Onyo wanawake hapa msiingie hapa hatari:aina mpya ya kisonono(Gonorrhoea) yasambaa duniani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Onyo wanawake hapa msiingie hapa hatari:aina mpya ya kisonono(Gonorrhoea) yasambaa duniani

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jun 28, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Aina mpya ya vimelea vya ugonjwa wa kisonono au "gono" ambavyo vinahimili dawa(resistant to drugs) zinazotumika kutibu ugojwa huu imegundulika duniani. Taarifa iliyotolewa na shirika la afya duniani (WHO) hivi karibuni imesema, ugonjwa wa kisonono unaoathiri mamilioni ya

  watu ulimwenguni umeanza kuwa sugu dhidhi ya dawa zinazotumiwa kuutibu na hivyo kuna hatari ya kutoweza kutibika kabisa.


  Shirika la afya duniani limetoa wito kwa serikali na madaktari kuongeza ufuatlijiaji wa aina hii ya kisonono kutokana na ugonjwa wa kisonono kuwa

  na athari nyingi kama mcharuko (inflammation), ugumba, matatizo wakati wa ujauzito na hata vifo vya kina mama wajawazito.


  “Aina hii mpya ya vimelea vya kisonono vinaonyesha usugu dhidhi ya dawa zote za antibiotiki tunazotumia dhidhi yake ikiwemo dawa za jamii ya

  cephalosporins ambazo ni dawa za mwisho katika kutibu ugonjwa wa kisonono, “ alisema Dk. Manjula Lusti-Narasimhan, mmoja wa wanasayansi wa shirika la afya duniani katika kitengo cha magonjwa ya zinaa.


  Miaka michache ijayo, aina hii mpya ya kisonono itakuwa sugu dhidhi ya dawa zote ambazo tunazo saizi “aliendelea kusema Dk. Manjula Lusti-

  Narasimhan wakati wa mahojiano na shirika la habari la The Associated Press kabla WHO haijatangaza rasmi hatua na mwongozo mpya wa kukabiliana na tishio la aina hii mpya ya kisonono.


  Inakisiwa watu milioni 106 ulimwenguni kote huathiriwa na ugonjwa wa kisonono kila mwaka.Ugonjwa wa kisonono pia huongeza hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa Virusi vya Ukimwi (VVU).


  “Ugonjwa sugu wa kisonono sio tatizo la bara la Ulaya au Afrika pekee bali ni tatizo la dunia nzima kwa sasa,’” alinukuliwa akisema Dk. Manjula Lusti-Narasimhan.


  Kwa mara ya kwanza, vimelea sugu vya ugonjwa wa kisonono dhidhi ya dawa aina ya cephalosporins viliripotiwa katika nchi ya Japan, ikifuatiwa na Uingereza, Hongkong na Norway.


  Wanasayansi wanaamini matumizi mabaya ya dawa aina ya antibiotiki pamoja na uwezo wa vimelea vya ugonjwa wa kisonono kubadilika na kuzoea

  mazingira mapya ndio chanzo kikuu cha kutokea kwa ugonjwa sugu wa kisonono na hivyo muda si mrefu ugonjwa huu utakuwa janga kubwa dunia

  nzima kama hatua za haraka hazitachukuliwa. Kuna uwezekano wa vimelea hivi sugu vya kisonono vinasambaa kwa sasa duniani bila kuweza

  kugundulika kutokana na nchi nyingi kutokuwa na ufuatiliaji na utunzaji kumbukumbu mzuri wa wagonjwa wake.


  Shirika la afya duniani limesema nchi zinatakiwa kuongeza ufuatiliaji wa wagonjwa wake pamoja na kudhibiti matumizi holela ya dawa za antibiotiki mpaka pale taarifa kamili za ugonjwa huu zitakapojulikana.


  “Elimu ya masuala ya kujamiana pamoja na matumizi sahihi ya mipira ya kondomu inahitajika ili kutokomeza kabisa ugonjwa huu sugu wa kisonono.

  Hatuwezi kuutokomeza kabisa ugonjwa huu bali tunaweza kuzuia usambaaji wake,”alisema Dk. Manjula Lusti-Narasimhan.

  Kwa taarifa zaidi za ugonjwa huu
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  MAGONJWA YA ZINAA - 1: (SEXUAL TRANSMITTED DISEASES)

  Kati ya magonjwa yanayoathiri watu wengi sana duniani ni magonjwa ya zinaa. Haya ni magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia vitendo vya ngono. Vitendo hivi vya ngono vinaweza kuwa kujamiana, kupiga

  denda (kissing), vitendo vya ngono kwa kutumia mdomo (oral genital sex), kujamiana kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) iwe

  kwa mwanamume na mwanamke au kati ya wanaume wenyewe na hata wale wanaotumia vifaa vya kufanyia ngono (vibrators).

  Magonjwa ya zinaa huathiri sana watu walio katika umri wa miaka 15 – 24 lakini hata kwa watu wengine ambao wana umri chini au zaidi ya huu niliotaja pia yanaonekana kwa wingi.

  Kuna magonjwa ya zinaa zaidi ya ishirini yanayotambulika duniani, baadhi ya magonjwa ya zinaa ni;

  • Kisonono (Gonorrhoea – "Gono" kama wengi wanavyopenda kuita kwa kifupi).
  • Chlamydia
  • Kaswende (Syphillis)
  • Human papilloma virus (HPV)
  • HIV/AIDS (Ukimwi/Upungufu wa kinga mwilini)
  • Hepatitis B, C, A
  • Herpes virus
  • Trichomoniasis
  • Bacteria Vaginosis
  • Pubic lice (chawa kwenye nywele za kinena)
  • Chancroid
  Magonjwa mengi ya zinaa yanatibika lakini kuna baadhi ambayo hayana tiba ya uhakika kama HPV, Hepatitis B na C, na HIV. Mengine yameanza kuwa sugu kutokana na matumizi ya dawa za antibiotics bila mpangilio, magonjwa hayo ni kama gono (gonorrhoea) na nk.


  Visababishi vya magonjwa ya zinaa


  • Vitendo vya ngono kama nilivyoeleza hapo awali
  • Kuanza vitendo vya ngono mapema au wakati wa umri mdogo
  • Kuwa na wapenzi wengi
  • Kufanya mapenzi ambao sio salama
  • Maambukizi kupitia michibuko au sehemu zilizokatika kwenye ngozi kwa kugusana na majimaji ya aina yoyote yanayotoka kwa mtu mwenye ugonjwa wa zinaa kama damu, shahawa nk. Hii inaweza kutokea bila mtu kujua kwani mara nyingi dalili za magonjwa ya zinaa zinakuwa hazionekani kwa wanawake na hata baadhi ya wanaume.
  Watu wengi huhisi kitendo cha kula denda (kissing) ni salama lakini si kama wanavyofikiria kwani baadhi ya magonjwa kama kaswende, herpes nk, yanaweza kuambukizwa kupitia njia hii. Kondomu husaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama gono, Chlamydia lakini sio kinga muafaka dhidhi ya magonjwa ya zinaa kama kaswende, genital herpes, genital warts, na magonjwa ya upungufu wa kinga mwilini (AIDS).

  Nitaanza kuzungumzia ugonjwa wa gono (gonorrhea) kwa leo na makala zitakazofuata nitakuwa nazungumzia ugonjwa mmoja baada ya mwengine


  Kisonono (gonorrhea) ni nini?


  Kisonono ni ugonjwa kati ya magonjwa ya zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Neisseria gonorrhoeae, bakteria ambao hukuwa na kuzaliana kwa haraka katika sehemu zenye unyevunyevu na joto mwilini kama kwenye shingo ya kizazi kwa

  wanawake (cervix), mirija ya kupitisha mkojo au shahawa (urethra), mdomoni na kwenye puru. Maambukizi mengi kwa wanawake hutokea kwenye shingo ya kizazi (cervix). Asilimia 75 ya ugonjwa wa gono hutokea kwa watu wenye umri wa miaka 15 – 29, wanawake walio katika umri wa miaka 15 -19 na wanaume walio katika umri wa miaka 20 – 24 wako kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu.

  Ugonjwa huu huambukizwa vipi?

  Ugonjwa huu huambukizwa kupitia vitendo vya ngono kupitia uke, njia ya haja kubwa (anus), kupitia mdomoni (oral sex).

  Ugonjwa unaweza kujitokeza kwenye sehemu za kujamiana, kwenye mdomo na kwenye puru (rectum). Ugonjwa wa gono

  huonekana sana kwa vijana, watu wenye maisha duni kiuchumi, watu wanaoishi mijini, watu weusi na watumiaji madawa ya
  kulevya.

  Dalili za ugonjwa wa kisonono


  Dalili za ugonjwa wa kisonono huanza kujitokeza kuanzia siku ya 2 hadi ya 7 baada ya mtu kupata maambukizi na huweza kuchelewa kwa wanawake. Dalili ni kama zifuatazo;

  Kwa wanaume:


  • Kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa (burning sensation)
  • Kutokwa na majimaji ya njano au meupe au ya kijani kutoka kwenye uume yanayoambatana na maumivu makali sana
  • Wakati mwengine maumivu au kuvimba kwa korodani (swollen testicles)
  • Maambukizi yakiwa kwenye puru (rectum) huambatana na maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa, kuwashwa sehemu za haja kubwa, na hata haja kubwa inaweza kutoka ikiambatana na damu, hii inatokea kwa wanaume na wanawake.
  Kwa wanawake:


  • Dalili kwa wanawake huwa si nyingi lakini wanawake wengi hawaonyeshi dalili zozote
  • Maumivu au kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa
  • Kuongezeka kwa kutoka majimaji kutoka kwenye tupu ya mwanamke ambayo ni ya njano au yamechanganyika na damu
  • Kutokwa na damu kupitia tupu ya mwanamke kabla ya hedhi kufika.
  • Kutokwa na damu baada ya kujamiana au baada ya tendo la ndoa
  • Kichefuchefu
  • Homa (fever)
  • Kutapika
  Vipimo vya ugonjwa wa kisonono


  • Swab for culture – Kipimo hiki hufanyika maabara kwa kupandikiza bakteria baada ya kufuta sehemu za siri kwa kutumia swab ili kuona kama kuna bakteria wanaosababisha gono.
  • Polymerase Chain Reaction (PCR) – Kipimo cha kuangalia vina saba (DNA) ya bakteria, ni ghali sana.

  Tiba ya ugonjwa wa kisonono ni nini?


  Tiba ya gono inahusisha na tiba ya ugonjwa wa Chlamydia kwani mara nyingi magonjwa haya huambatana kwa pamoja.Tiba hutegemea na umri wa mgonjwa na kama mtu ni mjamzito au la. Tiba ya gono ambayo sio sugu iliyo kwenye shingo ya kizazi

  (cervix), urethra na puru, dawa zinazotumika ni aina za cephalosporin dozi moja pamoja na dawa za aina ya macrolide

  antibiotics (mfano azithromycin) na za jamii ya penicillin (mfano doxycyclin) ili kutibu ugonjwa wa chlamydia. Mara nyingi kwa

  wale chini ya miaka 18 na wanawake wajawazito, hutibiwa kwa kuchomwa sindano. Fuata ushauri wa daktari kabla ya kutumia
  dawa hizi kwani dawa nyingi zina madhara kwa wajawazito (mfano doxycyclin). Ushauri nasaha hutolewa kwa wapenzi wote wawili na ni vizuri wapenzi wote wawili kutibiwa hata kama mmoja hana dalili za ugonjwa huu.

  Madhara ya ugonjwa wa kisonono  • Kutoweza kuzaa kwa mwanamke (tasa) au kutoweza kutungisha mimba kwa mwanamume (infertility)
  • Huweza kuathiri moyo (heart valves), ubongo,ngozi nk ambayo ni hatari sana kwa mtu yoyote.
  • Madhara kwenye sehemu za maungio au jointi (joint inflammation)
  • Kwa wanawake wale ambao hawajatibiwa wanaweza kupata ugonjwa wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) ambao huongeza asilimia ya mwanamke kuwa tasa.
  • Wale wanawake ambao ni wajawazito na wameambukizwa gono wako kwenye hatari ya mimba kutoka au kuzaa mapema kabla mimba haijatimiza umri wake (preterm labor).
  • Kwa wale wanaoambukizwa gono kipindi cha kukaribia kujifungua, wanaweza kuwaambukiza watoto wao na hivyo watoto kupata ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis), kuwa kipofu (blindness), homa ya mapafu (pneumonia) na ugonjwa wa mifupa (septic arthritis).

  Kinga ya kisonono  • Kutumia kondomu wakati wa kujamiana
  • Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
  • Kuacha vitendo vya ngono kama matumizi ya vifaa vya ngono hasa kwa wanawake mfano vibrators nk.
  • Kwa wanawake wajawazito – Hakikisha unahudhuria kliniki mapema ili upate kuchunguzwa na kupatiwa tiba muafaka kama utagundulika na ugonjwa wa gono au ugonjwa mwengine wowote.
  • Wanawake wajawazito wanashauriwa kujifungulia hospitali ili kama mtoto ameathirika na gono apate matibabu ya haraka baada ya kuzaliwa kuepusha kuwa kipofu.
  • Epuka kufanya ngono na mtu aliyeambukizwa gono.

  "Kumbuka ya kwamba hakuna kitu kama ngono salama kwani huwezi kujua kama wewe au mwenzako wakati wa kujamiana ameathirika au la, au una michibuko au umekatika kwenye ngozi au la kwani michibuko mengine inaweza isionekane au

  kugundulika kwa urahisi. Njia pekee na nzuri ni kuacha au kujikinga na vitendo vya ngono". Mtu aliyepata gono awali anaweza kupata tena.
  Magonjwa ya Zinaa - 1: (Sexual Transmitted Diseases)  [​IMG] [​IMG]
   
 3. k

  kisukari JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  mmh,yanatisha.thanks mzizi mkavu
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  tobaaaaaaaaa
   
 5. Sibhonike

  Sibhonike Senior Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Somo zuri.
  Asante Mzizi.
   
 6. sister

  sister JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,027
  Likes Received: 3,933
  Trophy Points: 280
  kazi ipo.
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu asante sana kwa somo hili na tahadhari pia
  halafu mbona hukunijibu mkuu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Sikukujibu kitu gani?kwani umenitumia PM.?mkuu Mr Rocky nitumie tena basi hiyo PM.
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu nilituma pm aise
  Ngoja niitume tena mkuu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. M

  MWAKIKALI Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  shukrani Rocky kwa taarifa, UGONJWA HUO UMEENEA SANA MAENEO YA MKOA WA KAGERA HASAHASA KARAGWE, RAFIKI ZANGU WENGI SANA WAMEUGUA NA UPONAJI WAKE SI WA UHAKIKA MAANA WANASEMA WAKITIBU NA KUPONA HUWA UNAJIRUDIA BAADA YA SIKU TATU HADI NNE MARA BAADA YA KUMALIZA DAWA.
  MMOJA ALIPEWA DAWA ZA AINA TATU KWA WAKATI NA SINDANO NDO KIDOGO YEYE HAUJARUDI.
   
 11. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,750
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Ahsante Mzizimkavu!
   
 12. ERIC JOSEPH

  ERIC JOSEPH JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  thanks xo much 4education
   
 13. cement

  cement JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 583
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nakukubali kaka katika hili!
   
 14. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Madaa nzuri pongezi sana ubarikiwa
   
 15. siralola

  siralola Member

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Somo zuri sana doctor asante kwa kutujuza.
   
 16. m

  manushiboy Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu akupe nguvu uendelee kuelimisha watu wake asante sana mkuu
   
 17. snug

  snug Member

  #17
  Sep 14, 2013
  Joined: Aug 8, 2013
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajua ni sindano gan na ni dawa gan izo alipewa
   
 18. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #18
  Sep 14, 2013
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  sister si mmekataliwa kuingia kwenye uzi huu?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. sister

  sister JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2013
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,027
  Likes Received: 3,933
  Trophy Points: 280
  si unajua binadam tulivyo wagumu kile tunachokatazwa ndicho tunachokifanya....
   
 20. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #20
  Sep 14, 2013
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Aiseeeee, nimeipenda hii
   
Loading...