Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Neno.

Ila kuna kitu kimoja nataka kukiweka sawa.

Mimi kwa upande wangu naona itakuwa bora zaidi iwapo kwa bahati mbaya Baba wa Mtoto awe ametangulia mbele ya haki, hapo hata ukichukua jumla unakuwa na Amani ya MOYO.

Lakini haya mambo ya kuchukua jumla, halafu Baba wa Mtoto awe kichwa cha PANZI halafu king'ang'anizi, kinachofuata ni kusumbuana.

Na utakuta mwingine hata kama Mapenzi yalishakwisha ila Baba wa Mtoto akisikia kuna Mtu anataka kuchukua jumla, basi hapo ni mwanzo wa matatizo.

Kisa cha kujitakia matatizo yasiyo ya ulazima, na yanayohepukika!?

Ni bora kuepusha shari
 
Umesomeka mkuu sio wote wataoa single mother we na wenzako mkioa haina shida
Usituaminishi au kutulazimisha kile utakacho wewe

Oa mkuu.. Nisubir uzi wako baada ya hapo sikio la kufa halisikii dawa kila siku mnaambiwa mnajifanya mna mihemko na huruma
 
Kuna mwingine huku anatafuta mume, ni single mother mzoefu ana watoto watatu kila mmoja na baba yake. Ukitaka namba yake ntakupa, kwa kweli yeye hana makosa, wanaume wanamwonea tu, nenda kampe faraja aliyoikosa. Una roho nzuri unavyoojieleza.
 
Viwanja vyenye mgogoro hivyo
Kiwanja chenye migogoro ni ngumu sana kukijenga. Utaishia kupanga miaka yote. Labda upate anayejua umuhimu wa ndoa au awe alijeruhiwa moyo vyakutosha.

Yeyote nitaoa ila Kiukweli siku nikioa single mother, vigezo na masharti vitazingatiwa mno.
 
Nina mwanamke ambae tuna mtoto, ila hatukuweza kuoana kutokana matatizo yaliyojitokeza wakati huo. Baadae alioolewa na sasa ni zaidi ya miaka mitano tangu aolewe, mtoto alimwaacha nyumbani kwao, nilimuomba baada ya kuolewa tukatishe mawasiliano kwa afya ya mahusiano yetu, tukawa hatusiwasiliani tena, mawasiliano pekee yakabaki kwa mamaake mzazi na mdogo wake wa kike.

Baadae nilimchukua mtoto nikampeleka Kenya kusoma, ikawa wakati wa likizo nampeleka kwa bibi yake maana ndiko alikokuzoea, sasa hivi karibuni nilimfuata mtoto nimpeleke shule, nikamkuta huyu mzazi mwenzangu yupo kwao, akaniambia kuwa alikuwa ananisubiria mimi ana mambo muhimu ya kuniambia. Akasema mazungumzo hayo yatafanyika mjini na vile vile alitaka kumfanyia mtoto wake shopping, tukaondoka mpaka mjini, lakini cha ajabu alitupeleka kwenye nyumba ambayo amejenga akasema amemjengea akanipa na documents zote, baadae akanionesha dukani ambalo amefungua na faida ataiweka kwenye akaunti ya mtoto.

Baadae tukaenda kupata chakula ili tuendelee na safari ya shule, tukiwa kwenye chakula nilimuuliza amewezaje kujenga na kufungua duka kubwa vile, akaniambia anamuibia mme wake, kwamba yeye ndie msimamizi wa biashara za mme wake na pesa zote anachukua, alinionesha akaunti yake imenona.

Mbaya zaidi kilichonifanya niandike hapa aliniomba usiku huo tuwe pamoja na kesho yake ndio tuendelee na safari, baada ya ombi hilo, nikamfikria jamaangu (simfahamu) jinsi anavyoibiwa na huyu mwanamke halafu na mimi nimuibie? Nikaona nikikataa moja kwa moja angejisikia vibaya, nikamdanganya nimeisha kanyaga miwaya, akaishia kunishukru na kunipongeza kwa kumuokoa.

Baada ya hapo nimefikria sana kuhusu hawa single mothers, hivi wanakwama wapi? Wanakumbuka nini kwa wanaume waliowazalisha?
 
Shida nini?
Amekuibia wewe?
Halafu unauliza singo maza mnakwama wapi,umejumlisha dingo maza wangapi kwa hiyo tabia ya hiyo mmoja?
Pia ni vema ungemuuliza anakwama wapi kama angekua kazubaa,hawazi future yake na mwanae,kesho anaweza achika hapo na mtoto hana shule hana pa kwenda.sasa ye kajiongeza we unaponda unatakaje?
Mwanamke ana akili kaona fursa,badala ya kuipiga teke naona awekeze kwa future ya mwanae.ana uhakika hata ndoa ikivunjika ana pa kulaza kichwa ye na mwanae,ana uhakika account itampeleka mtoto shule...halafu anakuamini kama baba wa mtoto anakushirikisha unajibaraguza unatakaje?
Si bure kama baba wa mtoto hapo ulipo hujui hata lini utamjengea urithi huyo mtoto,
Ovyo kabisa!
 
Back
Top Bottom