Open University, Form six leaver itawasaidia

Kiagoh92

Senior Member
Feb 23, 2018
101
56
Wapendwa Wahitimu Kidato cha Sita 2018,

Kwa Heshima kubwa, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinawapongeza sana kwa kuhitimu masomo yenu na kufuzu vizuri kupitia matokeo ya mtihani yaliyotangazwa hivi karibuni na NECTA.

Tunapenda kuwatangazia wale waliopungukiwa sifa kidogo za kujiunga moja kwa moja na shahada za awali kuwa wanayo fursa ya kujiunga na Foundation Programu (Arts, Science na Business Studies) pekee ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Foundation Programu hufunzwa kwa mwaka mmoja wa masomo na mhitimu atafanya mitihani na akifaulu kwa ufaulu uliowekwa atapata sifa ya kujiunga na Shahada ya Kwanza katika Vyuo Vikuu.

Sifa za kujiunga na Foundation Programu kwa mhitimu wa kidato cha Sita ni:

Ufaulu wa angalau point 1.5 katika masomo mawili. Yaani ufaulu wa alama E na S katika masomo mawili ndio mwisho. Kwa maneno mengine, mhitimu yeyote aliyepata alama D na E, E na E, au D na S, au C na S, au E na S ndiye mwenye sifa ya kujiunga na Foundation Programu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Hii ni sawa na kusema kwamba, wahitimu wote wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa daraja la tatu (Division 3) point 14, 15, 16 na 17 wana sifa ya kujiunga na Foundation Programu. Mhitimu mwenye Division 4 ya point 18 pia anaweza kujiunga na Foundation Programu kama kwenye masomo mawili ana alama E na S.

Kwa ufafanuzi huu naamini mtaelewa vizuri na mtatembelea matawi ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyopo katika mikoa yote ya Tanzania Bara na katika visiwa vya Unguja na Pemba ili kujaza fomu za Maombi zinazotolewa bure. Pia, unaweza kuomba moja kwa moja kupitia tovuti yetu ya www.out.ac.tz

Kwa wale ambao wapo Dar es Salaam Chuo kipo Kinondoni Biafra na katika jengo la Elimu ya Watu Wazima karibu na Maktaba Kuu ya Taifa eneo la Posta. Pia, wanaweza kutembelea banda letu katika Maonesho ya TCU ambayo yanaanza tarehe 18-21/07/2018 katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Hapo kutafanyika maombi ya papo kwa papo. Njoo na cheti chako cha kidato cha Nne na nambari ya mtihani ya kidato cha Sita. Kama bado hujachukua cheti chako cha kidato cha Nne njoo na nambari ya mtihani inatosha.

Kumbuka pia, Foundation Programu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania inapokea wahitimu wa Diploma mbalimbali wenye ufaulu wa GPA 2.9 mpaka 2.0

Pia, inapokea wahitimu wa NTA level 5.

Karibuni nyote wenye sifa tajwa hapo juu ili muweze kujiunga na Programu hii adhimu inayotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Pekee.

Kwa mawasiliano zaidi tupigie kupitia nambari 0719017254 au 0753000102

Imetolewa na:
Dkt. Mohamed Omary Maguo
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
17/07/2018
Dar es Salaam.
 
Mkuu nieleweshe vzur kuhusu kuhitimu degree open university inachukua muda gan kuhitimu
Gharama za courses za degree
 
Kumbuka pia, Foundation Programu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania inapokea wahitimu wa Diploma mbalimbali wenye ufaulu wa GPA 2.9 mpaka 2.0

Pia, inapokea wahitimu wa NTA level 5.

Karibuni nyote wenye sifa tajwa hapo juu ili muweze kujiunga na Programu hii adhimu inayotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Pekee.

Itangazeni programu yenu ya Foundation kupitia vyombo vya habari pia. Wengi wanakumbuka kupigwa stop kwa hii program na sio kufunguliwa, hivyo ifanyieni kazi ya ziada.
 
Wapendwa Wahitimu Kidato cha Sita 2018,

Kwa Heshima kubwa, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinawapongeza sana kwa kuhitimu masomo yenu na kufuzu vizuri kupitia matokeo ya mtihani yaliyotangazwa hivi karibuni na NECTA.

Tunapenda kuwatangazia wale waliopungukiwa sifa kidogo za kujiunga moja kwa moja na shahada za awali kuwa wanayo fursa ya kujiunga na Foundation Programu (Arts, Science na Business Studies) pekee ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Foundation Programu hufunzwa kwa mwaka mmoja wa masomo na mhitimu atafanya mitihani na akifaulu kwa ufaulu uliowekwa atapata sifa ya kujiunga na Shahada ya Kwanza katika Vyuo Vikuu.

Sifa za kujiunga na Foundation Programu kwa mhitimu wa kidato cha Sita ni:

Ufaulu wa angalau point 1.5 katika masomo mawili. Yaani ufaulu wa alama E na S katika masomo mawili ndio mwisho. Kwa maneno mengine, mhitimu yeyote aliyepata alama D na E, E na E, au D na S, au C na S, au E na S ndiye mwenye sifa ya kujiunga na Foundation Programu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Hii ni sawa na kusema kwamba, wahitimu wote wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa daraja la tatu (Division 3) point 14, 15, 16 na 17 wana sifa ya kujiunga na Foundation Programu. Mhitimu mwenye Division 4 ya point 18 pia anaweza kujiunga na Foundation Programu kama kwenye masomo mawili ana alama E na S.

Kwa ufafanuzi huu naamini mtaelewa vizuri na mtatembelea matawi ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyopo katika mikoa yote ya Tanzania Bara na katika visiwa vya Unguja na Pemba ili kujaza fomu za Maombi zinazotolewa bure. Pia, unaweza kuomba moja kwa moja kupitia tovuti yetu ya www.out.ac.tz

Kwa wale ambao wapo Dar es Salaam Chuo kipo Kinondoni Biafra na katika jengo la Elimu ya Watu Wazima karibu na Maktaba Kuu ya Taifa eneo la Posta. Pia, wanaweza kutembelea banda letu katika Maonesho ya TCU ambayo yanaanza tarehe 18-21/07/2018 katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Hapo kutafanyika maombi ya papo kwa papo. Njoo na cheti chako cha kidato cha Nne na nambari ya mtihani ya kidato cha Sita. Kama bado hujachukua cheti chako cha kidato cha Nne njoo na nambari ya mtihani inatosha.

Kumbuka pia, Foundation Programu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania inapokea wahitimu wa Diploma mbalimbali wenye ufaulu wa GPA 2.9 mpaka 2.0

Pia, inapokea wahitimu wa NTA level 5.

Karibuni nyote wenye sifa tajwa hapo juu ili muweze kujiunga na Programu hii adhimu inayotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Pekee.

Kwa mawasiliano zaidi tupigie kupitia nambari 0719017254 au 0753000102

Imetolewa na:
Dkt. Mohamed Omary Maguo
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
17/07/2018
Dar es Salaam.

Tatizo hawana foundation course za engineering na health sciences programs mfano medical laboratory or medical doctor foundation course
 
Mkuu hivi ni form six lever au "leaver"? Jamani mkiwa mnatumia maneno ya Kiingereza muwe mnaangalia "spelling" zake kabla ya kupost. Mnafanya Watanzania tunachekwa na kudharauliwa sana. Mbona siku hizi ni rahisi tu, ukiona spelling zinakushinda tumia "google".
 
Huria = holela au sio kiswahili fasaha???
Mimi siyo mtaalamu sana wa Kiswahili, lakini neno "holela" likitumika hapo halitaleta maana nzuri, "huria" nadhani ndilo neno sahihi zaidi.

Hata hivyo sidhani kama "huria" na "holela" zina maana moja, haya ni maneno mawili tofauti yakimaanisha vitu viwili tofauti sana.
 
mimi napenda uliza na kwenye tcu undergraduate admissions guidebooks wataweka zile qualifications zitakazo weza tumika kwa wenye foundation courses au inakuwajeeee wajuvi?
 
Wapendwa Wahitimu Kidato cha Sita 2018,

Kwa Heshima kubwa, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinawapongeza sana kwa kuhitimu masomo yenu na kufuzu vizuri kupitia matokeo ya mtihani yaliyotangazwa hivi karibuni na NECTA.

Tunapenda kuwatangazia wale waliopungukiwa sifa kidogo za kujiunga moja kwa moja na shahada za awali kuwa wanayo fursa ya kujiunga na Foundation Programu (Arts, Science na Business Studies) pekee ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Foundation Programu hufunzwa kwa mwaka mmoja wa masomo na mhitimu atafanya mitihani na akifaulu kwa ufaulu uliowekwa atapata sifa ya kujiunga na Shahada ya Kwanza katika Vyuo Vikuu.

Sifa za kujiunga na Foundation Programu kwa mhitimu wa kidato cha Sita ni:

Ufaulu wa angalau point 1.5 katika masomo mawili. Yaani ufaulu wa alama E na S katika masomo mawili ndio mwisho. Kwa maneno mengine, mhitimu yeyote aliyepata alama D na E, E na E, au D na S, au C na S, au E na S ndiye mwenye sifa ya kujiunga na Foundation Programu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Hii ni sawa na kusema kwamba, wahitimu wote wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa daraja la tatu (Division 3) point 14, 15, 16 na 17 wana sifa ya kujiunga na Foundation Programu. Mhitimu mwenye Division 4 ya point 18 pia anaweza kujiunga na Foundation Programu kama kwenye masomo mawili ana alama E na S.

Kwa ufafanuzi huu naamini mtaelewa vizuri na mtatembelea matawi ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyopo katika mikoa yote ya Tanzania Bara na katika visiwa vya Unguja na Pemba ili kujaza fomu za Maombi zinazotolewa bure. Pia, unaweza kuomba moja kwa moja kupitia tovuti yetu ya www.out.ac.tz

Kwa wale ambao wapo Dar es Salaam Chuo kipo Kinondoni Biafra na katika jengo la Elimu ya Watu Wazima karibu na Maktaba Kuu ya Taifa eneo la Posta. Pia, wanaweza kutembelea banda letu katika Maonesho ya TCU ambayo yanaanza tarehe 18-21/07/2018 katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Hapo kutafanyika maombi ya papo kwa papo. Njoo na cheti chako cha kidato cha Nne na nambari ya mtihani ya kidato cha Sita. Kama bado hujachukua cheti chako cha kidato cha Nne njoo na nambari ya mtihani inatosha.

Kumbuka pia, Foundation Programu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania inapokea wahitimu wa Diploma mbalimbali wenye ufaulu wa GPA 2.9 mpaka 2.0

Pia, inapokea wahitimu wa NTA level 5.

Karibuni nyote wenye sifa tajwa hapo juu ili muweze kujiunga na Programu hii adhimu inayotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Pekee.

Kwa mawasiliano zaidi tupigie kupitia nambari 0719017254 au 0753000102

Imetolewa na:
Dkt. Mohamed Omary Maguo
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
17/07/2018
Dar es Salaam.
Mkuu vipi kuhusu mkopo ? Niliona sehemu bodi ya mikopo inadai wanafunzi wa open universty hawatopatiwa mkopo
 
Back
Top Bottom