Open Marriages... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Open Marriages...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MwanajamiiOne, Apr 3, 2009.

 1. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #1
  Apr 3, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Salamu kwa wote.........


  Jamani eti hizi open marriages za wenzetu wazungu je kuna uwezekano kuwa wanatekeleza ule msemo wetu wa Mapenzi ni maua popote huchanua? hata kwa mtu ambaye ameoa au kuolewa?.

  Kwa maana ya kuwa kuolewa au kuoa si mwisho wa kupenda? Je kuna ukweli katika msemo huu na kama ni ndio vipi sisi ambao hatufuati taratibu hizi za open marriages au ndoa za mikataba, tunawezasema tunaishi kinafiki kwa kupingana na hali halisi au?

  Nazungumzia hizi ndoa za "Nitakuwa mwaminifu kwako Mpaka kifo kitutenganishe"
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  hebu fafanua zaidi MJ1 maana sijaelewa vizuri.
  You mean swingers or those cohabiting without a formal marriage?
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ofcourse, kuoa na kuolewa si mwisho wa kupenda,..lakini ndoa kama (mfano) ilivyo Kufunga, iwe swaumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, au Kwaresma,...au funga yeyote ile, lengo nia na madhumuni yake ni kujizuilia nje ya mipaka ya Nia uliyoweka.

  Kama umefunga Kwaresma, na ukaambiwa jizuilie vitu unavyovipenda, ama Nyama, Maziwa, Jibini na siagi... halafu katikati ya funga wewe ukala au kunywa hayo maana yake ushabatilisha funga yako na maana ya tendo hilo.
  Sawa sawa na waislamu akiamua kwa makusudi kula au kunywa katikati ya mchana wa funga yake ya Ramadhani...atakuwa keshafungulia!

  Ndoa ni hivyo hivyo,... kuoa maana yake 'kujifunga' na matamanio, hata kama utapenda, kutamani, au kushikwa na uchu kiasi gani... Jifungie tu humo humo kwenye ndoa, Open marriages zinaondoa maana kamili ya neno 'Marriage'.

  sijui wengine mwalionaje hili...
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Apr 3, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wale waliooana mami wangu si ndio wanaopractice hii au mie nimekosea? Yaani wanaoana then wako na ruhusa ya kupenda nje na kuwa na mpenzi wa nje kwa uwazi kwa kuwa penzi limeota pale?
   
 5. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  hizi ndoa czikubaliani nazo kabisa, kama ya wazungu tuwaachie wazungu mami,hapa tu tunapelekeshwa na hzi za kifungo ki hivi je ikiwa hizo open marriages c itakuwa balaa?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,539
  Likes Received: 81,974
  Trophy Points: 280
  Kupenda unaweza kupenda zaidi ya mmoja, lakini huwezi kuwapenda sawa sawa lazima utakuwa na mapenzi zaidi kwa mmoja kwa sababu mbali mbali. Kama wale wenye wake wawili au zaidi wanawapenda wote lakini kuna mmoja ndiyo mwenye kupendwa zaidi kuliko wengine.

  Hawa wanataka kuhalalisha tu kutembea nje na wenyewe wanadai utaratibu huu unasaidia sana kupunguza ugomvi nyumbani na hata divorce rate kwa wale participants wa hizi open marriages wanadai ni ndogo sana. Hata weusi wa Marekani wameanza kuiga utaratibu huu kidogo kidogo wengine yana washinda na wengine wanafurahia, lakini kwa maoni ya ngu inatak moyo wa hali ya juu kushiriki kwenye ndoa kama hizi, mungu apishilie mbali zisiingie kwetu.
   
 7. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Uzinzi ni tatizo lenye umri sawa na umri wa binadamu duniani.
  Utapenda wangapi ili ufike mwisho wa kupenda?
  Ni kupenda au ni kupembua?
   
Loading...