Oparesheni tokomeza; tumeamua kufunika Kombe mwanaharamu apite?

Noti mpya tz

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
974
225
Wote tunakubaliana Kuwa tatizo letu sio opareshen Tokomeza bali ni Jinsi ilivyoendeshwa na hii imepelekea mawaziri ambao wizara zao zilihusika wajiuzulu, kuna mengi bado yako Nyuma ya Pazia.
Tanzania ni nchi ya matukio inayoenda kwa Mfumo wa funika Kombe mwanaharamu apite hata kwa hili tumeamua kulfi funika Kombe kwa style ya ushabiki na ufinyu wa kutafakari.
1. Kumekuwa na tatizo Ktk mamlaka ya uteuzi wa mawaziri tangu mwanzo wa utawala huu, mamlaka imeshindwa kufanya maamuzi sahihi Ktk Nani ni Mtu sahihi wa wizara husika, rejea uteuzi wa mh. Chenge Kuwa waziri pamoja na Tuhuma zote alizokuwa nano, wizara zinawahusu watanganyika kuongozwa na wazanzibar, wizara ya maliasili na ya nishati kushindwa Kuwa na Watu wa Kuwania mipango na solutions za Munda mrefu.

2. Mawaziri wengi wanaohudumu sasa wameshindwa kuleta Tija Ktk wizara zao. Rejea wizara ya elimu na mipango mibovu inayodidimiza elimu lakini hakuna Hatua zinazochukuliwa kwa wa husika, wizara ya Kilimo kushindwa Kuwa Masada kwa wakulima pamoja na Kuwa na mipango mingi kwenye makaratasi Kama ilivokuwa kwenye op. tokomeza.

3. Waziri Mkuu; Huyu Alitakiwa awe amejiuzulukabla hata ya kufukuzwa uwaziri kwa hm. Ngeleja na Maige lakini ameendelea kuwepo madarakani pamoja na udhaifu mkubwa Kabisa wa kiutawala aliouonyesha, na kwakweli Huyu na mh. Rais ndiyo kiini cha matatizo yetu kwa kushindwa kuwawajibisha Watu walio china Yao na kuendelea kuleta uozo wao. Pengine nakubaliana na wanaosema tatizo letu ni Mfumo lakini tuna tatizo linalozidi Mfumo, tuna tatizo la kufanya maamuzi kuwaumiza Jamaa na rafiki zetu.

Tutafakari haya...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom