Open Letter: Rais Samia, TRA isiyo na Support yako, ni Kifo cha Taifa

Donyongijape

JF-Expert Member
May 28, 2010
1,497
811
Mhe Rais, naomba utumie dakika chache kusoma barua hii wewe mwenyewe, na kama hautapata muda naomba wasaidizi wako wakusaidie kuusoma na kukufikikishia.

Naandika haya kama Raia aliye na wasiwasi baada ya kutafakari kwa kina juu ya "TONE" yako uliyokwishaitoa hadharani kuhusu taasisi hii nyeti inayokusanya mapato ya nchi.

Pia ni baada ya kukaa na baadhi ya maafisa kodi ambao wanakiri kwamba toka kauli yako kazi yao imekuwa ngumu kupindukia ni kama wamewekwa benchi!

Mhe. Rais, kwa sasa kuna mambo makuu mawili yanayotokea ambayo sidhani kama umeshayajua.

i) Wafanyabiashara wameacha kutoa risiti za EFD na ukiwadai wanasema kabisa WASISUMBULIWE maana Rais wao ameshatoa maelekezo hayo. Wapo HOLIDAY!

Hata TRA wenyewe wamecancel mazoezi ya ku-enforce utoaji risiti. Maana wanajua wakienda watabagazwa!

Swali kubwa hapa, Je, Kodi gani itakusanywa na nchi bila watu kutoa risiti? Unawezaje kutrack mauzo ya mlipa kodi bila kutoa risiti ya EFD?

ii) Wafanyabiashara hawapeleki tena malipo ya kodi kwa kama kasi ya awali, kila mmoja ameset mind ya kupinga kodi maana anaona kama kile alichokadiriwa si sahihi baada ya kauli ya Rais.

Wataalam wenyewe wanasema impact yake itaonekana katika taarifa za mapato mwezi huu na ijayo!

Mhe Rais, katika taasisi zote chini yako zinazohitaji Top Level Presidential Support ya moja kwa moja ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Bila TRA yenye support ya Rais, Taifa linakufa, na hakika litashindwa kufikia malengo yake.

Ni sawa na katika taasisi za kawaida, kitengo ambacho kinaleta mapato kwa taasisi, ndicho Mkurugenzi Mkuu hukitolea macho na kukipa support yote inayohitajika ili aweze kufikia malengo yake kibiashara.

Mhe Rais, sitaki kurejea katika maagizo yako ya nyuma kuhusu namna TRA wanavyofanya kazi ambayo uliyatoa hadharani, ila ningekuwa mmoja wa washauri wako ningeshauri usiongee sentensi zile hadharani bali uongee moja kwa moja na Viongozi na Wafanyakazi wa TRA indoors.

Kwa nini??. Kwa sababu nature ya mfanyabiashara ni kulalamika na kuficha mapato yake halisi. Hakuna mfanyabiashara hata mmoja aliye genuine ya kipato chake, Popote duniani. Hakuna!

Mhe. Rais, unaweza kukuta mfanyabiashara anafanya biashara yenye mauzo ya Billioni 2 anadeclare faida ya milioni 4, Seriously?

Katika mazingira hayo unahitaji Taasisi yenye nguvu na mamlaka ili iweze kutafuta wapi mtu huyu alipodanganya ili Serikali iweze kukusanya kodi yake. Otherwise, utachukua hio hio Milioni 4 alafu maisha yanaendelea wakati kwa hakika labda mtu huyo alipaswa kulipa milioni 50.

Mwisho:
Natambua kupitia maneno ya Makamu wako, Mhe. Mpango, umeweka malengo ya Trillion 2 kwa Mwezi, lakini ukweli ni kwamba hata kama sheria zitabadilika na baadhi ya kodi kupungua lazima kuna nyingine zitapanda ili kufikia lengo la Trillion 2. Sasa nani atatumika kuenforce ukusanyaji huo? Je ni hao hao TRA? Je wataweza ku-enforce huo ukusanyaji bila support yako? Au kuna watu wanaku-sabotage ili ushindwe kufikia malengo hayo?

Naomba kuhitimisha kwa kukushukuru kwa muda wako.

Wako,
Raia aliye na wasiwasi.
15 April, 2021

Nyongeza muhimu kutoka kwa baadhi ya wadau 👇

Mkuu nakubaliana na wewe 100%.Statement za Rais Samia kuhusu ukusanyaji kodi ni msumari wa mwisho katika ukusanyaji kodi na mustakali mzima wa mapato ya serikali.Rais Samia anapaswa kutambua kwamba hakuna mfanyibiashara anayependa kulipa kodi kwa hiari,kwa hiyo her soft approach ni suicide.Hii ina maana kwamba ni lazima mbinu zozote zile zitumike ili kuhakikisha kwamba wafanyibiashara wanalipa kodi,kama hawataki kulipa kwa hiari.
Nashukuru sana kwa barua yako, ni vizuri akajua chanzo cha serikali kuchukua hatua ilizochukua na pili afuatilie historia ya nchi, kuhusu ulipaji kodi, na ukwepaji wa kumbukumbu, na pia kama anaona wa Tz uwezo huo hawana wa kujua jinsi ya kukabiliana na suala hili is kodi aombe ushauri wa pwc, au nchi kama UK , hii mifumo wanayoweka au walioweka wenzetu ndio inayosaidia, ukusanyaji wa kodi, sasa sisi tumechelewa, badala ya kukumbia kulifikia lengo husika tuna rudi nyuma, halafu tutakuja kulaumiana tena , kwa kudai kodi zaidi ya miaka 5.
Na viongozi wetu wakiwa wanasikiliza hadithi za wafanya biashara iwe kodi au wafanyakazi wa kigeni awaambie tu , malalamiko yenu nimesikia nitaweza washauri wangu , ili ajue na ya upande wa pili yakoje....

What's the maximum penalty for tax evasion in the UK? The penalty for tax evasion can be anything up to 200% of the tax due and can even result in jail time. For example, evasion of income tax can result in 6 months in prison or a fine up to £5,000, with a maximum sentence of seven years or an unlimited fine.

Kwa kweli unastahili kupewa nishani ya Mzalendo mkereketwa! Mungu akubariki sana! Wafanyabiashara ni watu muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa. Tatizo ni kwamba watanzania hatuna elimu ya kodi kama sehemu ya uzalendo. Tangu chekechea mpaka chuo kikuu hakuna mahali elimu ya kodi na umuhimu wake inafundishwa!
Kwa hiyo karibu wafanyabiashara wote hawalipi kodi kwa hiari! Ukiwapa mwanya watakwepa kodi au watatoa kodi kwa udanganyifu! Kwa sababu ya mazoea ya kukwepa kodi, wafanyabiashara wakifuatiliwa vilivyo kuhusu kodi wanahisi wanaonewa! Wakitoa kodi wanahisi faida inapungua maana walizoea kuifanya kodi iliyopaswa kulipwa kama sehemu ya faida!
Kwa sasa hivi TRA watakuwa na wakati mgumu sana wa kufuatilia kodi, maana wametafisirika kama vile walikuwa wanabambikiza kodi! Mama huu ushauri uliopewa ni wa muhimu sana! Wasaidizi wako wengine wanaweza wasikushauri huku wakitazamia ukwame halafu waseme hakuwa anakubali ushauri! Kwa mazingira ya Tanzania hiki kizazi chetu ni cha kulipa kodi kwa lazima wala katika hili tusidanganyane! Tuwekeze kwenye elimu ya kodi tangu chekechea ili vizazi vijavyo vione fahari ya kulipa kodi!! Mama kaza buti kabisa kwa habari ya kodi ikiwezekana katika hili uwe mkali kuliko mtangulizi wako. Ukikamata mkwepa kodi mfilisi kabisa ili wengine waogope! Vinginevyo we are bound to fail!

Kwa mtu niliye na tajiriba na IRS [TRA ya Marekani], naona kama vile Watanzania bado hatuko serious na ukusanyaji kodi!

IRS ni moja ya tax collecting agencies zisizo na mzaha.

Ukitaka kukusanya mapato kupitia kodi, basi ni lazima uwe thabiti.

Upole haufai.

Lakini pia haina maana kuwa ndo uonee watu, ingawa ni kawaida ya binadamu kuona anaonewa hata kama si kweli.

Postscriptum (PS): Kuna baadhi ya wachangiaji katika uzi huu wana attack mleta mada wakisema alikuwa mnufaika wa utaratibu wa awali i.e mfanyakazi TRA, alikuwemo kwenye taskforce n.k.

Inasikitisha sana pale mtu badala ya kusikiliza na kuijibu hoja anadhani wewe ni mnufaika, umehongwa, kibaraka sababu tu umenena jambo tofauti na aloamini. Ni legacy mbaya sana hii.

Niseme tu, mimi sio mfanyakazi wa TRA na sio mnufaika wa mfumo. ILA nimetoa experience yangu baada ya kuona realities mtaani (mfano suala la risiti limenikuta mimi kama mimi si mara moja) na pia katika mijadala yetu sisi wananchi pamoja na maoni ya baadhi ya maafisa wa TRA ambao tupo nao mitaani maana nao ni binadamu wa kawaida tunaishi nao.

So in simple terms, I did this not for any personal gain rather, I decided not to keep quite for National Interest.
 
Wakenya wapewe kazi wataliendeaha shirika vizuri kabisa!
Hawanaga ujinga wa kususia kazi!
Wana jua pia mipaka ya kazi
Hawajasusa, ila unfortunately kwetu sisi neno la Rais ni sheria. Usitegemee law enforcers kwenda against maneno/maagizo ya Rais, wawe wakenya au wamarekani
 
Kulipa kodi ni takwa la sheria, hao wafanyabiashara wanatakiwa kulipa kodi kutimiza wajibu wao, wakigoma wacha sheria ichukue mkondo wake, na hao maafisa wa TRA unaosema wameamua kukaa pembeni kwa kuogopa kubagazwa ni wazembe wanatakiwa kuadhibiwa.
 
Hawajasusa, ila unfortunately kwetu sisi neno la Rais ni sheria. Usitegemee law enforcers kwenda against maneno/maagizo ya Rais, wawe wakenya au wamarekani
Wakenya wana piga kazi sana ukweli ndio huo sisi tumezoea dhuluma hatujui kufuata sheria Kenya wana jua haki ya kisheria kuliko sisi!
TRA ipewe wakenya tu watafuata sheria bila kudhulumiwa serikali wala wafanya biashara!
 
Wasiwasi wako nini???Kwamba kodi haitakusanywa au itapungua??Mpe muda mheshimiwa rais anajua nini anafanya,Kufika Dar es Salaam kutoka Mwanza njia ni nyingi,unaweza ukatumia ndege ukafuka,basi ukafika,lorry ukafika baiskeli ukafika,pikiki ukafika,kutembea kwa mguu ukafika hata ungo ukafika,lengo ni kufika Dar sasa wewe utaona ni njia ipi kufuatana na uwezo wako na muda wako.
 
Huu ni ushauri wenye roho mbaya,wafanyabiashara wamenyanyasika sana acha nao waheme kidogo.TRA inapaswa kufanya kwa weledi na bila kutumia nguvu.Ukiambiwa hivyo unaenda kutengeneza monitoring system ya kujua kipi ni kipi.Kama kuna mtu hajatoa risiti sheria ipo wazi.
 
Mtoa hoja pamoja na hoja yako kuwa nzuri binafsi ninaona umeiandika kwa kuangalia upande mmoja wa coin,kodi no wajibu wa kila mwananchi na ni wajibu wa TRA kutoa elimu ya ufahamu ili watanzania tutambue umuhimu wa kulipa kodi,binafsi ningepata uwezo wa kushawishi serikali mambo yafuatayo kuhusu TRA;

ondoa neno Authority na badala yake wake a more friendly word Service,hii itasaidia kuondoa woga kwa walipa kodi hasa kuona kuwa hawalazimishwi ila ni wajibu wetu (Tanzania Revenue Service..TARS)

hivyo hivyo hata kwa jeshi letu la polisi(TAPS);pia TRA wasiwe wanakusanya tu pia wawe na uwezo wa kufanya return kwa walipa kodi kutegemea kiwango chao.nchi inahitaji uwajibikaji unaozingatia haki na wajibu wetu sio kila kitu ni nguvu tu.
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom