Nashukuru sana kwa barua yako, ni vizuri akajua chanzo cha serikali kuchukua hatua ilizochukua na pili afuatilie historia ya nchi, kuhusu ulipaji kodi, na ukwepaji wa kumbukumbu, na pia kama anaona wa Tz uwezo huo hawana wa kujua jinsi ya kukabiliana na suala hili is kodi aombe ushauri wa pwc, au nchi kama UK , hii mifumo wanayoweka au walioweka wenzetu ndio inayosaidia, ukusanyaji wa kodi, sasa sisi tumechelewa, badala ya kukumbia kulifikia lengo husika tuna rudi nyuma, halafu tutakuja kulaumiana tena , kwa kudai kodi zaidi ya miaka 5.Mhe Rais, naomba utumie dakika chache kusoma barua hii wewe mwenyewe, na kama hautapata muda naomba wasaidizi wako wakusaidie kuusoma na kukufikikishia.
Naandika haya kama Raia aliye na wasiwasi baada ya kutafakari kwa kina juu ya "TONE" yako uliyokwishaitoa hadharani kuhusu taasisi hii nyeti inayokusanya mapato ya nchi.
Pia ni baada ya kukaa na baadhi ya maafisa kodi ambao wanakiri kwamba toka kauli yako kazi yao imekuwa ngumu kupindukia. Na wanasema kabisa wamekaa benchi tu wanasikilizia!!!.
Mhe. Rais, kwa sasa kuna mambo makuu mawili yanayotokea ambayo sidhani kama umeshayajua.
i) Wafanyabiashara wameacha kutoa risiti za EFD na ukiwadai wanasema kabisa WASISUMBULIWE maana Rais wao ameshatoa maelekezo hayo. Wapo HOLIDAY!!.
Hata TRA wenyewe wamecancel mazoezi ya ku-enforce utoaji risiti. Maana wanajua wakienda watabagazwa!
Swali kubwa hapa, Je, Kodi gani itakusanywa na nchi bila watu kutoa risiti? Unawezaje kutrack mauzo ya mlipa kodi bila kutoa risiti ya EFD?
ii) Wafanyabiashara hawapeleki tena malipo ya kodi kwa kama kasi ya awali, kila mmoja ameset mind ya kupinga kodi maana anaona kama kile alichokadiriwa si sahihi baada ya kauli ya Rais.
Wataalam wenyewe wanasema impact yake itaonekana katika taarifa za mapato mwezi huu na ijayo!.
Mhe Rais, katika taasisi zote chini yako zinazohitaji Top Level Presidential Support ya moja kwa moja ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Bila TRA yenye support ya Rais, Taifa linakufa, na hakika litashindwa kufikia malengo yake.
Ni sawa na katika taasisi za kawaida, kitengo ambacho kinaleta mapato kwa taasisi, ndicho Mkurugenzi Mkuu hukitolea macho na kukipa support yote inayohitajika ili aweze kufikia malengo yake kibiashara.
Mhe Rais, sitaki kurejea katika maagizo yako ya nyuma kuhusu namna TRA wanavyofanya kazi ambayo uliyatoa hadharani, ila ningekuwa mmoja wa washauri wako ningeshauri usiongee sentensi zile hadharani bali uongee moja kwa moja na Viongozi na Wafanyakazi wa TRA indoors.
Kwa nini??. Kwa sababu nature ya mfanyabiashara ni kulalamika na kuficha mapato yake halisi. Hakuna mfanyabiashara hata mmoja aliye genuine ya kipato chake, Popote duniani. Hakuna!
Mhe. Rais, unaweza kukuta mfanyabiashara anafanya biashara yenye mauzo ya Billioni 2 anadeclare faida ya milioni 4, Seriously?
Katika mazingira hayo unahitaji Taasisi yenye nguvu na mamlaka ili iweze kutafuta wapi mtu huyu alipodanganya ili Serikali iweze kukusanya kodi yake. Otherwise, utachukua hio hio Milioni 4 alafu maisha yanaendelea wakati kwa hakika labda mtu huyo alipaswa kulipa milioni 50.
Mwisho:
Natambua kupitia maneno ya Makamu wako, Mhe. Mpango, umeweka malengo ya Trillion 2 kwa Mwezi, lakini ukweli ni kwamba hata kama sheria zitabadilika na baadhi ya kodi kupungua lazima kuna nyingine zitapanda ili kufikia lengo la Trillion 2. Sasa nani atatumika kuenforce ukusanyaji huo? Je ni hao hao TRA? Je wataweza ku-enforce huo ukusanyaji bila support yako? Au kuna watu wanaku-sabotage ili ushindwe kufikia malengo hayo?.
Naomba kuhitimisha kwa kukushukuru kwa muda wako.
Wako,
Raia aliye na wasiwasi.
15 April, 2021
Nakala:
Mhe Makamu wa Rais
Mhe Waziri Mkuu
Mhe Waziri wa Fedha
Kamishna wa TRA.
Na viongozi wetu wakiwa wanasikiliza hadithi za wafanya biashara iwe kodi au wafanyakazi wa kigeni awaambie tu , malalamiko yenu nimesikia nitaweza washauri wangu , ili ajue na ya upande wa pili yakoje.
Sasa inawezekana amemtoa Bure aliyekuwa commissioner general wa tra.
What's the maximum penalty for tax evasion in the UK? The penalty for tax evasion can be anything up to 200% of the tax due and can even result in jail time. For example, evasion of income tax can result in 6 months in prison or a fine up to £5,000, with a maximum sentence of seven years or an unlimited fine.
tax avoidance—An action taken to lessen tax liability and maximize after-tax income.
tax evasion—The failure to pay or a deliberate underpayment of taxes. underground economy—Money-making activities that people don't report to the government, including both illegal and legal activities.