Open Letter: Rais Samia, TRA isiyo na Support yako, ni Kifo cha Taifa

Najua ni mtumishi wa TRA,lakini ni kweli kwamba huwezi kumbembeleza mfanyibiashara asiyetaka kulipa kodi.Uta-coerse to some point,lakini akikataa ni lazima alazimishwe na sheria kufanya hivyo.
Wafanyabiashara sio waajiriwa, naona unaoverlook hilo
Tunduma wafanya biashara walihamia upande wa zambia walipoona wanasumbuliwa na kodi zisizoeleweka , na hadi leo hii baadhi hawajarudi upande wetu,. bado hujapata clue tu mfanyabiashara ni mtu gani?
unaweza kumnyanyasa muajiriwa kwa kuwa hana means , wafanyabiashara wanondoka na mitaji yao kuelekea kwenye nafuu ya kodi, na huwezi zuia hilo, mitaji ni yao na huko wanapokwenda wanapokelewa, kwa sababu watalipa kodi na kuchangia maendeleo ya nchi husika.
 
Hayo yote ni sawa kabisa mkuu,TRA wabuni new revenue sources,hilo halina ubishi,ila under scrutiny here are President Samias' statement ambayo ina potential ya kupunguza mapato.
Mapato yaliyokusanywa mengi yalikuwa cosmetic na fictious kwa vile yalitokana na dhuluma na kubambikwa/kupora ili mradi kufikia malengo yaliyokuwa yamewekwa bila uhalisia wa mapato ya biashara au faida,mitaji ilipigwa kodi na kuua biashara. Ndiyo maana biashara nyingi zikafa eg kampuni ya tumbaku morogoro.
 
Hii ni hatari sana.

KODI NDIO usalama na UHAI wa TAIFA bila kukusanya KODI basi tena ndio tunaenda kuzimu.

wafanya biashara walio wengi ni wa kwepa KODI kamwe hawawezi kulipa kodi bila kushurutishwa.

Kwenye suala la KODI viongozi wetu wawe imara.
kukwepa kodi ni kama tabia za utoro shuleni, ukitaka kutatua tatizo hili ni lazima ujiulize kwa nini wanafunzi ni watoro.
ukitjmia nguvu sana hufanikiwi na unazidi kuongeza tatizo , kuna nchi kukwepa kodi ni aibu maana kodi ipo wazi na inalipika.
 
kwa uchunguzi wangu, nimegundua kuna taasisi nyingi za serikali wanamhujumu mama. kama TRA wamevunjwa nguvu ya kukusanya, na wameamua kukaa tu kimya ili mapato yapungue na maza ajue cha kufanya. hilo bomu lipo na linakuja. nasema hivi kwasababu hakuna mtu anayeweza kulipa kodi kwa hiari, bila kushurutishwa kwa nchi zetu, ulaya sawa ila hapa hata mimi nalipa kodi kwa mbinde, kama hakuna kulazimishwa na fujo kidogo nakwepa vizuri tu. nafikiri mama anatakiwa atoe tamko kuwa aliposema wafanya biashara wasinyanyaswe nia haikuwa wasilipe kodi, mtu asiyelipa kodi ni kosa la jinai anatakiwa akamatwe. \

kama wanataka kurudisha wafanyabiashara, wapunguze makodi hayo ili tukusanye kwa watu wengi hata kama kidogokidogo, ili wafanyabiashara wasikimbie. na hicho kidogo tutakusanya kwa nguvu. EFD zitumike na anayenunua na kuuza bila hizo akamatwe. Magu alifanikiwa katika hili ndio maana tumeishi bila mikopo kwa muda mrefu tukitumia hela zetu wenyewe.
Weee kaa kimyaaa katika kipindi deni la taifa limepanda maradufu ni kipindi cha mwendazake
 
kukwepa kodi ni kama tabia za utoro shuleni, ukitaka kutatua tatizo hili ni lazima ujiulize kwa nini wanafunzi ni watoro.
ukitjmia nguvu sana hufanikiwi na unazidi kuongeza tatizo , kuna nchi kukwepa kodi ni aibu maana kodi ipo wazi na inalipika.
Nukuu;

"Mfanyabiashara/Tajiri kuingia ktk Ufalme wa Mbiguni ni sawa na ngamia kupenya ktk tundu la sindano"


wafanyabiashara walio wengi wanataka kupata faida kwa njia yoyote ile.................

wachache ni wazalendo kwa Taifa lao, wengi ni wa kwepa kodi.

ni ukosefu tu wa maadili na uzalendo, ndio maana kuna hata baadhi ya viongozi ni wabadhirifu wa mali za umma, vivo hivyo kuna baadhi ya wafanyabiashara sio waaminifu.

Tulipe kodi kwa ajili ya kulijenga taifa letu
 
Mhe Rais, naomba utumie dakika chache kusoma barua hii wewe mwenyewe, na kama hautapata muda naomba wasaidizi wako wakusaidie kuusoma na kukufikikishia.

Naandika haya kama Raia aliye na wasiwasi baada ya kutafakari kwa kina juu ya "TONE" yako uliyokwishaitoa hadharani kuhusu taasisi hii nyeti inayokusanya mapato ya nchi.

Pia ni baada ya kukaa na baadhi ya maafisa kodi ambao wanakiri kwamba toka kauli yako kazi yao imekuwa ngumu kupindukia ni kama wamewekwa benchi!

Mhe. Rais, kwa sasa kuna mambo makuu mawili yanayotokea ambayo sidhani kama umeshayajua.

i) Wafanyabiashara wameacha kutoa risiti za EFD na ukiwadai wanasema kabisa WASISUMBULIWE maana Rais wao ameshatoa maelekezo hayo. Wapo HOLIDAY!

Hata TRA wenyewe wamecancel mazoezi ya ku-enforce utoaji risiti. Maana wanajua wakienda watabagazwa!

Swali kubwa hapa, Je, Kodi gani itakusanywa na nchi bila watu kutoa risiti? Unawezaje kutrack mauzo ya mlipa kodi bila kutoa risiti ya EFD?

ii) Wafanyabiashara hawapeleki tena malipo ya kodi kwa kama kasi ya awali, kila mmoja ameset mind ya kupinga kodi maana anaona kama kile alichokadiriwa si sahihi baada ya kauli ya Rais.

Wataalam wenyewe wanasema impact yake itaonekana katika taarifa za mapato mwezi huu na ijayo!

Mhe Rais, katika taasisi zote chini yako zinazohitaji Top Level Presidential Support ya moja kwa moja ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Bila TRA yenye support ya Rais, Taifa linakufa, na hakika litashindwa kufikia malengo yake.

Ni sawa na katika taasisi za kawaida, kitengo ambacho kinaleta mapato kwa taasisi, ndicho Mkurugenzi Mkuu hukitolea macho na kukipa support yote inayohitajika ili aweze kufikia malengo yake kibiashara.

Mhe Rais, sitaki kurejea katika maagizo yako ya nyuma kuhusu namna TRA wanavyofanya kazi ambayo uliyatoa hadharani, ila ningekuwa mmoja wa washauri wako ningeshauri usiongee sentensi zile hadharani bali uongee moja kwa moja na Viongozi na Wafanyakazi wa TRA indoors.

Kwa nini??. Kwa sababu nature ya mfanyabiashara ni kulalamika na kuficha mapato yake halisi. Hakuna mfanyabiashara hata mmoja aliye genuine ya kipato chake, Popote duniani. Hakuna!

Mhe. Rais, unaweza kukuta mfanyabiashara anafanya biashara yenye mauzo ya Billioni 2 anadeclare faida ya milioni 4, Seriously?

Katika mazingira hayo unahitaji Taasisi yenye nguvu na mamlaka ili iweze kutafuta wapi mtu huyu alipodanganya ili Serikali iweze kukusanya kodi yake. Otherwise, utachukua hio hio Milioni 4 alafu maisha yanaendelea wakati kwa hakika labda mtu huyo alipaswa kulipa milioni 50.

Mwisho:
Natambua kupitia maneno ya Makamu wako, Mhe. Mpango, umeweka malengo ya Trillion 2 kwa Mwezi, lakini ukweli ni kwamba hata kama sheria zitabadilika na baadhi ya kodi kupungua lazima kuna nyingine zitapanda ili kufikia lengo la Trillion 2. Sasa nani atatumika kuenforce ukusanyaji huo? Je ni hao hao TRA? Je wataweza ku-enforce huo ukusanyaji bila support yako? Au kuna watu wanaku-sabotage ili ushindwe kufikia malengo hayo?

Naomba kuhitimisha kwa kukushukuru kwa muda wako.

Wako,
Raia aliye na wasiwasi.
15 April, 2021

Nyongeza muhimu kutoka kwa baadhi ya wadau 👇








Postscriptum (PS):
Kuna baadhi ya wachangiaji katika uzi huu wana attack mleta mada wakisema alikuwa mnufaika wa utaratibu wa awali i.e mfanyakazi TRA, alikuwemo kwenye taskforce n.k.

Inasikitisha sana pale mtu badala ya kusikiliza na kuijibu hoja anadhani wewe ni mnufaika, umehongwa, kibaraka sababu tu umenena jambo tofauti na aloamini. Ni legacy mbaya sana hii.

Niseme tu, mimi sio mfanyakazi wa TRA na sio mnufaika wa mfumo. ILA nimetoa experience yangu baada ya kuona realities mtaani (mfano suala la risiti limenikuta mimi kama mimi si mara moja) na pia katika mijadala yetu sisi wananchi pamoja na maoni ya baadhi ya maafisa wa TRA ambao tupo nao mitaani maana nao ni binadamu wa kawaida tunaishi nao.

So in simple terms, I did this not for any personal gain rather, I decided not to keep quite for National Interest.
Kilichozungumzwa ni kama zile kodi za ushuru wa magari bandarini, kodi ilikuwa milioni 3 mara paap imekuwa milioni 5 na usipolipa gari linapigwa mnada. Wakati sheria zinasema tozo za kodi zinapangwa na kupitishwa bungeni wakati wa bajeti ya bunge na sio tu Kamishna wa TRA au Rais wa nchi atavyojisikia. Ndio akasema TRA tozeni kodi kwa sheria na kutoonea
 
Back
Top Bottom