu Asgnment Hakua Vatabu Hakuna Kuna Watu Hata Fild Hawajaenda,wakugenzi Wengi Wakiulizwa Wanaonekana Hawana Majibu,waogopa Ogopa ,wanavyo Dai Ada Duuuuuuu Utafikili Umesoma Masomo Yote Wanawaludisha Nyuma Watu .
 
Pale kichwa alikuwa Prof GRV Mmari. Huyu mzee alikuwa mkuu wetu Mlimani enzi zile, alifanya mambo makubwa sana, akatolewa kwa sababu za kisiasa. Lakini alipokabidhiwa hiyo OUT aliweza kuiunda from scratch hadi ikafikia hadhi ya kupigiwa mfano.
 
Back
Top Bottom