Oparesheni UKUTA yapingwa, wake wa viongozi wa UKAWA wawasihi waume zao waachane na mpango huo

Sasa na wewe mleta Mada unataka kumsihi nani?
Halafu ninachoona huu mjadala baadhi ya watu wa CCM watamtukana na kumdhalilisha Joyce wakijifanya kuwa ni watu wa CHADEMA.

Lengo kuleta mgawanyiko na kujenga chuki za ndani kwa ndani na kutoa watu kwenye ajenda
Huu uzi ni wa kupuuza
Tatizo liko kwa wahariri wa gazeti ambalo wewe pia tunaona makala zako zikichapishwa-Raia Mwema/Raia Tanzania, hili ndilo gazeti limeona hii ni stori na likatumia headline ya "Wake wa viongozi...."! Ukifuatilia kinachoandikwa na gazeti hili ni rahisi kubaini kuwa lina ajenda maalum dhidi ya Chadema/upinzani. Headline zake huwa za ajabuajabu zenye nia ovu dhidi ya upinzani/Chadema. Headline ya jana kwenye lead stori ya Raia Mwema nayo ni ya kimkakati. hovyo kabisa!
 
Wana jamvi wasalam.
Wakati UKAWA wakiwa na mpango wa kufanya maandamano nchi nzima ya kupinga kwa kile wanacho kisema ni unyanyasaji na ukandamizaji wa demokrasia.

Huku kukiwa na katazo kubwa sana la kuzuia maandamano hayo. Baadhi ya wake wa viongozi waandamizi wa UKAWA wameanza kufunguka na kueleza jinsi ambavyo wamekuwa wakiwasihi waume zao kuachana na mpango huo kwani unaweza kuwapa tabu wao na wataumia.

Aliye kuwa wa kwanza kufunguka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa picha ni Bi Joyce Kiria mke wa Ndug Henry Kilewo ambaye ni kiongozi ndani ya chadema.

Alisema amekuwa akimsihi kila leo kuwambia wenzie watafute njia nyingine kwani njia wanayo taka kutumia hawato fanikiwa.. Aliweka wazi kabisa kuwa tofauti na Mh JK ambaye alikuwa akiwachekea na pengine kuwaalika ikulu kunywa nao chai wanapo tofautiana huyu wa sasa hana muda huo na wasimchokoze..

Bi Joyce Kiria alienda mbali na musema alimwambia mumewe kuwa aangalia future ya watoto wake na familia na alinganishe na huo UKUTA.

Pia aliwaomba wanawake wa viongozi wa UKAWA waungane kuwasihi waume zao kuachana na mpango huo na kutafuta njia nyingine ya kutatua migogoro hiyo na si maandamano.

Wana jamvi kama mtakumbuka kipindi cha Mh JK Kilewo alishakumbwa na case kubwa iliyo mpelekea mkewe kuzunguka kwenye vyombo vya habari kuomba huruma ya Rais mmewe aachiwe hivyo anaongea anacho kifahamu.

Wana jamvi karibuni.
View attachment 374852View attachment 374853View attachment 374854
Umeandika kuwa 'wake wa viongozi UKAWA wapinga' halafu katika taarifa yote umemuongelea huyo mwanamke mmoja. Je hao wake wa viongozi wengine ni akina nani? au ni wewe?
 
Sasa na wewe mleta Mada unataka kumsihi nani?
Halafu ninachoona huu mjadala baadhi ya watu wa CCM watamtukana na kumdhalilisha Joyce wakijifanya kuwa ni watu wa CHADEMA.

Lengo kuleta mgawanyiko na kujenga chuki za ndani kwa ndani na kutoa watu kwenye ajenda
Huu uzi ni wa kupuuza
 
Sasa na wewe mleta Mada unataka kumsihi nani?
Halafu ninachoona huu mjadala baadhi ya watu wa CCM watamtukana na kumdhalilisha Joyce wakijifanya kuwa ni watu wa CHADEMA.

Lengo kuleta mgawanyiko na kujenga chuki za ndani kwa ndani na kutoa watu kwenye ajenda
Huu uzi ni wa kupuuza

Ben yanaposemwa ambayo huyapendi tulia na uyasikilize. Usiwe kila kinacho kuudhi basi kipuuzwe. Kwani Joyce sio mke wa kiongozi wa CDM ?. Penye ukweli kubali tu .
 
Sasa na wewe mleta Mada unataka kumsihi nani?
Halafu ninachoona huu mjadala baadhi ya watu wa CCM watamtukana na kumdhalilisha Joyce wakijifanya kuwa ni watu wa CHADEMA.

Lengo kuleta mgawanyiko na kujenga chuki za
ndani kwa ndani na kutoa watu kwenye ajenda
Huu uzi ni wa kupuuza
Uzi wananzisha lumumba buku 7 alafu wao ndiyo wanauchangia wenyewe...
 
joyce kiria nae upeo wake wa kifikra ni sawa na jingalao,lizabon na mleta mada
 
1470414078173.jpg


Wadau,
Hivi kama kweli hiyo tar 1 Sept zoezi la kujenga ukuta likifanyika, viongozi wangapi wa CHADEMA watakuwa tayari kuingia 'front line' na wake/familia zao? So far, tunashuhudia wake wa viongozi wa chadema "wanaandamana" mitandaoni kupinga waumezao kuandamana.
Kama nakumbuka sahihi, Josephine Mshumbusi (mke wa Dr. W Slaa) ndo mke wa kiongozi pekee aliyeweza kuingia 'front line' kwenye battlefield...kwa kitendo hiki, Je, ni sawa kusema kuwa Dr & Mrs W. Slaa ndo "the most courageous couple" kwenye ulimwengu wa siasa za upinzani Tanzania?
 
Hakyanani damu hii iliyomwagika kwa ajili ya kuitetea chadema tena ndani ya gwanda lazima iwatafune wale wote waliosababisha mme wake Dr Slaa atimke kuelekea kusipojulikana. tamaa ya pesa kweli ilizika ndoto hizi zilizoibuka za wapambanaji waliokuwa wakiupinga ufisadi kwa dhati kabisa. wajanja wakaamua kulamba manoti na kuamua kubadilishia gia angani ili kuwasafisha wale watuhumiwa ambao kwa miaka kadhaa walikuwa wakiwatuhumu ni mafisadi. KWELI PESA NI MWANAHARAMU. pesa is money! !
 
Na Joyce Kiria.

Yes sikulilia ndani alipoingia matatizoni..... Niligangamala nikapaza sauti na wanangu mchana kweupeee... Haikuwa rahisi hata kidogo lakini ilinibidi kujitoa fahamu kwa ajili ya kuokoa familia yangu
.
.
Leo napoona dalili nyingine za kuingia kwenye matatizo makubwa zaidi ya haya, kamwe siwezi kukaa kimya.... Yes sintakaa kimya nimwache aende kutumbukia shimoni nitamwambia bila aibu kama nilivyompigania bila aibu .
.
Dear love, umenikasirikia sana kwa kitendo hiki ninachofanya... Lakini naomba ukumbuke wakati unapitia matatizo, ni Mimi nilikuwepo na wewe wakati wote mpz wangu mtoto nililazimika kumwachisha ziwa akiwa mdogo sana akalia sana akazoea nikamwacha na Dada kila ilipokuwa tarehe ya kesi nikaja kukutia moyo mpz wangu Tabora mbali kote... Nikajikaza sanaaaa, kukuonyesha tabasamu ili kukupa Amani japo njia nzima nililia sana kwa uchungu ulilia kila uliponionamimi nilijikaza sikulia mbele yako ili nisikuache na mawazooooo....
.
.
Kila nilipokuja Gerezani kukuona uliwaulizia rafiki zako ulokuwa unawaamini sana, tena uliamini wangekuja kesho yake, hukuwaona mpaka ukatoka...ulikuwa unawaulizia kama wamenitafuta, nilikujibu hakuna aliyenitafuta mpz ukaumia sana mpz wangu... Kuna wengine hukutaka hata kuongea nao baada ya kutoka ndani na kurudi uraiani....
.
.
My love, Siko tayari kupitia mateso niliyopata love, siko tayari kukuona katika mazingira magumu kama yale mbaya zaidi ni ya KULAZIMISHA... Labda yatokee bahati mbaya... Lakini ya kwenda kuyatafuta hapana baba..... Najua tena nauhakika hauko tayari kuniona tena katika mateso kama Yale...hilo nauhakika nalo....
.
.
Nimewaambia watoto wanisamehe kama nitakuwa nimekosea, lakini naimani hata wao cha moto walikiona, wasingependa baba yao aingie tena kwenye shida kama ile au zaidi ya ile.... .
.
Popote ulipo jua nakupenda sana ndo maana nakulinda mume wangu kwa garama yeyote .
.
Kwangu Mimi Familia kwanza, Taifa kwanza, chama baadae.....TAFADHALINI UKUTA WEKENI KANDO MFANYE MAZUNGUMZO MEZANI... MSIFANYE UBABE TULIZENI JAZBA KWA FAIDA YA FAMILIA ZENU NA TAIFA ZIMA....
.
.
(NYie mafala mnaosema nimwambie chumbani kwani tunakula dyudyu hapa? mxiuuuuuu zenu)
 
Na Joyce Kiria against UKUTA
Jpili iliyopita daddy alihojiwa na Tido Mhando juu ya hali ya kisiasa nchini.... Kiukweli daddy alinibariki sana kwenye mazungumzo yake na Tido... Alitulia na akajibu maswali yote kwa umakini wa hali ya juu na kwa heshima kubwa kwa Rais wa nchi hii....alionyesha wazi Anakubaliana na hali halisi kwamba Rais wa nchi ni Magufuli... Haijalishi alimshinda kwa bao LA kitu gani.(dady kagoma kuwa nyumbu)
.
.
Alipoulizwa kuhusu UKUTA alisema HAKUNA HAJA YA KUFIKA HUKO UKUTANI.... Na akasema duniani kote MABAVU hayasaidii kutatua migogoro na changamoto za Taifa.. akaongeza na kusisitiza kwamba SIASA NI MAZUNGUMZO... Akaomba sana wakae wazungumze, wasiogopane... Bali wakae meza moja waongee kujenga nchi yetu TANZANIA.... (Nikajiuliza moyoni walishaenda ikulu kuomba kumuona Rais wakazuiwa???)
.
.
Nikapata hisia huenda Daddy alitoa ushauri wa kutatua haya mambo kwa mazungumzo lakini hakusikilizwa... Maana huku mtaa wa pili wameshazoea kutishiatishia na kutunatuna muda wote ndo maana tunaitwa chama cha vurugu daddy hajazoea hizo kashkash maskini baba wa watu, akaona akaongelee AzamTv
.
.
Kiukweli Viongozi wakuu upinzani ongeeni na Rais kwa upole na unyenyekevu tena kwa Adabu... Hicho ndo kinachokosekana kwenu kabisa minaona... Naamini Rais anapoona bit zenu na majina ya kumkebehi juu "dikteta uchwara" hafurahii kabisa....anafadhaika tunavyomdharau wakati yeye ndo Rais halali kisheria... Badala ya kumdhihaki mngetafuta nafasi mkae nae mumweleze tatizo lililopo na kumuomba arekebishe...navyomjua huyo baba angewaskiliza fastaaaa....
.
.
Yaani waliofungiwa bungeni wangefunguliwa, bunge lingeonyeshwa live, mikutano mngefanya nchi nzima n.k Sasa mkiendelea kumtunishia misuli wakati yeye ndo rais halali Tutashaaaaa...jamani mwanaume wa kisukuma hataki kushushwa kifala (hata Mimi nsingekubali kuamrishwa na wapinzani wakati rais ni Mimi) na wapinzani hatutaki kushuka kwanini??? Jamani tusubiri 2020 tujaribu tena, Ila kwa sasa tukubali rais ni MAGUFULI...Tusitake kumpelekesha tumpe nafasi afanye kazi, tukiona anakosea tumfate kwa heshima
.
.
Mkiendelea na UKUTA Wananchi tutashaaaaaaaa..... GOOD MORNING
 
#UKUTA utawaangukia watu wengi...Tahadhari Kama una nia nzuri na nchi yako fanya kazi UKUTA ni mbovu usije ukakuangukia....
 
Wewe buku 7 ushaikosa,umekosa kabisa maneno ya 'kutuokota'?
You are not serious.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom